Elections 2010 JK ziarani Iringa watoto wa shule watolewa madarasani kumlaki

Elections 2010 JK ziarani Iringa watoto wa shule watolewa madarasani kumlaki

Jamani hivi hii Nchi inaelekea wapi jamani!!! yaani watoto wetu badala ya kukaa darasani kusoma wanapangishwa foleni kumpokea JK kweli hii siyo haki :mad2::mad2:

Kwanza darasa la nne karibu wanafanya mtihani wao wa taifa halikadhalka form four nao wanakaribia kuanza mitihani ya kumaliza sasa huo muda wanaopoteza barabarani kumsubiri Jk aje kuwahaidi ahadi hewa siwangekuwa nanajisomea na kukumbushana maswali mawili matatu???

Naomba Jaji Makame utuafafanulie kuhusu hili jambo kwa kweli kama TUME YAKO IMERIDHISHWA NA WATOTO WETU KUTOLEWA DARASANI KUMPOKEA JK? na kama hili jambo linakubalika basi liwe kwa VIONGOZI WOTE WANAOGOMBEA URAIS SIO UPANDE MMOJA NDIO UFANYIWE HIVYO alafu tuone kama Elimu yetu itapanda ama kushuka

mkuu, haya ya kupanga watoto barabarani hayajaanza leo na yamekuwepo tokea nyerere akiwa kijana, kwahiyo naona kama kumlaumu tunaelekea wapi ni kama sielewi kidogo

Nakuuunga mkono kwamba this has to be stopped and tume ya uchaguzi needs to make a statement... lakini je, hata wasipoitwa, inawezekana kweli kwa mtoto mdogo kubaki darasani wakati anasikia rais wake tena anayemuona kwenye tv na picha nyingi kila mtaa hadi makaburini anapita just a few steps away??

waalimu wenyewe wanaweza kuwa kwa kwanza kujipanga barabarani
 
Kaka hizi picha ni za enzi zile za mwalimu Kambarage ,kwani mimi najiona pale nimesimama chini ya ukuta tukimsubiri Nyerere apite na kweli alipita hata bila ya kutusalimia wakati tulikuwa tunamsubiri toka asubuhi.
Eee, kweli mmechoka ka jk wenu, enzi za Mwalimu kulikuwa na sanlug ya mchina? Kulikuwa na yeboyebo? Kulikuwa na sura za kupoteza matumaini kama tunazoziona hapo? Hao green guard wamebeba sura ya nani hapo kwenye vifua vyao? Mjukuu wangu namuona hapo kaenda kwa kulazimishwa tu na alizaliwa miaka 5 baada ya Nyerere kututoka. Polee!!!
 
Kama huoni Ubaya wa Watoto kukatishwa vipindi vyao ili wakampokee Mgombea Urais, nadhani wewe ndiwe Lofa
Hao ndo ccm bwana,wanashindwa hata kujua kwa nini elimu inashuka kiwango,wamezifanya shule za kata kama nyenzo za kutimiza utashi wao kisiasa na ndo maana hao madenti wa sekondary hapo ni kutoka kwenye kata,mbona hatuwaoni wale wa st.nanihii? Huo ni utumwa waari,kasi na guvu zaidi.
 
Kaka hizi picha ni za enzi zile za mwalimu Kambarage ,kwani mimi najiona pale nimesimama chini ya ukuta tukimsubiri Nyerere apite na kweli alipita hata bila ya kutusalimia wakati tulikuwa tunamsubiri toka asubuhi.

Enzi za Nyerere Kulikuwa na pikipiki za toyo na viatu vya yeboyebo????????
Wewe ni boya kiduanzi!
 
maskini kikwete. umeishiwa wasikilizaji wa mikutano yako kiasi hiki?
 
Hao ndo ccm bwana,wanashindwa hata kujua kwa nini elimu inashuka kiwango,wamezifanya shule za kata kama nyenzo za kutimiza utashi wao kisiasa na ndo maana hao madenti wa sekondary hapo ni kutoka kwenye kata,mbona hatuwaoni wale wa st.nanihii? Huo ni utumwa waari,kasi na guvu zaidi.

na bado RizWan hajaenda huko na FesTi Lady naye bado...watapanga sana misitari na vumbi watakula.......
dis iS unfair indeed....
 
Back
Top Bottom