JK tazama mwezio huyu

JK tazama mwezio huyu

Game Theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2006
Posts
8,546
Reaction score
855
Wakati JK anapigwa mawe na watu waliomchagua, Tazameni mwenzie Obama leo St Louis amabako umati wa watu LAKI MOJA walikuwa wanamsikiliza

2i0ejvb.jpg

obamastlouis_Q_20081018135311.jpg
 
Inabidi turudi kweye drawing board

Bahati mbaya JK hana drawing board , yeye alidhani kuwa kiongozi wa nchi ni lelemama, hivyo hakujali ni namna gani anaingia madarakani. Matokeo yake sasa hao waliombeba kumuingiza madarakani kumbe ni mafisadi na hana jinsi ya kuwashughulikia. Atatusaidia sana Watanzania akiamua kuachia ngazi sasa hivi na wala asisubiri 2010.
 
Lakini kumbukeni hata JK alianza hiv hiv. Tusubiri tuonae
 
Kama mliwaona wafadhili wa JK na still mkadhani ni kiongozi mzuri then huna haja ya kujilaumu.
Kwa hiyo kama mtandao mliwajuwa bado mkadhani wataipeleka nchi kwenye right direction.... Then bado huna haja ya kujilaumu provided sasa hautarudia makosa wakati wa kuangalia kuwa ni nani umpigie kura na kwanini....Ujumbe huu ni kwa watanzania..Hakuna haja ya kujilaumu...Tusirudie makosa.
Na ndio maana hata kuhusu Obama...Watu wake na washauri wake ni watu wazuri....Hata kama ni matajiri...Bado ni wale matajiri ambao wanaona sasa haina haja ya kuendeleza unyonyaji tena...Kwamba its time to look for the poor and less benefited.
Ni nia nzuri ambayo inamfanya Mc Cain anadai kuwa jamaa ni msoshalisti anayetaka kuleta usoshalisti marekani....Maneno ambayo ni mazito kiana due to the fact that socialism haingaliwi kwa jicho zuri na wamarekani.
 
Lakini kumbukeni hata JK alianza hiv hiv. Tusubiri tuonae
Hapana. Mwanzo wake JK haukuwa kama wa Obama. Obama unajua anasimama wapi. JK aliwalaghai Watanzania kwa lugha rahisi rahisi ya maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kasi mpya ari mpya etc.
 
Hapana. Mwanzo wake JK haukuwa kama wa Obama. Obama unajua anasimama wapi. JK aliwalaghai Watanzania kwa lugha rahisi rahisi ya maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kasi mpya ari mpya etc.

Correct, but do not copy and paste
 
Hapana. Mwanzo wake JK haukuwa kama wa Obama. Obama unajua anasimama wapi. JK aliwalaghai Watanzania kwa lugha rahisi rahisi ya maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kasi mpya ari mpya etc.

Ni kweli kabisa, halafu kinachoudhi zaidi ni kwamba jamaa hata hafanyi bidii yoyote ya japo kutimiza moja ya ahadi zake. Leo hii akitangaza watakaa na viongozi wa makampuni ya kuchimba madini ili kuhakikisha baada ya miezi mitatu wanakubaliana mikataba mipya ambayo itakuwa na maslahi kwa Watanzania, basi atajichukulia credits nyingi sana. Akitangaza Kiwira iliuzwa katika mazingira ya kutatanisha hivyo kuanzia leo inarudishwa rasmi katika umiliki wa Watanzania, wengi tutampongeza sana, lakini wapi!!!!! Ama kweli la kuvunda halina ubani!!
 
Mimi bado nawashangaa watu wenye matumaini kuwa JK anaweza kubadilika na kufanya kweli wakati yeye mwenyewe akihojiwa na Shaka sali alikiri kuwa hajui chanzo cha umasikini wa Tanzania. Sasa mnategema atajua solution kama chanzo hajui? Nashauri akasome kwanza angalau miezi 3 (Boot camp ya nguvu) ili akirudi aanze kufanya kazi.
 
Kama ni kukusanya watu tu, hiyo sio issue. Hata yeye aliwapagawisha watanzania zaidi ya hata Obama leo. Alikuwa akipita sehemu watu wanaacha kila kitu wanaenda kumsikiiza. Wakati huo ulikuwa ukimpinga JK unaonekana mchawi, kama ambavyo leo hii unahitaji ujasiri wa mwenda wazimu kumkosoa Obama!!
 
