Elections 2010 JK ziarani Iringa watoto wa shule watolewa madarasani kumlaki

Bora maisha kwa mtanzania, huyu mwalimu kapewa maagizo na DEO na asifanye hivyo aone kama hajapelekwa swekeni, mi nafikiri huu ni unyanyasaji namba 1 na JK anatakiwa kushtakiwa kwa hili, haki za watoto ziko wapi hapa?
 
Mgonjwa wa kifafa kachanganyikiwa jamani! asije akaanguka tena jukwaani
 

kwenye hizo kuta za madarasa ni vumbi, hakuna walimu, vitabu ,sasa si bora waende kumshuhudia anaewapa mateso ili wamjue. CCM ikifa kama kipo cha kumiss itakuwa pumba za makamba, uongo wa Mbayuwayu,mipasho ya mama "WAMA" na mashauzi ya "Ridh". One day Yes CCM itakuwa kama KANU
 
Kuna tatizo gani kwa watoto hao kumpokea prez wao? Haya mawazo ya kilofa yataisha lini?
 
CCM imekwisha.Kwa kuwa shauri tu wanzishe bendi na sio chama cha siasa bendi yao hiitwe CCM Orchestra chini ya uongozi wa Jakaya ukisaidiwa na Makamba kutoka Tanga Tanzania.
 
Jamani huu upuuzi umerudi tena!!! Nakumbuka yupo kiongozi wakati wa Mkapa alipiga marufuku wanafunzi kutolewa madarasani kwa ajili ya kuwapokea viongozi, kweli CCM imekwisha!!!
 
Mkuu Fidel asante sana kwa Picha, leo nilipita maeneo ya Ilula nikaona Wanafunzi wengi wanaelekea alikokuwa anahutubia JK, sasa najiuliza JK amepokelewa kama Mgombea Urais au Rais? Naona CCM wanafanya mambo ya aibu kabisa, badala ya Watoto kukaa darasani na kufuta Ujinga wanawashindisha juwani

Shame on you CCM kwa hili
 
Kuna tatizo gani kwa watoto hao kumpokea prez wao? Haya mawazo ya kilofa yataisha lini?

Kama huoni Ubaya wa Watoto kukatishwa vipindi vyao ili wakampokee Mgombea Urais, nadhani wewe ndiwe Lofa
 
Huku ni kukiuka HAKI ZA WATOTO. Its a humamn rights issue. Naomba NGO zinazojihusisha na haki za watoto zijitokeze kuonya CCM iache hii tabia chafu.

Mtu unakwenda kumlaki mtu unayempenda. Sasa hawa watoto wanalazimishwa wampende mgombea urais wa CCM? Do they have to sacrifice their classes for him?

CCM acheni kunyanyasa watoto wetu!
 
Nahisi hao wa primary kwenye madarasa yao hakuna hata madawati ya kutosha, vitabu vya kutosha, vyo ni adimu, ratio ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi themanini, paa la shule limekwisha oza, wengi wao wazazi ni maskini wa kutupa, mwalimu wao ni 'voda fasta', hakuna maabara, sijui kama by 2013 watakuwa na uwezo wa kutumia computer, wengine kwa umri wao walitakiwa kuwa sekondari, wala si wapiga kura wanasikiliza ili iweje, mwalimu huyo 'voda fasta' anataka ukuu wa wilaya. Kwa kifupi mwalimu huyo, voda fasta, anatakiwa kukalipiwa na wazazi!
 
Kuna tatizo gani kwa watoto hao kumpokea prez wao? Haya mawazo ya kilofa yataisha lini?

....du kibunango kwa kuita wenzio malofa.....yes ni malofa kwa kuwa hawaishi kwa mapesa ya mafisadi...

hivi mwanafunzi kumlazimisha kumpokea mgombea na wakati kura hapigi inasaidia nini....si muache waende kwa mapenzi yao............

mwaka huu ugali moto ...mboga moto...zanzibar ...inaenda CUF na huku moto ndio huoooo!!
 
Hii ni kashfa mbaya.
Inabidi mtu awekewe pingamizi tena kuhusu hili

Ni kweli ni makosa. Hilo pingamizi nani atalikubali? Mteule wa Kikwete ama mwingine?
 
Halafu jana kuna tafiti imeonyesha kuwa wanafunzi wa darasa la saba wanamaliza shule hata kusoma jina lake hajui hivi kwa mtindo huu tutainua elimu?
 
Jana kwenye vyombo vya habari kuna asasi iliofanya utafiti na kugundua kuwa kuna wanafunzi wanamaliza darasa hata jina lake hajui kuliandika hivi kwa mtindo huu tunainua elimu kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…