Elections 2010 JK ziarani Iringa watoto wa shule watolewa madarasani kumlaki

Elections 2010 JK ziarani Iringa watoto wa shule watolewa madarasani kumlaki

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,947
Reaction score
4,470
IMG_0952.JPG

Watoto wa shule wakiwa kando kando ya barabara kumsubiri mgombea urais kwa tiketi ya CCM JK kwa muda huu walitakiwa wawepo darasani kujisomea na kufuta adui namba moja Ujinga nchini.

IMG_0953.JPG

Hawa ndo wanamsubili JK kumlaki katika mji wa Ilula wilaya ya Kilolo jimbo la waziri wa Elimu ya juu Prof. Msola

IMG_0944.JPG

Huyu sijui ni Ticha wa hawa watoto au ndo kigogo wa CCM haijaweza kujulikana.

IMG_0930.JPG

Hata wa sekondari nao wapo wanamsubili JK

IMG_0934.JPG

Wanafunzi walio lazimishwa kutoka madarasani kuja kumlaki JK wakipiga soga

IMG_0929.JPG
 
Hii kali ya mwaka. JK kapumzike tu jamaa yetu.
 
Jamani hivi hii Nchi inaelekea wapi jamani!!! yaani watoto wetu badala ya kukaa darasani kusoma wanapangishwa foleni kumpokea JK kweli hii siyo haki :mad2::mad2:

Kwanza darasa la nne karibu wanafanya mtihani wao wa taifa halikadhalka form four nao wanakaribia kuanza mitihani ya kumaliza sasa huo muda wanaopoteza barabarani kumsubiri Jk aje kuwahaidi ahadi hewa siwangekuwa nanajisomea na kukumbushana maswali mawili matatu???

Naomba Jaji Makame utuafafanulie kuhusu hili jambo kwa kweli kama TUME YAKO IMERIDHISHWA NA WATOTO WETU KUTOLEWA DARASANI KUMPOKEA JK? na kama hili jambo linakubalika basi liwe kwa VIONGOZI WOTE WANAOGOMBEA URAIS SIO UPANDE MMOJA NDIO UFANYIWE HIVYO alafu tuone kama Elimu yetu itapanda ama kushuka
 
mhhhh wanafunzi hao wa shule za msingi ni kuwaghiribu maana hawana maamuzi
 
NEC, Msajili wa Vyama -- kwa nini mnakuwa mabubu kiasi cha kutisha katika mambo haya? Speak up -- you always claim to be independent, but we always say you are NOT!!!! You have failed to show your "independence!" And thism is not the first time. Huko Kirumba Mwanza hundreds of schoolgirls were herded into the stadium to beef up the crowd for JK -- and you were totally blind and deaf!
 
mhhhh wanafunzi hao wa shule za msingi ni kuwaghiribu maana hawana maamuzi

Wamejaza wanafunzi ili ionekane kuwa JK alijaza nyomi Iringa kumbe wengi ni wanafunzi.
Lakini hao wanafunzi walipaswa wawepo darasani sijui walimu nao vp? Au wameenda kiutashi?
 
Hawa jamaa (sisihemu - CCM) wanaanza kutapatapa. Sasa JK anataka kuwadanganya nini hawa watoto. Hebu angalia CCM ilichowafanyia - madogo wanaonekana wamechoka kabisa na serikali ya CCM haina mpango wa kuwapa elimu bora. Inatamani waendelee kuwa wajinga ili watawaliwe daima. Maana mjinga hata akiambiwa pumba za CCM ataziamini tu kiurahisi. CCM hawapendi wananchi wapate elimu bora ndo maana wamewajengea shule za kata ambazo hazina walimu.
 
Hawana mvuto,... hawana jpya.... wamekosa watu wa kuwasikiliza ndo maana wanawakusanya ma-dent!
 
Hii ni kashfa mbaya.
Inabidi mtu awekewe pingamizi tena kuhusu hili
 
Walikuwa wanajifunza somo la incapacitated at work. Wanashuhudia mahututi wao akiendelea kugombea. Bora hata Mugabe mara mia duh!!
 
huku tuankolea sasa, utafikiri enzi zile za chama kimoja?
 
huu si ukoloni. Nakumbuka hata mm nilitilewa kimkapa ati kilikuwa kinapita..du! Hivi bado wazee waliosoma kipondi cha ukoloni bado wapo tu madarakani? Wao ndio wanayo bado hii hulka ya kuwaabudu wakubwa wao. Oo GOD help this country.
 
huu si ukoloni?. Nakumbuka hata mm nilitolewa kimkapa ati kilikuwa kinapita..du! Hivi bado wazee waliosoma kipindi cha ukoloni bado wapo tu madarakani? Wao ndio wanayo bado hii hulka ya kuwaabudu wakubwa wao. Oo GOD help this country.
 
IMG_0952.JPG

Watoto wa shule wakiwa kando kando ya barabara kumsubiri mgombea urais kwa tiketi ya CCM JK kwa muda huu walitakiwa wawepo darasani kujisomea na kufuta adui namba moja Ujinga nchini.

IMG_0953.JPG

Hawa ndo wanamsubili JK kumlaki katika mji wa Ilula wilaya ya Kilolo jimbo la waziri wa Elimu ya juu Prof. Msola

IMG_0944.JPG

Huyu sijui ni Ticha wa hawa watoto au ndo kigogo wa CCM haijaweza kujulikana.

IMG_0930.JPG

Hata wa sekondari nao wapo wanamsubili JK

IMG_0934.JPG

Wanafunzi walio lazimishwa kutoka madarasani kuja kumlaki JK wakipiga soga

IMG_0929.JPG

Kaka hizi picha ni za enzi zile za mwalimu Kambarage ,kwani mimi najiona pale nimesimama chini ya ukuta tukimsubiri Nyerere apite na kweli alipita hata bila ya kutusalimia wakati tulikuwa tunamsubiri toka asubuhi.
 
Unapokuwa mjinga basi ukiwa kwa werevu ufiche kwa kukaa kimya!
 
Kaka hizi picha ni za enzi zile za mwalimu Kambarage ,kwani mimi najiona pale nimesimama chini ya ukuta tukimsubiri Nyerere apite na kweli alipita hata bila ya kutusalimia wakati tulikuwa tunamsubiri toka asubuhi.

Mzee umeona pumba hizi ndo maana nikakwambia wewe lazima ni Yanga kandambili....unatakaa hata ukweli
 
Kaka hizi picha ni za enzi zile za mwalimu Kambarage ,kwani mimi najiona pale nimesimama chini ya ukuta tukimsubiri Nyerere apite na kweli alipita hata bila ya kutusalimia wakati tulikuwa tunamsubiri toka asubuhi.

Pole nahisi bado unaota amka kumekucha
 
Back
Top Bottom