Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
mhhhhh ha ahaha haha haha...hapa najua tutasikia mengi na kudanganywa tutadanganywa najua...haya ongezeni chumvi mtutie wivu!
Kwa mtazamo wangu JKT kweli ni kupoteza muda na wakati kama si kujifunza wizi, uongo, umalaya na kugombana na maafande.
Umoja na mshikamano katika Tanzania tumefundishwa toka tukiwa mashuleni kwa kupitia somo la siasa kwa wale wazee wenzangu na kwa sasa wanaita jina lingine.
Tanzania ilikuwa inahimiza sana umoja na mshikamano (Pitia katiba ya TANU) na kidogo pia katika katiba ya CCM.
Nyimbo nyingi tulizoimbishwa JKT pia tulikuwa tunaimba mashuleni katika Mchakamchaka nk. Pia katika baadhi ya mikoa tulikuwa na chipukizi, game scouts, Tanu youth league nk.
JKT ni kupoteza muda na wala si lolote zaidi.
Lakini Mwanakijiji kauliza swali kama JKT lilikuwa ufisadi? Mpaka sasa hamna mtu aliyejibu zaidi ya kutoa stori....
JKT ilinipotezea muda wa mwaka mzima kabisa. Vile vile ilinifanya nikosane na kimwana wangu tuliyekuwa tumekutana high School na kuahidiana kuoana (kama kweli ahadi hiyo ilikuwa serious). Jambo nililochukia JKT zaidi ilkikuwa ni ile discipline ya woga na unafiki ambao ulikuwa unatokana na yale mafunoz ya msuli yaliyokuwa yakitolewa.
Hata hivyo JKT ilinikutanisha na watu wengi sana na kunifanya nijifunze mengi sana kuhusu jamii yetu. Ingawa sasa hivi sikumbuki hata mtu mmja kati ya marafiki hao niliokutana nao JKT, kwa miaka mitano ya kwanza tangu kumaliza JKT nilikuwa nakutana nao na walinisaidia sana kujenga network yangu hapo Dar.
Jambo ninalokumbuka sana ni pale nilipomaliza mafunzo ya ukamnada pale Ruvu na kupewa tepe moja ya kijani na kupandishwa cheo kutoka Serviceman na kuwa "Volunteer Lance Corpolar" au "Green Kwanja." Kwa miezi sita niliyotumia cheo hicho cha V-L/Cl niliwafanya kuruta walioningia Januari waione JKT kama sehemu ya mafunzo zaidi ya mateso; sikuhimiza discipline ya woga na nilikuwa mkali sana ninapopewa nidhamu ya ya kinafiki. Kwa bahati mbaya juhudi zangu zilikuwa ni kama punje ya mchele kwenye gunia zima; laiti wale makamanda wengine nao wangejifunza kwangu namna ya kuwatraini kuruta wale kiakili na kijamii.
Lakini Mwanakijiji kauliza swali kama JKT lilikuwa ufisadi? Mpaka sasa hamna mtu aliyejibu zaidi ya kutoa stori....
mwanakijiji you are not serious today. Kama kuna kitu kinachonipa raha ninapokumbuka historia ya maisha yangu basi si kingine ila ni JKT. Nani anawakumbuka kina Afande Mtono wa Mlale na Mlay wa Mafinga? Sikumbuki kama niliwahi kuwa na uvumilivu katika maisha kama wakati ule. Halafu ilikuwa ni burudani ya pekee kwa makoplo kuongea kiingereza cha kuvunja ili waonekane na wao ni wasomi.
Nakumbuka koplo mmoja alinotolea mpya aliponiamrisha kuchanganya chakula changu na cha kuruta mwingine kwenye mustini (sic) moja ile nimpatie mustini yangu: Akaja na hii kali: "wewe rikututa, confuse chakura chako na cha mwenzio kwenye mustini moja nataka hiyo mustini yako niitumie. Umesiki?"
Lakini Mwanakijiji kauliza swali kama JKT lilikuwa ufisadi? Mpaka sasa hamna mtu aliyejibu zaidi ya kutoa stori....