Kaka usemayo ni kweli. Hakuna kilicho maarufu kikadumu au kuisha kikiwa maarufu hivyo hivyo. Obama asome alama za nyakati kwa JK. Wa marekani wanategemea kuona Real Changes tena kwa kipindi kifupi sana ambacho siamini Obama anavyojiuza kwao kweli ataweza kutimiza. Hapo ndipo atakapokuja kugeukwa na hao hao wanamshabikia sasa na kumuona ni mzushi tu kama vile leo tunavyomuona JK mzushi kwa watanzania.

Tunamuomba Obama asidhani USA ni kama Kenya au Tanzania ambako unaeza ukaleta siasa za kihuni na watu wakakutizama tu.

Hakuna kitu kibaya kama watu kutarajia makubwa kuliko uwezo wako wa kuyatenda. Mkapa kamaliza fresh maana hakuna aliyetegemea anaweza kutimiza aliyokuwa ameahidi. kwanza kila mtu aliamini hata Urais hatouweza kwamba tungekuwa tunaongozwa na Nyerere kupitia Mkapa. hiyo imemuwezesha kutulia na kuweza kujipanga na kutimiza zaidi ya 80% ya alivyotaka kufanya.

Obama asidhani itaendelea kuwa shangwe ki hivyo kila siku. hizi shangwe zote zinaishia Nov 4 baada ya hapo ni kiwango cha kazi tu kitaangaliwa. John anaaminika maana uwezo wa kazi anaaminika anao na ndo maana hata kwenye chama chake hakupata upinzani mkubwa. Kazi kwako OBAMA na wanaokufagilia
 
Bahati mbaya JK hana drawing board , yeye alidhani kuwa kiongozi wa nchi ni lelemama, hivyo hakujali ni namna gani anaingia madarakani. Matokeo yake sasa hao waliombeba kumuingiza madarakani kumbe ni mafisadi na hana jinsi ya kuwashughulikia. Atatusaidia sana Watanzania akiamua kuachia ngazi sasa hivi na wala asisubiri 2010.

Ampe nani Nchi...?
 
"President Jakaya Mrisho Kikwete came to power on a populist vote. Wamachinga and the semi-employed and unemployed youth of Dar-es-Salaam symbolized his populist support. He promised them one million jobs. Kikwete's first task was to convert his populist support into a popular support. Populist is fragile; it is ambivalent and can go in either direction, progressive or reactionary. In a country like Tanzania with over 12,000 villages, in which live some 80 per cent of the population, mostly smallholders peasants, converting populism to popularity means establishing a close rapport with village communities...While the populist support was not converted into a popular support, worse, within one year the President even lost his popular support, thanks to his short-sighted liutenants who mercilessly chased away Wamachinga thus piling up numbers of unemployed. Now the President will have to create not one, but perhaps 1.4 million jobs to accomodate the former Wamachingas!" - Professor Issa Shivji on 'One Year On: A False Start' (The Citizen, 20 December 2006)

Senator Obama populism is indeed both fragile and ambivalent - just ask JK!
 
Bahati mbaya JK hana drawing board , yeye alidhani kuwa kiongozi wa nchi ni lelemama, hivyo hakujali ni namna gani anaingia madarakani. Matokeo yake sasa hao waliombeba kumuingiza madarakani kumbe ni mafisadi na hana jinsi ya kuwashughulikia. Atatusaidia sana Watanzania akiamua kuachia ngazi sasa hivi na wala asisubiri 2010.

Kweli,inaonekana alikuwa na strategy ya kuingia madarakanbi tu. Alitumia miaka kumi akijiandaa kuingia madarakani.Lakinim inavyoonekana, hakuwa na strategy ta jinsi ya kuongozi akishaingia madarakani
 
Kama ni kukusanya watu tu, hiyo sio issue. Hata yeye aliwapagawisha watanzania zaidi ya hata Obama leo. Alikuwa akipita sehemu watu wanaacha kila kitu wanaenda kumsikiiza. Wakati huo ulikuwa ukimpinga JK unaonekana mchawi, kama ambavyo leo hii unahitaji ujasiri wa mwenda wazimu kumkosoa Obama!!

