JK Hatembei na Fuko La Fedha

Ile siasa yetu ya kujitegemea tumeicha wapi? Au ilikuwa ni wimbo tu, rais anaenda nje kuomba na wananchi wanamuomba rais!

Inawezekana kabisa kuwa raia walifanya makosa kumuuliza mkuu aina hilo la swali.Lakini kuna namna ya kujibu kiasi cha kuwafurahisah watu, pia kuna namna ya kudela na viongozi wa chini.Kwani inaonyesha hawana vikao vya mara kwa mara.Maswali haya yanaonyesha pia kuwa wananchi pamoja na wabunge wao wamekata tamaa.

Shule au miradi mingi kweli inafanywa na wananchi wenyewe serikali ni kuongeza nguvu haijalishi miradi hiyo ni mikubwa au midogo kiasi gani.WATANZANIA WANAPASWA KUPEWA FARAJA HATA YA MANENO TU!
 
Mbona nahisi kama kuna mtu/watu wamedekezwa!?

Upo Right kama hisia zako na zangu ziko sawa ni kwamba. Hawa jamaa wamezoea kila kitu Siasa tu, Rais atoe mchango kinyume na taratibu za Fedha mradi tu ionekane ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani Ya Chama. Na hasa mbunge alitaka kujionesha kuwa yeye yupo karibu na Mkuu wa Nchi ili 2010 apate ubwete.
 
Subirini msikie Rostam kaenda njombe kuwatuliza wananchi na kutoa mchango wa kujenga shule na zahanati!
 
Tangu lini FISADI akaombwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa???????????? Tutamlaumu Prezidaa bure tunasahau prezidaa wetu ni FISADI mweupe. FISADI anaombwa pesa nyingi kama kufungulia mradi wa MGODI wa MADINI, Mradi wa kusambaza UMEME Tanzania nzima na nchi jirani, Mdadi wa kununua RADA au kutengeneza sare za vyombo vya dola. Since FISADI madau yake ni makubwa makubwa, hakuona umuhimu wa kuchangia ujenzi wa madarasa wanetu waweze kusoma. Anyway, aliona hapati gain yoyote hata kama angetoa mchango. Maake FISADI akitoa anategemea kupata money back.

Mtaamini kama ni FISADI wa madau makubwa asipo-APOLOGIZE kwa wananchi kutokana na kauli hiyo. Yangu masikio.
 
hamjiulizi kwanini mkuu alikuwa mkali katika sehemu zile imalinyi na ilembula..kumbuka imalinyi ni kijiji anachotokea adui wake wa kisiasa philip mangula na siku yenyewe ya tukio mangula alikuwa miongoni kwa viongozi waliokuwepo kumlaki.ndio maana akawa mkali pale muungwana pamoja na kuchangia milioni mbili alizosema hatembei nazo.

watu wa vijijini hawajaelemishwa hata hiyo siasa ya ujamaa na kujitegemea,kwasababu kila jamii miaka hii imejiingiza katika biashara zaidi ya kukuza maendelea ya vijiji ndio maana hawawezi kuipa kipaumbele hiyo siasa ya kusaidiana kujenga vijiji vya ujamaa kama enzi za mwalimu.vijiji hivi bila kuwezeshwa nyenzo mbalimbali,raslimali uchumi havitaendelea kamwe na zitabaki kuwa omba omba hata baada ya miaka 100
 
............MIMI NIJUAVYO RAIS YEYOTE ANATEMBEA NA FUKO LA PESA ...KAMA ANATAKA KUZIPIGA PANGA ASEME...KWENYE MSAFARA WA RAIS HAPAKOSEKANI PESA ....NA NDIO MAANA MARAIS WOTE WALIOTANGULIA ....AKIENDA MAHALI AKISHASOMEWA RISALA ...HUTOA PLEDGE YA CASH KUONGEZEA ANAPOTAKA...PESA IPO LIMITED NA MSHAURI WAKE WA PESA HUMSHAIRI KILA AENDAPO NI KIASI GANI ANAWEZA KUTOA MOJA KWA MOJA....HII NI KATIKA KUJENGA MAHUSIANO MEMA...INAPONEKANA PESA NYINGI ZA MFUKO WA RAIS..HUWA ANAZITUMIA ULAYA KUNUNUA MAWANI NA MAKOTI YA GUCCI.........WENZAKE KINA KIBAKI,MUSEVENI,KAGAME ets...wakienda vijijini huwa hawaoni hatari kuwa suprise wanakijiji kwa kumpatia mmoja wao kiasi cha pesa....kama ishara ya upendo!@!!...that is just a gesture ..but any empowerment programmes are meant to be sustainable...mabilioni ya kikwete is not one of the sustainable microeconomic programmes ..this was rather meant to reward presidents political suppporters ......and benefiting..remote bank managers and politician..while kikwete is just making hypocritical useless noises.........
 

