Jk aongoza maziko ya shekh yahya hussein

Jk aongoza maziko ya shekh yahya hussein

sio waislamu wote wenye tabia hizo za kufuga majini nma kuyanyenyekea,mamangu muislamu na hana tabia hizi ni wachache kama marehemu na wafuasi wake kina maalim juma ndio wanaowachafua wenzao na maushirikina yao
Msinichukie bila sababu mwenzenu!!!
Taaluma hii haifundishi uovu...bahati nzuri hata katika ilmu ya dini naielewa kiasi changu Alhamdulillah!
Nimeona/kusoma vyombo vya habari madaktar wakifanya kinyume cha maadili yao...lakini hakuna wanaowasusa madaktari.
Wanasiasa si wote ni wasafi lakini hawajachukiwa wote.
So it's better kuheshimu mtu/watu ambao hujamuuliza/hujawauliza hayo unayoona ni makosa.
Nakaribisha maswali mbali mbali niyajibu....ili ujue niko vipi katika taaluma hii.
Namkubali sana Marhuum Shaykh Yahya.
 
nazani ni technic yao tu-ni sawa na prezdaa wetu ambavyo idadi ya watoto wake nayo ni utata mtupu
 
Jamani eti hata Mzee wa upako Antony Lusekelo anamsifu Yahya makubwa
Tena alisema alimuota kabla ya kifo chake kabla ya siku tatu....sijui alimaanisha nini?
Kwa kawaida ndoto inahitaji tafsiri yake.
Mbona hakuelezea kama aliota kabla ya tukio?!!.
 
nyie watu wa humu vpi!! huo mgawanyo wa ilimu kila mtu anaujuzi wake hapa duniani'shekhe yeye ni mtu wa nyota kama marehemu''pole ustaadh kila nafsi itaonja umauti''walikuwepo wakapotea hata sisi tutakwenda na wengime watakuja''R I P shekhe husein yahya babu yetu''kuna watu umewasaidia sana.
 
Pole maalimu, kila nafsi itaonjoa mauti. Mwenyezi Mungu akupe moyo wa subira.
 


May 22nd, 2011


http://mohammeddewji.com/blog/wp-co...-kwa-Marehemu-Magomeni-Mwembe-chai-Mei-22.jpg
Rais Kikwete akipokewa na Hassan Yahya Hussein, Mtoto mkubwa wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein alipokwenda kuhani msiba wa mnajimu huyo maarufuf nyumbani kwa Marehemu Magomeni Mwembe chai leo.

Rais Kikwete ana Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein walikoenda kuhani msiba wa mnajimu huyo mashuhuri Magomeni Mwembe Chai leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akibadilishana mawazo na viongozi wa dini kabla ya kuwasili kwa mwili wa aliyekuwa Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein katika makaburi ya Tambaza jijini Dar. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadiki.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akisikiliza mawaidha wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein aliyefariki dunia jana jijini. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki.

Mwili Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein ukisubiri kushushwa kaburini tayari kwa maziko.


Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mtoto wa mwisho wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein aliyezikwa leo katika makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki kumzika Mnajimu Mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati.

Mziwanda wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein akitia udongo kwenye kaburi la baba yake wakati wa mazishi.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Suleiman Kova akishiriki Mazishi ya Sheikh Yahya Hussein aliyezikwa leo Alasiri jijini Dar.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia uratibu na uhusiano Mh. Steven Wassira akishiriki katika mazishi ya Mnajimu Mashuhuri wa Afrika ya Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein.

Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa Mh. Nape Mnauye akishiriki katika mazishi ya Sheikh Yahya Hussein.

Mwili wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein ukiswaliwa nyumani kwake kabla ya kuelekea makaburini.


Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akiwasili nyumbani kwa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.

Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mh. John Cheyo akitoa wasifu wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.

Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof. Ibrahim Lipumba akitoa wasifu wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.

Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akitoa wasifu wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.

Mamia ya waombelezaji wakisiliza mawaidha nyumbani kwa marehemu Sheikh Yahya Hussein.

Wakinamama wakionekana na huzuni kubwa ya kuondoka kwa kipenzi cha wengi Sheikh Yahya Hussein.

Kinamama wakilia kwa uchungu msibani.


Msafara wa kuelekea makaburini ukiongozwa na mapikipiki.

Umati wa waombelezaji ukielekea makaburini.
 
kufa kila mtu atakufa, na si vyema kumhukumu aliyetangulia. Kwani uzima ni wa Mungu na kifo ni kazi yake. Kuhusu kuanguka kwa jk cdhani ni vyema kuhusisha na ushirikina, kwani hata Dr Slaa alianguka, na akavunjika na mkono, na hiyo tuiteje?, sihani kama tutakuwa tunaendeshwa na hisia na kuropoka itatufikisha kwenye ukombozi na ushawishi tunaoutaka. Wafaham kama mbowe alikuwepo kwenye msiba? Jiulize Sheikh yahya nani asiyemfaham ? Siasa ni watu. Usitoe maneno ya kuwafanya baadhi ya watu watilie shaka mtazamo wako.

Hapo kwenye red, sawa kabisa... Huko kwengine hakunihusu...!
 
Inaelekea alikuwa si mchezo huyu mzee,waombolezaji wengi wanaonekana wakiwa na huzuni ya kiukweli,hata hao viongozi wa vyama vya siasa wanaonekana wana huzuni kweli kweli,i wonder nani ataachiwa mikoba kati ya hao watoto wake.
 
Inaelekea alikuwa si mchezo huyu mzee,waombolezaji wengi wanaonekana wakiwa na huzuni ya kiukweli,hata hao viongozi wa vyama vya siasa wanaonekana wana huzuni kweli kweli,i wonder nani ataachiwa mikoba kati ya hao watoto wake.

Mtoto aliyempokea Rais Kikwete picha ya Juu Hassan ndie aliyechukua hiyo mikoba - nasikia huyo kijana ni CHADEMA...
 
Moja kati ya sifa nyingine ya Marehem ambayo wasio waislam hawaijui ni kuwa Marehem alikuwa ni mooja kati ya wasomaji wakubwa sana wa wa Qur'an na kuna kipindi alishinda mashindano ya kusoma huko Cairo. Ilibidi washindani wake waingine mitini

Ama kweli msikiti wa Mtoro na K tea shop ya mtaa wa Chagga watakumisss
Inallillahi wa Inna Illahi Raj'uun
 

Mamia ya waombelezaji wakisiliza mawaidha nyumbani kwa marehemu Sheikh Yahya Hussein.

Wakinamama wakionekana na huzuni kubwa ya kuondoka kwa kipenzi cha wengi Sheikh Yahya Hussein.

Msiba wa Shehe Yahaya umekusanya watu wengi kuliko mikutanao ya CCM magamba!
 
hivi kwanini wasingemzika na mkw'ere humohumo, agggghrrrrr nikiona picha ya mkwer'e nahisi kutapika
 
Back
Top Bottom