Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,168
- 10,810
Ile siasa yetu ya kujitegemea tumeicha wapi? Au ilikuwa ni wimbo tu, rais anaenda nje kuomba na wananchi wanamuomba rais!
Kwa ambao hamjakaa vijijini mtalaumu, ila hizi shule kata zimefanywa mashamba ya watu, ukifika tu kijijini hata kama umeenda msibani utaambiwa uchangie ujenzi!
Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hutoa mabati nondo cement na mbao. wananchi hutakiwa kusomba mchanga na mawe tu, ambapo vijijini mawe yanapatikana bure, mchanga husombwa kwa kichwa na akinamama.
Sasa wanaposema nguvu zimaisha inamaana walikuwa wagonjwa au walikuwa na njaa!
Mkuu alitegemea aulizwe habari za epa, umeme na maji, sio kuambiwa hawana nguvu za kubeba mawe, sasa walitaka abebe yeye mabegani?
Mbona tarime hawachangishwi hela na shule zinajengwa kama kawaida, waende wakajifunze huko sio kumlalamikia mkuu wa kaya.
Inawezekana kabisa kuwa raia walifanya makosa kumuuliza mkuu aina hilo la swali.Lakini kuna namna ya kujibu kiasi cha kuwafurahisah watu, pia kuna namna ya kudela na viongozi wa chini.Kwani inaonyesha hawana vikao vya mara kwa mara.Maswali haya yanaonyesha pia kuwa wananchi pamoja na wabunge wao wamekata tamaa.
Shule au miradi mingi kweli inafanywa na wananchi wenyewe serikali ni kuongeza nguvu haijalishi miradi hiyo ni mikubwa au midogo kiasi gani.WATANZANIA WANAPASWA KUPEWA FARAJA HATA YA MANENO TU!