JKT kurejeshwa, wazo zuri au limepitwa na wakati?

JKT kurejeshwa, wazo zuri au limepitwa na wakati?

Weweeee NImekutana na wenzangu sasa

Nilikuwa K833 JKT Oljoro a.k.a kambi ya mawe.
nakumbuka sana rollcall moja ya siku za kwanza kwanza ambako afande mmoja kwa jina aliitwa Kichele akiita majina alifikia jina la mmoja wetu aliyeitwa Maiko. Yeye afande akaita Michaeli, Akarudia mara tatu Michaeli hakuna liyeitika. Mwishoni kabisa akabaki mmoja ambaye hajaitwa jina. Akaambiwa aangalie jina lake kwenye orodha ya makuruta akaonyesha lile Michael. Afande akamuuliza wewe unaitwa nani. Akamwambia mimi ndiye huyu Maiko. Akamng'akia UNA AKILI KWELI WEWE. MIMI NI WAPI NIMETAJA MAIKO? NINAMTAKA MICHAELI. Ahaaa nyiye ndiyo mliokuja kutumikia majina ya watoto wa matajiri eeeh. Basi umeshindwa. Nitakumaliza mimi!!!!!!!!

Kama si Sir Major kuja eneo la hangani ghafla: dogo angeipata fresh siku ile.

Moja mbili tatu moja
 
JKT ni nzuri sana katika kujenga umoja miongoni mwa Watanzania, lakini watoto wa 'Baba zao' walikuwa hawafanyi lolote zaidi ya kupatiwa vyeti vya magonjwa mbali mbali wasiyokuwa nayo ili wasihenyeke kama watoto wa wakulima na wafanyakazi. Na sasa hivi wengi wao wanaosoma nje ya nchi ndiyo hawatatia mguu kabisa huko JKT. Pia kuna baadhi ya "Watanzania" tulikuwa hatuwaoni kabisa JKT walikuwa wanatumia fedha zao kuhakikisha wanaikwepa JKT kwa kila hali.
 
Samahani wakuu nimekuja late ktk mada moja muhimu sana.
Mkuu Mwanakijiji ndugu yangu kama wewe hukupenda JKT basi sii wote, na nadhani sababu zako ziko nje ya malengo ya awali ya hizi kambi. Usichukulie sana uendeshaji mbovu wa baadhi ya watu kutoa hukumu ya malengo ya JKT.
Watu wengi sana wamezungumza mengi kuhusiana na JKT na hasa kuihusisha na Ukomunist lakini ukweli hasa wa JKT ni muundo wa Kibbutz zile za Israel.
Mwalimu Nyerere aliiga Kibbutz za Israel kwa malengo ya sawa isipokuwa sisi Tanzania tulishindwa kwenda na wakati pia tulishuhudia Abuse ya madaraka. Ndio maana ktk baadhi ya mada za miaka miwili iliyopita nilisisitiza sana kuangalia upya malengo na umuhimu wa kuwepo kambi hizi..Na tuchukulie kambi za Kibbutz kuwa mfano bora kwetu ktk uendeshaji wa kambi.

Nchi za kiafrika tunapokwama ni kutokuwa na nidhamu ya kazi yoyote ile siku zote sisi hu abuse madaraka ama huingiza vitu ambavyo ni nje ya malengo ya kile kilichokusudiwa.
Tazama Israel leo hii ktk Kibbutz zao ndipo utaalam mkubwa wa uvumbuzi wa mbegu za mimea mbali mbali inayoweza kustawi huzalishwa huku. kuna Lab za kila aina toka Uvuvi, Mifugo na kadhalika mbali na zile shughuli za kijeshi..Watu toka sehemu mbali mbali duniani huenda ku volunteer na michango kibao ya fedha na mawazo huwekwa ktk majaribio. Kibbutz zimekuwa sehemu za majaribio ya kisayansi kabla kitu hicho hakija hit market ama kupelekwa kwa wananchi. Kibbutz ni sehemu ya uchumi wa Israel mbali ya Ulinzi sio kwetu TZ..
Tanzania JKT imekuwa kama adhabu, sehemu ya Ufuska, Ukubwa na ubwana basi ili mradi tumekosa dira. Kwa mtaji huu hata mimi sikubaliani kabisa kurudishwa kwa JKT ikiwa hakuna malengo mapya na mfumo tofauti wa kuendesha kambi hizo..JKT ni chimbuko la MAARIFA kwa vijana wetu ktk Ulinzi bila kusahau uti wa mgongo wa uchumi wetu KILIMO (ukulima, Uvuvi na Ufugaji)...Hapo ndipo elimu ya darasa huwekwa ktk majaribio badala ya kuwa kambi za mateso..
 
