JK Ampeleka Augustino Mrema kutibiwa India?

JK Ampeleka Augustino Mrema kutibiwa India?

Mrema apelekwa India kwa matibabu, Kalembo akimbizwa hospitali
broken-heart.jpg
*MKUU WA MKOA TANGA AISHIWA NGUVU NA KUKIMBIZWA HOSPITALI

Mashaka Kibaya, Korogwe na Boniface Meena

WAKATI mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema yuko nchini India kwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari, mkuu wa mkoa wa Tanga, Meja Jenerali Said kalembo aliishiwa nguvu akiwa ziarani na kukimbizwa hospitalini.

Mrema, ambaye aliondoka wiki iliyopita, atakuwa akitibiwa Hospitali ya Appollo iliyo jijini Bambay.

Kaimu katibu mkuu wa TLP, Hamad Tao alisema Mrema amekwenda India ili kukutana na wataalam wa ugonjwa huo.

"Amekwenda tangu wiki iliyopita na atakaa huko kwa wiki tatu ili wataalam waweze kumpatia matibabu,"alisema Tao.

Alisema kuwa huo umekuwa ni utaratibu wa Mrema, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kwenda India kutibiwaugonjwa huo ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda sasa.

Alisema kuwa Mrema anagharimia mwenyewe matibabu yake na kwamba hatumii fedha za TLP.

"Amejigharimia mwenyewe na si TLP iliyomgharimia... amebakiza wiki mbili za matibabu kabla hajarejea nchini," alisema Tao.

Wakati huo huo, mkuu wa mkoa wa Tanga, Meja Jenerali Said Kalembo jana alikatiza ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri ya Korogwe baada ya kuugua ghafla.

Kalembo alijisikia vibaya akiwa ukumbi wa halmashauri majira ya saa 3:00 asubuhi na alionekana kuhisi kizunguzungu na hivyo kuinamia meza kwa muda, lakini baadaye alipata nafuu na kuendelea kuzungumza na watendaji wa halmashauri hiyo.

Kalembo aliendelea na ratiba na kuelekea kwenye mradi wa maji ambako hali yake ilionekana kubadilika na akaanza kupepesuka na hivyo kusaidiwa kuingia kwenye gari lake na mkuu wa wilaya ya Korogwe na baadaye akarudishwa hoteli ya Motel White Parot alipofikia kwa mapumziko.

Mganga mkuu wa wilaya ya Korogwe, Dk Rashidi Said na mwenzake walifika hotelini hapo kumpatia huduma ya kwanza na kuongezewa maji.

Baadaye Kalembo alitolewa hotelini hapo akiwa ametundikiwa dripu na kuingizwa kwenye gari lake kupelekwa Hospitali ya Bombo, Tanga. Tukio hilo lilionekana kuwachanganya viongozi wa wilaya hiyo.


Chanzo Mwananchi.


Hii sasa kali tumwamini Bwana Tao au kiranja.Wakati mwingine kudandia maneno ya mitaani si vizuri tafadhali Mkuu kiranja omba radhi jamvi kwa kuleta habari za mitaani
 
ukisoma gazeti la mwananchi la leo....kiongozi mmoja wa TLP amedai mrema yuko india kwa matibabu ambayo amejigharamia mwenyewe.... ukweli uko wapi sasa...(ila kwa jinsi yule mzee alivyofuliwa i doubt kama amejilipia kweli... we mpaka ss hv anakaa nyumba ya chama(habari za kuaminika )


wanasema sio mara yaa kwanza kwenda kujitibia nje[ukisoma gazeti]....

infact mrema sio kwamba pesa ya kutumia na familia yake hana....kwani hata watoto wake anawalipia karo shule nzuri tu.....na kuna ambao wapo nje ..ie ujerumani,uingereza na south africa.....
 
Ngongo said:
Sheikh Yahaya Hussein anastahili kugharamiwa matibabu na serekali kwasababu ni mtu wa system.Umewahi kusoma The dark side of Nyerere by Ludovick S Mwijage ungetambua Tanzania ni zaidi ya unavyoijua.