Kenya hawakuwa na JKT na wamekuwa nchi nzuri tu, tena iliyoendelea kiuchumi. Muda mrefu ambao wengi wetu tungekuwa tumeshamaliza elimu ya juu tulitakiwa kwenda kuchimba mitaro, mahandaki, kujenga nyumba, kuchoma matofali na wale waliokuwa ruvu watakumbuka mpunga!
Kama ningetaka kujenga nyumba au kulima mashamba ningefanya ya kwangu mwenyewe. Mbona sasa hivi watu hawalazimishwi kwenda JKT lakini bado wana uzalendo? Nadhani ile ilikuwa ni hofu ya vita baridi zaidi kuliko kitu kingine chochote.
I agree maana context ya mada jinsi alivyoleta Mwanakijiji haviendani na kichwa cha habari!Mimi nadhani sasa tunali-abuse hili neno Ufisadi....
JKT tulikuwa tunafundishwa uwongo, umalaya, wizi, nidhamu ya woga na unafiki na wala si kingine.
Matokeo ya mafunzo hayo ya JKT leo hii tunayaona dhahiri kwamba Taifa limejaa viumbe waoga ambao wanashindwa ama wanaogopa kudai haki zao kisheria.
Tazama nchi inavyoendeshwa leo hii, wananchi ile kuandamana tu kuonesha kwamba hawafurahishwi na hali iliyopo inakuwa ngumu. Huo ni woga na wala si uzalendo kama mnavyodai hapa.
JKT ilikuwa ni nyimbo za kumsifu Nyerere, Chama na viongozi wa chama tawala na kukutisha wewe kijana kwamba bila Nyerere, Chama tawala na viongozi wa chama hicho basi hakuna la maana litakalotokea Tanzania.
Pia JKT ilitumika sana katika kutunywesha maji ya bendera ya CCM kinguvu, kutuvunja matumaini ya kuweza kujitawala, kutunyima uhuru wetu kifkra (kimawazo).
JKT serikali ilikuwa inatumia pesa nyingi kuliko mapato yaliyokuwa yanapatikana kutokana na shughuli za uzalishaji makambini humo.
tulichotakiwa kukifanya katika kipindi kile cha mwaka mzima ni kuwatuma vijana wetu waende kufanya kazi kwa kujitolea tokana na fani zao walizosomea. Kama umesomea ubwana mifugo basi ukafanye kazi ya ubwana mifugo chini ya mtaalam wa mifugo bila mshahara, ila upatiwe maradhi, chakula nk. Lakini JKT ilivyokuwa ni kwamba unapelekwa kambini ambako unakutana na afande (standard seven), kwanza anawivu na wewe umesoma, maelewano madogo zaidi ya kuongopeana na kuogopana, kupeana mateso yasiyo kichwa wala miguu wakidai huo ndiyo ukakamavu.
Kama lengo la JKT (Jeshi La Kujenga Taifa) ni kujenga taifa, sasa kwanini kuna kupigana mikwara na maafande?. Kwa nini makambi yalishindwa kujiendesha yenyewe ama kujitegemea?.
Kwa upande wangu there is no way I will send my kids to JKT kama itarudishwa leo hii hata kwa mtutu wa bunduki.
Kuna vitu ambavyo namuunga mkono Nyerere lakini hili lilitupotezea muda wa mwaka mzima kusota kwenye mitaro na yare "maafande".
JKT tulikuwa tunafundishwa uwongo, umalaya, wizi, nidhamu ya woga na unafiki na wala si kingine.
Matokeo ya mafunzo hayo ya JKT leo hii tunayaona dhahiri kwamba Taifa limejaa viumbe waoga ambao wanashindwa ama wanaogopa kudai haki zao kisheria.
Kama lengo la JKT (Jeshi La Kujenga Taifa) ni kujenga taifa, sasa kwanini kuna kupigana mikwara na maafande?. Kwa nini makambi yalishindwa kujiendesha yenyewe ama kujitegemea?.
Kwa upande wangu there is no way I will send my kids to JKT kama itarudishwa leo hii hata kwa mtutu wa bunduki.