Mimi nina mtazamo tofauti kidogo. Lengo la JKT lilikuwa zuri na kiasi fulani ilisaidia kujenga ukakamavu, uzalendo, usawa (wote tulivaa sare za aina moja, kulala sehemu ziazofanana na kula kwenye Mess tins) na mtandao(Nikipita ofisi mbali mbali TZ hukutana na watu tuliokuwa jeshini pamoja).
JKT ilikuja kuharibiwa kutokana na ubadhirifu na hujuma za waliopewa dhamana ya kuisimamia. Aidha, viongozi na wachache wenye uwezo, nao walichangia kuiua JKT kwa kuwa hawakupenda kuwaona watoto wao wanapata "shida".
I enjoyed my time at the National Service and I am not regreting it-Mpiganaji

JKT ilikuwa ina umuhimu katika kujenga umoja miongoni mwa vijana wa Kitanzania toka mikoa mbali mbali, lakini 'viongozi' kutoka chama na serikali ndiyo walisababisha kuleta kasoro kubwa ndani ya JKT maana waliwatafutia watoto wao vyeti vya kila ugonjwa mbaya Tanzania ili kuhakikisha hawashiriki kabisa katika shughuli mbali mbali zikiwemo za mazoezi na uzalishaji. Kama wana mpango wa kuirudisha hiyo 2010 basi wahakikishe watoto wa viongozi hata wale watakaosoma nje ya nchi wanapitia huko na kuhenyeka kama wanavyohenyeka watoto wa wakulima na wafanyakazi, vinginevyo hakuna umuhimu wa kuirudisha JKT
 
JKT kimeo,nimekaa Ruvu mwaka mzima nikaambulia kujua kula mihogo mibichi na kunywa mayai mabichi basi.
 
Alisema pia kuwa, kupeleka majeshi katika nchi za nje kulinda amani kunasaidia kujenga mahusiano, ingawa pia alisema kuwa katika jeshi urefu na ufupi huhitajika kutegemea na kazi atakazofanya askari mhusika.

Source: Mwananchi

Uuuuuuiiiiii ! Magazeti sasa yameshajichokea.

Uhusiano wa kimataifa na physical qualification za mwanajeshi wapi na wapi ?

Halafu hawajaeleza hilo jeshi lilifutwa kwa nini na lini, hususan baada ya Waziri kusema JKT ni good idea, "ni wajibu."

Na likiwepo hilo jeshi la JKT usipojiunga nalo matokeo yake nini ?

Toa context mwandishi, toa background.

Otherwise, wananchi tunajadili vitu based on half-@$$ information. I mean, wale wanaosema hili jeshi ni zuri, linakutanisha vijana wa nchi nzima, linajenga ukakamavu and all that jazz, niambie, kwa nini mlilifuta ?

Na kilichofanya lifutwe wakati huo sasa hivi hakipo ? Utasikia sasa hivi tuna hela. Well, wakati ule hela zilienda wapi na sasa hivi hela mmepata wapi ? Uchumi umekua au Wizara ya Ulinzi imechimba madini ikapata hela ?

Poor Waziri, poor crummy press, poor old country of mine! Who shalt serve thy!
 
NImechelewa,lakini i could not let this pass without me commenting.
JKT ilikuwa supa.Na mara nyingi tulikuja kujua uzuri au faida yake baada ya kumaliza jeshi.Mi nakumbuka pale Ruvu tulikuwa tunatoroka na kwenda kwa Babu,then mchana tunavizia jikoni kama kuna mshkaji mpishi siku hio anakupa maharage na ugali ambao bado unakua kama uji,then unapotelea tena porini,huku mfukoni una Tanbond ambayo unachanganya kwenye maharage...kulikuwa hakuna chakula kitamu kama hicho! Acheni jama,JKT ilikuwa supa!
 
Serikali imeazimia kuyarejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa wahitimu wa elimu ya sekondari na vyuo kuanzia mwaka 2010.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi.