Ngongo,

..kuwa mtu wa system isiwe kigezo cha upendeleo.

..mwisho wa siku tunaweza kuhalalisha mambo mengi sana ya ajabu kwasababu tu mhusika ni mtu wa system.

..tunachosisitiza hapa ni kwamba uwekwe utaratibu wa wazi na unaoeleweka wa wananchi kuweza kutibiwa nje ya nchi.

..kwa hali ilivyo sasa hivi tunaona kwamba nafasi za kutibiwa nje zinapatikana kwa wakubwa wachache na kwa njia za kujuana-juana.

..hii nchi imejengwa kwa misingi ya USAWA.

NB:

..asante, nitakitafuta kitabu cha Ludovick Mwijage.
 
Mrema amerejea jana kutoka India na anatarajia kukutana na waandishi wa habari jumatau ofisi kwake kuelezea safari yake.
 
La Mrema kwenda kutibiwa India si jambo geni, kwa watanzania; kwani ni watu wengi wamekuwa wakipelekwa kwa gharama za serikali kutibiwa nje ya nchi, hata wale wambao hawana majina makubwa.Wengine wanaenda kwa kujigharamia wenyewe.Kama Mrema kalipiwa na serikali ni haki yake kama mtanzania mwingine anavyoweza kulipiwa.
 
Siasa haina maana ya uhasama! Fikra ya kujipendekeza ama kupendeleawa ni mitizamo tu, maana ninaamini Mrema siyo mwanasiasa wa kwanza kupewa msaada wa matibabu na Rais.
 
Watu wengi wanakwenda India kutibiwa na hili la Mrema si la kwanza. Je amelipiwa na JK, inawezekana iwe hivyo na pia inawezekana kabisa iwe ni ubunifu tu wa wanaodai hivyo. Kama kweli JK ametowa pesa zake kumlipia ingenishangaza sio kwa kuwa hiyo si fadhila njema bali kwa kuwa serikali inayo mipango kama hiyo kuwasaidia hasa viongozi na hata raia wa kawaida wanaostahili. Ni dhana yangu kuwa kama Mrema, ndugu na marafiki wake hawakumlipia basi itakuwa ni serikali iliyofanya hivyo. Na kama kweli JK ametowa pesa zake mwenyewe kumsaidia Mrema basi sina budi kumpongeza JK kwa imani hiyo na Mwenyezi Mungu amuwezeshe zaidi asaidie wengi wengine.
 
Mwenyekiti wa TLP Bw Augustino Lyatonga Mrema amekanusha vikali kupelekwa India na JK kutibiwa ugonjwa unaomkabiri wa kisukari. Aidha, Waziri wa Mambo ya ndani na "Naibu Waziri Mkuu" wa awamu ya pili amesema bayana kuwa hajafikia hatua ya kuwa ombaomba kiasi hicho. Swali kwa wanaJF, je, madai ya kupelekwa mzee wa kiraracha India na Mkulu ni uzushi kama tulivyojadili humu jamvini?
 
Mulongo mkubwa, haaminiki, hana lolote, anaweweseka, anajionea haya, vipande vya pesa vimemuondolea hekima yake na ujasiri wake....shame on him.
 
Mwenyekiti wa TLP Bw Augustino Lyatonga Mrema amekanusha vikali kupelekwa India na JK kutibiwa ugonjwa unaomkabiri wa kisukari. Aidha, Waziri wa Mambo ya ndani na "Naibu Waziri Mkuu" wa awamu ya pili amesema bayana kuwa hajafikia hatua ya kuwa ombaomba kiasi hicho. Swali kwa wanaJF, je, madai ya kupelekwa mzee wa kiraracha India na Mkulu ni uzushi kama tulivyojadili humu jamvini?

Yasije yakawa yale ya RA na rafiki yake Mtikila!
 
Mrema kutibiwa hi haki yake kama mwananchi na hasa ukizingatia mchango wake katika nchi hii. Siyo favour ya JK ni kwamba JK ameona umuhimu huo. Alimlipia saidi kubeneya sembuse MREMA?
 
Back
Top Bottom