JK Ampeleka Augustino Mrema kutibiwa India?

Lakini ni binadamu kama binadamu wengine hivyo kama Jk ameamua kulipa Gharama za usafiri ni vizuri tu hakuna shaka kabisa
 
Hii ni haki yake kutibiwa,amelitumikia taifa hili kwa uaminifu sana. Leo hii kupelekwa kwake nje kutibiwa watu wanataka kujizolea sifa.

Nchi hii tunapenda sifa zisizo na msingi kabisa,sasa kama Rais kampeleka binafsi pia ni jambo jema lakini asije akawa anafanya hivyo ili kulipwa fadhili kwani mrema kama Naibu waziri mkuu wa Zamani anastahili hayo yote.

Sijui Ni lini tutaendelea!
 

Ndugu kizomanizo

I think this is your first post cant you say Hello to your fellow members please or it doesnt matter!
 
Hata kama ni serikali, mbona wengi wanapelekwa nje kupitia wizara ya afya?
Kwani Mrema ndiyo inakuwa kuna jambo nyuma?
Kuwe na jambo (string attached) au hakuna Mrema anastahili kutibiwa na serikali. Alishakuwa naibu waziri mkuu na amefanya kazi nyingi kwa wananchi wa "inji" hii.
Tunamatakia matibabu mazuri apone haraka!
 
Aende tu akatibiwe. After all Mrema na Kikwete wako renki moja...wote ni wenyeviti wa Chama
 

Mtu B,
Hiyo foleni ya kwenda kutibiwa nje isiyoeleweka nani yuko mbele na nani anafuatia ndio inayoleta hisia ya matibabu kutumika kama hongo au kuwepo kwa wananchi walio bora zaidi kuliko wengine.

Mrema ana haki ya kutibiwa lakini ingekuwa vema waTZ wakafahamishwa na wao wakiugua watasaidiwaje maana nchi itakapodaiwa deni litakuwa ni la kwetu wote?
 

That's the plight of the majority who, unfortunately, are not in a position to attract the attention of their government or JK. Motives aside, JK funding of the medical care of Mzee wa Kiraracha on its own cannot elicit annoyance. But note that Mrema just got lucky whatever the circumstances. 🙁
 
Acha utani wakati ndugu huyu anaumwa,
 
Hii taarfa yako haijakamilika.
nina mashaka na soucre yako.
 
Taarifa yako haijakamilika.
Nina mashaka na source yako.
 
Hivi amempa shilingi ngapi ($??) kwa ajili ya matibabu hayo?
 
Amelipiwa gharama zote na JK ,na hapa sisemi kuwa ni serikali no. Ni JK personaly ndio amelipia gharama zote kuanzia tiketi ya ndege hadi matibabu yake yote akiwa huko.

Ameonyesha uungwana kuokoa maisha ya binadamu mwenzake. Abarikiwe.😀
 

acha cheap conclusion na kusema vitu visivyo practical, nimekuuliza je sisi wananchi wangapi wangekuwa tayari kumlipia gharama za matibabu Mrema? umesema anatakiwa kuwa mwaminifu mpaka kufa!!! yaani yeye afe kwa jina la kuwa mpinzani? kwani anawasaidia nani? huoni kuwa msemo wako dio uliomfanya basi ajikombe kwa JK(kwa maneno yako)? na msemo wako huu ndio unawafanya wapinzani wengi kutokuwa waaminifu! kama mwananchi mwenyewe ni wewe!!

To my side, I do believe Mrema angesaidiwa na serikali hata kama asingemfagilia JK, Mrema usimfananishe na wewe.By the way kwa conclusion yako vipi kuhusu Kubenea si naye alipelekwa na JK? Unasemaje sasa kuwa mwanahalisi ni la JK?-I do believe so but on on the ground ya kuwa Kubenea alipelekwa India!

acheni utani na kifo jamani!!
 

JK na Mrema,ni kama chanda na pete no body can watenganisha them
 
haya ni majungu Mtu yeyote aliyewahi kuwa na cheo cha katibu mkuu au zaidi anatibiwa na serikali hivyo si JK bali ni serikali.
 
Ni vizuri kuwa na Mkuu wa Nchi kama JK anayeona huruma kwa raia wake aliye na ugonjwa usiotibika nchini, halafu akamgharimia binafsi kumpeleka nje kutibiwa.

Ingekuwa ni jambo la kutukuka kama huruma hii ingesimikwa nchini ili Watanzania wajue kuwa endapo watapatikana na bahati mbaya kuugua ugonjwa unaoweza kutibiwa nje tu, basi watapelekwa huko kwa matibabu. Kutibiwa nje na Serikali, sio tu fedha za kodi yetu zinatumika, bali hata akiba yetu ya fedha za kigeni zinatumika.

Kutumika kwa fedha za kigeni kunapungaza uwezo wetu kitaifa wa kununua madawa toka nje na vifaa vingine muhimu kwa maendeleo na ustawi wa umma kwa jumla. Kwa hiyo inafaa kuwe na utaratibu unaoeleweka na wa wazi, badala ya huduma kama hiyo kutolewa kama zawadi au hongo kwa kupigia viongozi kampeni za kisiasa.
 
Huyo anayeitwa JK ni Wizara ya afya au ni mtu binafsi. Mbona ni wengi wanapelekwa India na hatusemi JK kawapeleka. Sifa za bei nafuu.

Kuna haja ya kuwa na Wizara ya afya? Matibabu yote naona sasa hivi ni India.

Napendekeza Wizara ya afya ifutwe.
 
Mzee Mrema amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu sana; amehitaji matibabu kwa muda mrefu. Hivyo kupatiwa matibabu haya kwa msaada wa mtu yeyote siyo jambo la kubeza bali la kuunga mkono na kushukuru. Kama Mrema angeomba asaidiwe michango ili apelekwe nje kutibiwa nina uhakika wa asilimia kubwa kati yetu tutakaa pembeni na kuombea wengine wachangie!

Of course kuna politics behind but that is irrelevant. Kwa kumsaidia sasa hivi JK amehakikisha kuwa Mrema kamwe hawezi kusimama against him in an election.. now that is the story behind the story.. .. you do this, we will do that.. isn't that what quid pro quo is? Mrema did his part for JK, and JK has just returned the favor.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…