JK apangua makatibu wakuu

JK apangua makatibu wakuu

Mwandishi Wetu
Daily News; Saturday,November 29, 2008 @18:01

Mgonja wa Hazina aastafu

Mmoja wa makatibu wakuu waliofanya kazi kwa muda mrefu, Gray Mgonja...Kutokana na kustaafu kwa Mgonja na wenzake watatu

Wamestaafu Makatibu wakuu watatu, na yeye ni mmoja tu kati ya Makatibu Wakuu waliofanya kazi muda mrefu, na mwandishi kasema hilo, sasa kwa nini Mgonja ndie kichwa cha hii habari ?

Kuna kitu maalum kuhusu tambala ( historia, rekodi, visa ) vya career ya Mgonja ambavyo mwandishi anataka lakini anashindwa kuvisema. Anaogopa kuandika "Mgonjwa amekuwa akihushwa na tuhuma mbali mbali za ufisadi." !!!

Kwa sasa, Mgonja ambaye yuko katika likizo ya kustaafu, amestaafu...

"Likizo ya kustaafu" ndio kitu gani hicho ? Kuna mtu ameshawahi kusikia mpango wa "likizo ya kustaafu" ?

Mwingine ni Seti Kamuhanda anayekwenda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Awali alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba) Ikulu;

Hapa naona January Makamba kapona, au hii sio kazi yake ya sasa na yeye ?

... rais amemhamisha Naibu Katibu Mkuu Fanuel Mbonde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu.

Umesemaje mwandishi ?

Daily News bwana !
 
Sasa Mkuu FMES huoni kwamba mambo kama haya kama aliyajua kusubiri mpaka Paris ni kuchemsha? Na kwamba serikali ikiwa viwanja huko kunatakiwa collective responsibility?

Alikuwa wapi wakati mipango hii inapitishwa na kuwa adopted kusubiri mpaka ughaibuni kusema hivi?

- Sawa sawa unavyosema, lakini katika perfect political system za huko majuu sio bongo, ambako Professor Sarungi bingwa wa kutibu mifupa anaweza kuwa waziri wa uilinzi.

- Muungwana alikuwa foreign huyu sister alikua Hazina, kwa kawaida foreign huwa wanaamini wanajua sana kuliko sekta zote za serikali bongo, kwa hiyo huwa hawakubali ushauri wa mtu yoyote, ndio maana huyu sister aliamua kumtolea uvivu bosi wao huko huko majuu.

- Halafu hizi huwa ni kawaida sana wakulu wetu wanapokwenda nje kwenye mikutano ya kimataifa, sometimes hata hotuba ya kiongozi huwa wameisahau bongo! Kuna wakati waziri anakwenda kwenye mkutano wa wakurugenzi na kuishia kurudishiwa mlangoni!
 
- Sawa sawa unavyosema, lakini katika perfect political system za huko majuu sio bongo, ambako Professor Sarungi bingwa wa kutibu mifupa anaweza kuwa waziri wa uilinzi.

Dr Florens Turuka kuwa katibu mkuu wa utamaduni na michezo ni kumpoteza huyu mshikaji bure, jamaa ni kichwa sana na hana hata chembe ya ufisadi. Ana doctorate ya micro-economics jamaa akiwa chuoni alikuwa hapendi kabisa michezo !!!! kwanini Muungwana asingempa wizara ambayo angeweza kutumia shule yake ipsavyo?
 
Naona kuna makosa yalitokea wakati nina post, naomba mniwie radhi na pia naona kuna mtu mwingine kasha post habari zinazofanana na nilizotaka kupost zenye kichwa cha habari "Mgonja wa Hazina aastafu"
 
... rais amemhamisha Naibu Katibu Mkuu Fanuel Mbonde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kuhani,

My understanding is, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, kuna Ofisi ya Waziri Mkuu (proper -Waziri Pinda) na pia kuna Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa (TAMISEMI - Waziri whoever is the current Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI).

Kwa hiyo mtu kutolewa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu (proper) technically ni kutoka Wizara moja kwenda nyingine.
 
Dr Florens Turuka kuwa katibu mkuu wa utamaduni na michezo ni kumpoteza huyu mshikaji bure, jamaa ni kichwa sana na hana hata chembe ya ufisadi. Ana doctorate ya micro-economics jamaa akiwa chuoni alikuwa hapendi kabisa michezo !!!! kwanini Muungwana asingempa wizara ambayo angeweza kutumia shule yake ipsavyo?

Kwa kutumia Keynesian na Adam Smith Principles, Turuka atahkikisha Michezo, Utamaduni na habari zitabadilika mwendo kama zile grafu za supply na demand, M1 mpaka M3 na kwisha kuongeza GDP na GNP za Taifa!
 
On the second note, Dr. Turuka inabidi aachane na ungini na kufahamu AliKiba ni nani, ajuwe Ze Comedy ili awe na furaha na akikaa sambamba na Micho na Maximo, atakuwa shabiki wa Yanga!
 
Bora Blandina Nyoni na Shamsa Mwangunga wametengenishwa maana ilikuwa kama Baghdad kila siku kunafuka moshi
 
kwa heri mgonja...tutakutana kisutu!!!!
 
Mgonjaaa ajipange kwenda kunyea ndoo!It is time...........afu the rest you know!
 
