Leo nimemsikia Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Mabele akiongelea kuhusu kuanzisha somo la Uzalendo wa Kimtandao kwenye mafunzo ya Vijana.
Napenda kuwaambia JWTZ hasa JKT, wajitathmini sana kwa hili wanalofanya kulingana na nyakati zilizopo.
Kibaya zaidi wanachotangaza kuanza kukifanya kinawafanya Wananchi wawe na hasira zaidi dhidi yao kwa sababu kwa sasa karibu kila Mwananchi anafahamu kuwa Nchi inaangamizwa na kansa ya Ufisadi wa kutisha wa Viongozi wa kisiasa na familia zao huku Serikali wakizuiq vyombo vya habari kutoa taarifa za Ufisadi huo hali iliyopelekea Wazalendo wa kweli wa Taifa hili kutumia Mitandao ya Kijamii kuwatasrifu Wananchi.
Napenda kuwaambia JWTZ hasa JKT tu, hali zetu wananchi wa kawaida ni mbaya sana. Huduma za kijamii ni mbaya sana , si maji si madawa hospitalini vyote kupatikana ni kwa majaliwa kwa sababu ya rushwa na dili za Viongozi na Wanasiasa. Miundombinu inajengwa kwa kiwango kibaya kwa sababu ya rushwa huku watoto wetu wakisoma kwenye shule zisizo la vifaa bora vya kufundishia na mazingira mazuri
Usalama wa Wananchi wa Tanzania ni mdogo sana. Watu wanaotekeleA haki zao z kikatiba kutoa maoni na kupinga mabaya ikiwemo rushwa na matumizi mabaya ya madaraka wanatekwa, kupotezwa, kuuwawa na kufunguliwa kesi za uongo ili wakae magerezani.
Kibaya zaidi haya yote yanafanyika huku wao waliokula kiapo kuilinda Katiba wakiwa kimya hawafanyi chochote.
Ni heri wajirudishe darasani wenyewe Wanajeshi na kuanza kufundishana namna ya kuishi kiapo chao cha kuilinda Katiba inayokataa maovu ya rushwa, ubadhilifu na kunyanyasa Wananchi kuliko kuwa machawa wa Wanasiasa eti kuwafundisha vijana kuhusu Uzalendo wa Mitandaoni wakati Taifa linaangamia.