andrewk
JF-Expert Member
- Apr 13, 2010
- 3,102
- 489
waamndaaji watoto wao, badala ya kuwapa wazee wanaojua historia ya dunia.....AIBU SANA
Tukiwa tunaendelea kuangalia funeral rites za Nelson Mandela, mliosikiliza hotuba ya JK ni kwamba kaeleza umati kwamba Mandela alifika Tanganyika kwa mara ya kwanza January 1962. Kwamba safari hiyo alikuja kisiri akipitia Mbeya na kuingia Tanganyika. Kisha akapewa passport ya Tanzania kusafiria.
Hapa ndipo tunaposema viongoziwetu hawapekui vitabu au documents au hata kukumbuka tu. Ukweli ni kwamba histroia haisemi hivyo. Historia inasema kwamba January 1962 ulikuwa ni mweiz mmoja tu tangu Tangayika ijitawale ikiwa na Prime Minister Nyerere. Tukio kuu la kihistoria ni kwamba Huo mwezi karibi wiki mbili zilitawaliwa na NEC ya TANU ambayo ilipomalizika Nyerere akajiuzulu u-Prime Minister na akamuachia Rashid Kawawa.
Gavana-General Richard Turnbull asingeweza kutoa passport Nelson Mandela kirahisi.
Ukweli kuhusu ujio wa Mandela ni kwamba alikuja hapa December 1962, yaani mwaka huohuo, na akawepo kushuhudia Tanganyika ikipata status ya Republic. Hapo ndipo angeweza kupata passport ya Tanganyika na ndicho kilichotokea.
Sikuweza kuamini JK alipokuwa anasoma zile tarehe mbele ya dunia nzima, kwa sababu mtu aliyechimubka historia ya Mandela kokote ilikoandikwa anajua wazi kwamba Mandela alikuja hapa December 1962.
Na hata Mandela kwenye kitabu chake alichoandika kiitwacho A LONG WALK TO FREEDOM, ISBN: 9780349106533, pg. 345: {..we arrived in Dar Es Salaam the next day and I met Julius Nyerere, the newly independent country's firss President..}
Hivyo, wakati ule asingemkuta Nyerere akiwa President, na wakati pekee alipokuwa President ni kuanzia December 09, 1962.
Tuwe tunasoma kabla ya kwenda public.