GE2025 JKT kuja na mafunzo mapya kukuza uzalendo wa vijana mitandaoni

GE2025 JKT kuja na mafunzo mapya kukuza uzalendo wa vijana mitandaoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema jeshi hilo litaanzisha masomo ya uzalendo wa kidigitali kutokana na ukweli kwamba vijana wengi hupatikana kwenye mitandao ili kuwajengea na kukuza uzalendo katika mambo wanayofanya wakiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Meja Jenerali Mabele alitoa kauli hiyo katika kikosi cha 822KJ Rwamkoma, wilayani Butiama, mkoani Mara, mara baada ya vijana kuhitimu mafunzo yaliyodumu kwa miezi mitatu.

Pia Soma:Vijana wa JKT Waonywa Kuhusu Mitandao, Waandaliwa kwa Mapambano ya Taifa
​
 
Amekoswa kazi za kufanya kabisa kabisa?

Yaani uzarendo upi Ili Hali wakubwa huko juu hawana hata chembe kidogo ya uzarendo yaani Hadi watu wa usalama jeshi nk halafu sisi ndo atuone hatuna uzarendo Hadi aanzishe program ya kidijital?
 
Mnataka kufundisha vijana namna ya ku comment mtandaoni???!! mmechelewa sana. Sijui ni kwa nini Hawa wazee wetu bado wana mindset/sotware ya 1990's huko, hawataki kuendana na uhalisia
 
FB_IMG_1758877681974.jpg

Leo nimemsikia Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Mabele akiongelea kuhusu kuanzisha somo la Uzalendo wa Kimtandao kwenye mafunzo ya Vijana.

Napenda kuwaambia JWTZ hasa JKT, wajitathmini sana kwa hili wanalofanya kulingana na nyakati zilizopo.

Kibaya zaidi wanachotangaza kuanza kukifanya kinawafanya Wananchi wawe na hasira zaidi dhidi yao kwa sababu kwa sasa karibu kila Mwananchi anafahamu kuwa Nchi inaangamizwa na kansa ya Ufisadi wa kutisha wa Viongozi wa kisiasa na familia zao huku Serikali wakizuiq vyombo vya habari kutoa taarifa za Ufisadi huo hali iliyopelekea Wazalendo wa kweli wa Taifa hili kutumia Mitandao ya Kijamii kuwatasrifu Wananchi.

Napenda kuwaambia JWTZ hasa JKT tu, hali zetu wananchi wa kawaida ni mbaya sana. Huduma za kijamii ni mbaya sana , si maji si madawa hospitalini vyote kupatikana ni kwa majaliwa kwa sababu ya rushwa na dili za Viongozi na Wanasiasa. Miundombinu inajengwa kwa kiwango kibaya kwa sababu ya rushwa huku watoto wetu wakisoma kwenye shule zisizo la vifaa bora vya kufundishia na mazingira mazuri

Usalama wa Wananchi wa Tanzania ni mdogo sana. Watu wanaotekeleA haki zao z kikatiba kutoa maoni na kupinga mabaya ikiwemo rushwa na matumizi mabaya ya madaraka wanatekwa, kupotezwa, kuuwawa na kufunguliwa kesi za uongo ili wakae magerezani.

Kibaya zaidi haya yote yanafanyika huku wao waliokula kiapo kuilinda Katiba wakiwa kimya hawafanyi chochote.

Ni heri wajirudishe darasani wenyewe Wanajeshi na kuanza kufundishana namna ya kuishi kiapo chao cha kuilinda Katiba inayokataa maovu ya rushwa, ubadhilifu na kunyanyasa Wananchi kuliko kuwa machawa wa Wanasiasa eti kuwafundisha vijana kuhusu Uzalendo wa Mitandaoni wakati Taifa linaangamia.
 
Mheshimiwa Meja Jenerali, Uzalendo hauletwi kwa mafunzo tu ya mitandaoni, maneno matamu ya wanasiasa, propaganda zao! Uzalendo unaletwa matendo mema, na yasiyo na chembe ya shaka!

Tena hayo matendo mema yanatakiwa kuanzia kwa viongozi wenye dhamana ya kuwaongoza wengine! Mwalimu Nyerere ni mfano mzuri wa viongozi walio uishi uzalendo.

Mwalimu hakuwa mbinafsi! Mwalimu hakuwa mwizi! Mwalimu hakuwa mla rushwa! Mwalimu hakuwa mpiga dili! Mwalimu hakuwa fisadi, na wala hakuwakumbatia mafisadi! Mwalimu aliifanya Ikulu kama mahali patakatifu, badala ya eneo la kupangia mikakati ya kuihujumu nchi! Mwalimu hakuwa na upendeleo wa Kikanda, Kabila, ndugu, marafiki, mwalimu alizilinda raslimali za nchi kwa manufaa ya wananchi wote, nk.

Mjeshimiwa Meja Jenerali, Viongozi wenye dhamana ya kuongoza wengine ndiyo wanatakiwa kuwa wa kwanza kufundishwa nini maana ya uzalendo! Maana wengi wao hata hawaelewi.
 
Hawa viongozi wa usalama wenye umri kuanzia 45+ kwanza wao wanaona kila kitu wanakijua na pia mawazo yao wanaona bora mda wote wakati ukwel Dunia sasa haipo hivyo swala la uzalendo linaanzia elimu yachini kabisa sema uvumi umevumishwa kwamba ukienda kwenye majeshi ndiyo unajifunza uzalendo hapo kuongeza vitengo kupatiana nafasi wakat hilo swala lianzie elimu ya msing
 
Mabele Yuko hapo kulinda ugali Wake TU,
Ivi wewe mabele unaelewa maana ya uzalendo?

Uzalendo sio nidhamu ya uoga Bali, Kila citizens kuwajibika kwenye kujenga na kumiliki uchumi wa Tanzania.

Nimekasirika sana kwa kauli ya mabele anaonekana ni MTU selfishness alafu Malaya mkubwa wewe
 
Tumekuwa na Jeshi la kipuuzi sana hivi sasa. Kama hii ndo thinking ya Majenerali wetu basi tumekwisha kama Taifa.
 
Yaani eti wao ndo wanafundishe uzalendo? Tena ni bora kama shida ni maadili na uzalendo ukampeleka mwanao seminari pure utakuwa umemsaidia na si huko jeshini.

Wao wenyewe wanatuhumiwa kuhongwa, kuruhusu viongozi wetu wazalendo kuuwawa. Wanaruhusu nchi kufilisiwa na wenye roho mbaya vyote vikiwa mbele ya macho yao alafu eti leo ndo wanafundishe uzalendo, labda wawafundishe chipukizi wa chama chao.

Jeshi limeshindwa kulinda mipaka, kuilinda katiba ya nchi na mali za nchi. Jeshi kama genge la maskani za vijana wahuni wahuni
 
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema jeshi hilo litaanzisha masomo ya uzalendo wa kidigitali kutokana na ukweli kwamba vijana wengi hupatikana kwenye mitandao ili kuwajengea na kukuza uzalendo katika mambo wanayofanya wakiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Meja Jenerali Mabele alitoa kauli hiyo katika kikosi cha 822KJ Rwamkoma, wilayani Butiama, mkoani Mara, mara baada ya vijana kuhitimu mafunzo yaliyodumu kwa miezi mitatu.

Pia Soma:Vijana wa JKT Waonywa Kuhusu Mitandao, Waandaliwa kwa Mapambano ya Taifa
​
huo ni utapeli
 
Mitandao gani wakati serikali ina ban mitandao pendwa watu hawaipati mpaka kwa VPN?
 
Back
Top Bottom