Alisema kurejeshwa kwa mafunzo hayo kunalenga kuwajengea vijana ukakamavu, kupenda utaifa na kujiajiri.

Dk. Mwinyi alisema mikakati ya wizara yake ni kupanua wigo wa ajira kwa kuwaajiri wahitimu wa elimu ya sekondari ambao pia watachangia kuwa na jeshi la kisasa litakalohimili ushindani wa kimataifa.
 
Serikali imeazimia kuyarejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa wahitimu wa elimu ya sekondari na vyuo kuanzia mwaka 2010.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi.

Alisema kurejeshwa kwa mafunzo hayo kunalenga kuwajengea vijana ukakamavu, kupenda utaifa na kujiajiri.

Dk. Mwinyi alisema mikakati ya wizara yake ni kupanua wigo wa ajira kwa kuwaajiri wahitimu wa elimu ya sekondari ambao pia watachangia kuwa na jeshi la kisasa litakalohimili ushindani wa kimataifa.

And who is gonna pay for these?EU,USAID ama George W Bush?Guess no one is gonna finance it!Mimi naunga mkono ila kweli its a total wastage of time,money and resources!
Wangekaa chini wakajiuliza kwa nini huko it failed before starting all over again!
 
Laukama JKT itachukua maana halisi ya neno hili na kujengwa upya kwa maana ya jina lake, nadhani itakuwa hatua moja muhimu sana ktk maendeleo ya Tanzania kwa sababu tuna kambi ambazo kweli zinaweza kutumika kama JESHI la KUJENGA TAIFA...

Tatizo la maneno ya kiswahili, mara nyingi hutafsrika kama ilivyo, JESHI:- Bila shaka ni wapiganaji wenye silaha. - LA KUJENGA TAIFA... Hapo ndipo tulipokwama tukafikiria wataweza kujenga vipi Taifa na bunduki za SMG au G5....?
Ni wakati muafaka wa kuwapatia vijana wetu waliomaliza masomo iwe secondary, au chuo Kikuu zana na vifaa vya utendeaji kazi, hilo jeshi la vijana wetu liwe na agenda moja kubwa ktk KUJENGA TAIFA badala ya kufundishwa nidhamu ya kijeshi na kuogopa (sio kuheshimu) viongozi.
 
Laukama JKT itachukua maana halisi ya neno hili na kujengwa upya kwa maana ya jina lake, nadhani itakuwa hatua moja muhimu sana ktk maendeleo ya Tanzania kwa sababu tuna kambi ambazo kweli zinaweza kutumika kama JESHI la KUJENGA TAIFA...

Tatizo la maneno ya kiswahili, mara nyingi hutafsrika kama ilivyo JESHI basi bila shaka ni wapiganaji wenye silaha..KUJENGA TAIFA... hapo ndipo tulipokwama tukafikiria wataweza kujenga vipi taifa na bunduki za SMG au G5....?
Ni wakati muafaka wa kuwapatia vija a wetu waliomaliza masomo iwe secondary, au chuo Kikuu zana na vifaa vya utendeaji kazi, hilo jeshi liwe na agenda moja kubwa ktk KUJENGA TAIFA badala ya kufundishwa nidhanu ya jeshini na kuogopa (sio kuheshimu) viongozi.

Well tunapoongolea kurudisha JKT lazima tuangalie na challenge za kisasa vile vile, ni mara nyingi tumesikia majambazi walikamatwa walikuwa wanajeshi au polisi ambao ni wastaafu au wapo kazini. Tutakapofundisha watu wengi jinsi ya kushika silaha na kuitumia kama sehemu ya mafunzo tumejiandaaje kwa watu kuja kutumia ujuzi huo mitaani watakapokosa la kufanya?
 
Nasikitika Sikuwahi pitia Jeshi....labda kwa kipindi nilipo fikia muda wa kwenda jeshi..lilikuwa limeshafutwa...

Ila nchi kama burundi,Rwanda,Congo,Ghana,Angola wana ka utaratibu kama tulio kuwa nao hapa wa baada ya kumaliza f6 unawekwenda jeshi...na ni ngumu kuendelea na masomo ya chuo bila kupitia Jeshi.Hii ni nzuri kwani mnakutana watu wa aina zote tanzania...mnafundishwa kuoishi na kuheshimiana...kuondoa umimi,ukabira,usomi..kwani pale hata kama ulitoka na Division 1 point 7 uko form 4 hapo haina thamani.