..si rais aliyenunua waandishi..hata resource zetu na walinzi wakitumika kulinda nyumba za ndogo hawaoni....kweli ..miaka ya shetani...teh ndio walisemaga CHAGUO LA SHETA... oooh sorry LA MUNGU!!!!
 


Hii ni aibu.
 
Jk kwisha habari yake hata kuwajibu watu wa chini namna ile ameshindwa kabisa...sasa anategemea picha waliopata wale watu itawatoka karibuni mana wamemsikia wenyewe akiwajibu "kunya"....hata kujibu kisiasa wala kidiplomasia ameshindwa???
 
Kweli ashibaye kamwe hawezi kumkumbuka mwenye njaa. Huu ni msemo wa kawaida tu ila kwa alichokisema JK kwa wananchi hawa kinatakiwa kupewa tafakari ya kina. Amekuwa na hasira na wananchi wake waliomchagua kwanini???

Kwanza inawezekana kuna jambo liliomuudhi Mh. Rais, kiasi akashindwa kuhimili hasira zake. Lakini kama Rais hakutakiwa kung'aka namna ile. Kufanya vile kunapunguza imani ya wananchi wake kwa CCM na yeye mwenyewe binafsi. Ushauri wangu ni kwamba atumie njia ya kidemokrasia akanushe hilo kwamba hakumaanisha hivyo.
 
Huyu jamaa inabidi aingie studio tu atoke na album maanke mimi siungi mkono usanii wake uso na tija.

Mbona kipindi cha kampeni aliitwa mteule wa Mungu?

Mbona alikua anapita kwenye magari ya wazi na kusema sitawaangusha watanzania? Yaani leo hii imekua ni kejeli na hasira?

Mkuu,hapa katudharau sisi wananchi sasa sijui watu hao hao wataruhusiwa kuandamana kuilaani hiyo kauli yake? Si ni wanademokrasia sisi? au yeye na wafuasi wake hawaamini ktk demokrasia yaani kisiri siri wantumia udikteta
 
Pole sana mzee Mangula na wananchi wa Imalinyi lakini nina tatizo kidogo na huyu Yono Kevela, siasa si sehemu yake ila kaivamia tu kwa vile ana vijisenti lakini pia ninakiri kuwa mkoa wa Iringa kuna tatizo kwa sasa na wasipoangalia litaugawa ule mkoa vipande, uchaguzi wa 2005 na 2007 ccm umeendelea kuwagawa na 2010 tatizo litakuwa kubwa sana. Hawa jamaa CCM hawakuwa tayari kuwapoteza wale wazee NEC na Uenyekiti zaidi ya kuhujumiana ndani ya CCM wenyewe, sasa wameanza kujutia na kuwasaka wachawi hapo ndipo chokochoko inaporudi kisengerenyuma.

JK atakuwa alikuwa na sababu za msingi za kuwakaripia hawa ndg zetu, na ninathubutu kukiri kuwa mkoani Iringa na wilaya zake hakuna kuaminiana ndani ya CCM ukienda kwa wabunge huko ndio hatari. Kama wasaidizi wamemwambia akina Mangula wameandaa kumpiga maswali huko kijijini unategemea nini toka kwa muungwana? Ni lazima awe mkweli na lazima ukweli uume wakuu.

Poleni wana Njombe na pia Muungwana kwa shughuli pevu.
 
The sad thing is, even if there was a lesson to teach, and a discipline to instill the president bungled the occassion by his trademark colloquism and lack of communication skills.Reading him one would be excuse to think that this guy actually believes he is no mere politician and has attained the status of a demi god.
 
mbona huwa hawatoi maneno kama haya wakati wa kampeni?
 
hata kama nia ya rais ilikuwa ni kuwafunza wananchi kujaribu kutatua matatizo mengine wao wenyewe au kwa kutumia ngazi za wilaya, kuwakaripia hivyo kama watoto ni ukosefu wa heshima kwa raia wake.

inashangaza kuona aliyesema maneno ya aibu hivyo ni mwana diplomasia wa siku nyingi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…