Inachekesha sana, yaani mtu kama humjui JK atakuchezea sana, kila siku atakuwaacha mdomo wazi. Haya bwana endeleeni kutega mikono...mkisubiri matunda yadondoke! Kuna tofauti kubwa sana kati ya kutaka kufanya na kuwa na uwezo wa kufanya Vilevile kuna tofauti kubwa sana katika siasa kati ya kuwa ofisini na kuwa madarakani..akili ni nywele...
Kitila I am afraid i agree with you. Sasa hivi kama kuna kitu kinachoitwa miiko ya uongozi, basi hapa Tanzania hakipo, na anayosema JK ni kuwazuga watu, au naweza kusema anasema ili kutekeleza wajibu anaopaswa kuutekeleza yaani kuzungumza akiwa kama Kiongozi, lakini so far sioni utendaji na utekelezaji wa yale anayosema.
Siamini kama viongozi wetu huwa wanaingia madarakani kwa uchu wa kuiendeleza Tanzania, kwa nia ya kuifanya Tanzania iwe nchi ya watu wenye maisha bora, nchi yenye watu wasiodhalilika kwa kutoishi maisha ya kubabaisha. Ninachoona ni kuwa wengi (sio wote) wanaingia madarakani kwa lengo la kujitajirisha au kutumia nafasi za uongozi kufananikisha mambo yao ya kujitajirisha.
Ninaamini kuwa kama kweli serikali ingekuwa na nia ya kuendeleza nchi, tungeona mabadiliko mengi ambayo ni tangible. Kwenye nchi za wenzetu tukisikia GDP inaongezeka, au uchumi unaendelea vizuri ina maana umaskini unapungua, watu wanakuwa na hopes za kupata ajira na kuwa na maisha mazuri, lakini hapa kwetu ni vice versa.
For sure kutokana na Azimio la Zanzibar, naweza kusema sasa hivi ukiangalia uchumi binafsi wa mawaziri wetu unapaa, EL alivyosema uchumi unapaa, kwa maoni yangu alikuwa anazungumzia uchumi wake binafsi, which is very true, wake na wa mawaziri wengine unapaa haswa.
JKN alisema sasa hivi ukizungumzia Azimio la Arusha (miiko ya uongozi) utakuwa kama mwendawazimu. Mimi binafsi sikubaliani na vipengele vingi vya Azimio la Arusha, kwa sababu vingi ni very utopian, lakini nakubaliana sana na vya miiko ya uongozi. Lakini navyo leo hii havitekelezeki. CCM wamelease chama kwa wafanya biashara, sasa hivi wanataka returns na faida juu, kama ukileta miiko sasa hivi hakuna atakayerudisha investment yake na kupata returns. Ninachokiona sasa hivi ni kuwa tunazungwa tu, na tutaendelea kuzugwa hadi tutakapoamua na kuweza kuchukua hatua, lakini wakati huo watu watakuwa wameneemeka sana, in our expense.