Mkuu, uzoefu wangu unaonyesha tofauti na haya unayoyasema. Mimi nilikwenda JKT, nilianzia Ruvu baadaye nikapelekwa Chita. Sikufundishwa chochote miongobni mwa hivyo ulivyoviorodhesha. Nilipokuwa Ruvu maafande walikuwa wanatupa mbinu za kuwaibia mayai ya kuku. Chita ilikuwa ni kama utumwa, watu 100 tulitakiwa kupalilia mpunga (kwa kung'oa magugu) kwenye shamba la ekari 100! CO aliomba dawa za kuua magugu (nadhani hicho ndicho kilimo bora) akanyimwa. bahati nzuri na yeye alikuwa mwelewa, akatuongoza katika mgomo wa kupalilia hadi madawa yalipoletwa, tena ilikuwa too late, hatyukuweza kupalilia hata robo ya mashamba tuliyokuwa tumepanda.Hiyo ndiyo JKT niliyopitia mimi, labda wewe mwenzetu una uzoefu tofauti