Ni kipindi cha kina Obama, Zuma ... etc... upepo huo mkuu!!!
 
Ndugu zangu,

Katika hili suala naomba kuwaomba mkubali ukweli kwamba watanzania wote tunapaswa kubeba lawama na wala si Jakaya pekee yake.
Jakaya alipokuwa anaomba kura ama ridhaa ya watanzania kwenda Ikulu tuliona na kusikia wazi mapesa yakimwagwa kama njugu kila kona ya Tanzania.
Jakaya amekuwa mtumishi wa serikali kwa muda mrefu na wala hajawahi kuwa mfanyabiashara mashuhuri, sasa kwanini tusijiulize mapema wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba huyu Jakaya anapata wapi mapesa ya kumwaga kama njugu?. Jakaya alinunua kura zetu kwa maana kwamba tuliuza haki zetu kimsingi na kwa sasa hatuna haki tena ya kumuuliza anafanyia nini kura zetu alizonunua. Je na yeye akianza kuwauliza watanzania mlifanyia nini mapesa aliyowapa wakati wa kampeni mtamjibu nini?.

Hapa napenda kuwaeleza kwamba tuwe makini sana katika kuchambua, kupendekeza na kuchagua viongozi wa ngazi za juu. Tusibabaike na sauti nzuri, wala ahadi tamutamu, wala sura, wala pesa, wala kujuana.

Yanayotea katika uongozi wa Tanzania kwa sasa ni lawama zinatuhusu watanzania wote. Kama kweli tumechoka na kuelewa makosa yetu basi tuige mfano wa wana Tarime na Mbeya ili 2010 uwe ndiyo mwisho wa Chama Cha Mafisadi kutawala Tanzania.
 
Lakini kumbukeni hata JK alianza hiv hiv. Tusubiri tuonae

Obama hacheki cheki kama JK he is a real Man with Vision and Mission. Sio kweli kuwa JK alianza kama Obama, Obama amehudhuria midahalo mitatu na ameshinda yote na JK alikimbia mdahalo ulioandaliwa na UDSM 2005. Umeona ni jinsi gani inatofautisha jinsi watu hawa wawili walivyoanza!
 
Kweli,inaonekana alikuwa na strategy ya kuingia madarakanbi tu. Alitumia miaka kumi akijiandaa kuingia madarakani.Lakinim inavyoonekana, hakuwa na strategy ta jinsi ya kuongozi akishaingia madarakani

Aliuchukulia Ugombea Urais na Urais wenyewe simple kama beuty contest.
 
Wakati JK anapigwa mawe na watu waliomchagua, Tazameni mwenzie Obama leo St Louis amabako umati wa watu LAKI MOJA walikuwa wanamsikiliza

2i0ejvb.jpg

obamastlouis_Q_20081018135311.jpg

Ndugu usihadaliwe na huo umati wa watu na kumlinganisha Rais wetu hapa Tz na obama kwanza JK tayri yeye ni rais wa hii nchi na Obama ndio anahangaika kuomba hizo kura Kwatarifa yako mpaka kufikia jana usiku imesadikiwa kuwa watu weupe wengi na wakiwemo weusi hawatompigia kura Obama na ishara za kushindwa kwake zipo kubwa wengi walisema hawapo Tayari kuongozwa na mtu mweusi na wacha hilo kuna wale wastafu wa chama chake wametowa kauli ya kutompigia mtu mweusi kama yeye pia katika kampeni ya mlango kwa mlango kuna msichana mmoja mweupe ambae ni upande wa obama alishangazwa katika maeneo ambayo akiambiwa wakati alipokuwa anapita kuwashawishi watu kumpigia obama kuna kuna wale waliofika mpaka kusema kuwa hatuwezi kumchaguwa mtu kama yeye kutuongoza likatumiaka neno (N)kumbainisha Obama isitoshe kuna wale waliokuwa akisema bila kujificha imetambulika kuwa wengi wakiulizwa hujifanya wapo nae lakini ukweli hawatompigia kura na muombea mungu apate lakini akikosa hapo ndio wafrika tutazidi kuelewa tupo katika nafasi gani katika ulimwengu wa mtu mweupe na hasa kwa sisi wafrika halisi wachilia wale waliozaliwa huko
 
Back
Top Bottom