Wote ni sawa na mnakuwa sawa muda wote,unaondolewa ile dhana ya wewe ni bora kuliko wengine....ambayo kwa sasa vijana wengi wanabaguana kutokana na nani ana nini ana amesomea wapi.Ile dhana iliondolewa na jeshi.Rwanda wanaitumia sana kwa kuwa nchi ilipitia wakati mgumu sana 10 yrs back.

Mwanakijiji anasema ilikuwa ni kuwapotezea muda...lakini ilikuwa ikifanyika wakati wanafunzi wakiwa wanasubili kwenda vyuoni ule muda badala ya kukaa nyumbani walikuwa wanakwenda Jeshi.Achilia mbali matatizo iliyo kuwa nayo...ni kwasababu wengi wa maafande wakati huo shule ilikuwa fupi...walikuwa wanaona mtu anakuja toka f6 hapo kama ni tatizo na anakwenda chuo basi wanamtesa...

Kwa sasa wengi wao ni wasomi na wengine wanajiendeleza wanajua maana ya shule..kuwaaandaa hawa vijana waende kuwa wanancho bora...kuwapa ile spirit ya uzalendo.Ukakamavu...misimamo isiyo yumba...tena ingekuwa vyema wakaletwa wa cuba,Russia,China kufindisha jeshi hilo...

Am out.
 
Siku za karibuni nilisikia kwamba kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria(compulsory) limeanza tena.Hii imekaakaaje sasa?,malengo ni yale yale? ,Muundo ni upi ule wa zama zetu au mpya?.Naomba mwenye habari anihabarishe,kwani dhana ya uwepo wa Jeshi hilo kwa mujibu wa sheria achilia mbali kule kujitolea ulikuwa ukinipa shida sana kutafakari katika zama hizi.Kwani zama hizi za mafisadi sidhani kama kuna mtu au watu watakaokubali kupeleka watoto wao kwenye hilo Jeshi.
 
Mimi ningekuwa wa kwanza kujiunga tena: angalau kurefresh dozi ya uzalendo, uvumilivu, utaifa na umoja wetu -attibutes ambazo naona zinaanza kupotea haswa kwa vijana wetu!
 
Siku za karibuni nilisikia kwamba kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria(compulsory) limeanza tena.Hii imekaakaaje sasa?,malengo ni yale yale? ,Muundo ni upi ule wa zama zetu au mpya?.Naomba mwenye habari anihabarishe,kwani dhana ya uwepo wa Jeshi hilo kwa mujibu wa sheria achilia mbali kule kujitolea ulikuwa ukinipa shida sana kutafakari katika zama hizi.Kwani zama hizi za mafisadi sidhani kama kuna mtu au watu watakaokubali kupeleka watoto wao kwenye hilo Jeshi.

No, not such a weak state as we have now in Tanzania can dare launch JKT!
JKT without clear ideology? No, not possible! You can sit back and forget.
 
JKT bado ipo tu kwa mujibu wa sheria na wapo vijana wengi wanaojiunga kila mwaka. Na kwa taarifa ni kwamba Polisi, Magereza na TPDF wanaajiri vijana waliopitia JKT hivi sasa!
 
JKT bado ipo tu kwa mujibu wa sheria na wapo vijana wengi wanaojiunga kila mwaka. Na kwa taarifa ni kwamba Polisi, Magereza na TPDF wanaajiri vijana waliopitia JKT hivi sasa!

Mujibu wa sheria Mkuu ni kwamba kila amalizaye shule kidato cha sita au kozi nyinginezo baada ya kidato cha nne anawajibika kutumikia Taifa katika kipindi cha miezi sita hadi kumi na mbili.Najua kuwa JKT kwa kujitolea bado iliendelea hoja yangu hapa ni ile kwa mujibu tu!!
 
Wakuu nimesoma mahali kwamba serikali ina mpango wa kurudisha JKT kwa "wasomi wetu" naomba nieleweshwe vizuri kwa wale wenye data. Na pia je kuna umuhimu kweli katika kipindi hiki?
 
Haitaluwa na maana. Awamu hii ya nne ya kifisadi nadhani watoto wa mafisadi watakwepa JKT kwa kusaidiwa na wazazi wao, na kama vipi wataenda kusoma nje.
 
Back
Top Bottom