- Wananchi angalieni another scenario inayotembea mjini leo sina uhakika na ukweli wake, inasema hivi:-
kulikuwa na vikao vya siri vya kamati za el kugombea urais vilivyokuwa vikifanyika katika hotel ya mzee mmoja mjini anayeitwa Msiba. vikao hivyo vilikuwa vikiongozwa na mramba. na leo mtoto wa mramba ameolewa na mtoto wa huyo msiba. kwamba harakati zimewaka moto za 2010 kwa sababu makubaliano ya mtandao yalikua muungwana atawale term moja tu amuachie el lakini sasa anaonekana kukiuka makubaliano.
 
Rutabanzibwa fisadi bado yumo tu, na sasa anakwenda kuonana na Fisadi mwingine MASHA. Mmmh Kikwete una shughuli kaka.

Kwa Rutabanzibwa kumwita fisadi nadhani ni mapema mno na twaeza mwonea.The man is a fearless fighter wa ufisadi.Alipigana kufa na kupona kupinga mikataba mibovu ya IPTL lakini akazidiwa nguvu na mafisadi.

Binafsi namheshimu kama mtu mwenye msimamo asiyependa rushwa kabisa na wala hana mpango nayo,mchapa kazi na asiyeyumba akiamua kusimamia kitu.labda awe alibadilika hapo katikati maana binadamu aweza geuka awapo safarini akaacha kuangalia mbele aendako akageuka nyuma kukumbatia kusalimiana na kula na mafisadi.

Kwenye kundi la mafisadi walioko sasa Rutabanzibwa nawaza kumtoa.Sina uhakika sana kama niko sahihi au siko sahihi lakini nafikiria nimtoe kichwani mwangu kwenye kundi la mafisadi ninaowawazia.
 
- Wananchi angalieni another scenario inayotembea mjini leo sina uhakika na ukweli wake, inasema hivi:-
kulikuwa na vikao vya siri vya kamati za el kugombea urais vilivyokuwa vikifanyika katika hotel ya mzee mmoja mjini anayeitwa Msiba. vikao hivyo vilikuwa vikiongozwa na mramba. na leo mtoto wa mramba ameolewa na mtoto wa huyo msiba. kwamba harakati zimewaka moto za 2010 kwa sababu makubaliano ya mtandao yalikua muungwana atawale term moja tu amuachie el lakini sasa anaonekana kukiuka makubaliano.

Mkuu hii habari nzito hii, sijui ita turn out vipi.
 
Kwa kutumia Keynesian na Adam Smith Principles, Turuka atahkikisha Michezo, Utamaduni na habari zitabadilika mwendo kama zile grafu za supply na demand, M1 mpaka M3 na kwisha kuongeza GDP na GNP za Taifa!

Mkuu sidhani kwa jinsi ufisadi ulivyokithiri nchini laws za Money supply zinafuatiliwa katika nchi yetu. Hiyo M0, M1, M2, M3 nafikiri ilisharukwa zamani ambapo watu binafsi kama akina Mzindakaya, waliweza kuruka chain na kwenda reserve kuchukua personal loans, ambayo ali i default. Huo ni mfano mmoja mdogo tu. The same applies to all who are now convicted with EPA.
Hivi experts wa uchumi pale BoT wana dermine vipi money cirlculation wakati kuna large amount of money zinatoka kinyume cha sheria tena kwa usiri mkubwa, and these large sums are supposed to be unaccounted for? How are they able to determine the real GDP of the country?
 
Dr Florens Turuka kuwa katibu mkuu wa utamaduni na michezo ni kumpoteza huyu mshikaji bure, jamaa ni kichwa sana na hana hata chembe ya ufisadi. Ana doctorate ya micro-economics jamaa akiwa chuoni alikuwa hapendi kabisa michezo !!!! kwanini Muungwana asingempa wizara ambayo angeweza kutumia shule yake ipsavyo?

Kwa system ya Tanzania, hata uwe kichwa vipi bure, maamuzi yote lazima kikao!!

Kuna watu wanauwezo mkubwa sana, tena wakutoa maamuzi mazito hawajiamni, wanasubiri ('collective responsibilities') - maamuzi yatolewe na kikao.
 
Wizara ya Mali Asili na Utalii ni nyeti mno. Inatakiwa Katibu Mkuu aliyesomea mambo hayo. Katibu mkuu ni kama engine, anatakiwa ajue utendaji wote kwa ajili ya kumshauri Waziri. Mawaziri ni watekelezaji wa Sera, na huwa wanahamishwa mara kwa mara.

Najiuliza je hao makatibu wakuu wote katika wizara zote wanafahamu utaalam au shughuli nyeti za kiutendaji au wataanza kujifunza kwa Makamishna na wakurugenzi tena?
Hii ni Shida ndo maana maamuzi yanachukua muda mrefu sana kutekeleza au kuchukuliwa. Bureaucrasy ni kubwa sana.Hata mtu akituma barua au email (barua pepe) itachukua muda mrefu sana kujibiwa tofauti na Mashirika au makampuni Binafsi.
Tanzanian we act and perform to slowly that is why we are behind our Colleagues Kenya.

I don't know if this is Ujamaa effect or what?????
 
Dr Florens Turuka kuwa katibu mkuu wa utamaduni na michezo ni kumpoteza huyu mshikaji bure, jamaa ni kichwa sana na hana hata chembe ya ufisadi. Ana doctorate ya micro-economics jamaa akiwa chuoni alikuwa hapendi kabisa michezo !!!! kwanini Muungwana asingempa wizara ambayo angeweza kutumia shule yake ipsavyo?

Kwanini nayeye asikatae kama si kutanguliza masirahi yake mbele...Wabogo bwana kila m2 anaangali tumbo lake zaidi...
 
Back
Top Bottom