Nimeona wazazi wanalalamika kuwa watoto wao wamekataliwa kupokewa Hapo JKT Ruvu. Nashauri kama JKT nao hawajielewi hawawezi jiendesha wapewe DP World tu waiendeshe. Hakuna kucheka cheka na watu kwa sasa.
Tangazo lao liliorodhesha vifaa vifuatavyo
1. Bukta ya rangi ya 'dark blue' yenye mpira kiunoni, iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu
2. T-shirt ya rangi ya kijani (green vest)
3. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue
4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari
5. Soksi ndefu za rangi nyeusi
6. Track suit ya rangi ya kijani au blue
7. Nyaraka zote zinazohitajika katika udahili wa kujiunga na Elimu ya juu, zikiwemo cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kuhutimu kidato cha nne nk
Hata hivyo baada ya kufika kambini vijana katika baadhi ya kambi wameambiwa tangazo lililotoka halihusu kambi hilo hivyo wenyewe wana utaratibu wao wakaelekezwa wahakikishe vitu vifuatavyo vinapatikana haraka kama
1. Buti za maji au mvua (gum boot)
2. Mchango wa rambi rambi
3. Pesa ya matumizi
4. Rasketi ya kubebea vifaa
5. Pesa ya kwenda saluni!!
6. Karatasi na vifaa vingine vya stationery
7. Picha
8. Vitu vingine lukuki
Maswali yanaibuka kutoka kwa wazazi
1. Je, kwanini serikali imeitisha vijana wote waliomaliza kidato cha sita kwenda JKT kwa mjibu wa sheria huku wakiwabebesha gharama zote za vifaa vya kutumia wakati wana bajeti kwa ajili ya programu hiyo ya uzalendo?
2. Kwanini serikali kupitia jeshii la kujenga taifa ilitoa tangazo ambalo halijabeba mahitaji kwa kila kambi badala ya kuacha vijana mpaka wafike kambini kisha wapate usumbufu? Si bora wangeteua makundi kwa zamu kwa kulingana na uwezo wa kuwahudumia badala ya kuwabebesha wazazi gharama kwa masuala ambayo serikali ndio inataka kujenga maadili na uzalendo wa kizazi cha vijana wa sasa?
3. Je, serikali haijabaini kwamba vijana walioitwa kwa mafunzo hayo kiakili hawatakuwa sawa maana wanahisi wananunua kile watakacho funzwa hivyo hawatokuwa tayari kutumia kwa hiari mpaka walipwe pesa wakimaliza?
Mwisho
1. Serikali kupitia jeshi letu ambalo limejaa wataalamu wenye weledi wa kutosha tafadhali toeni wa mafunzo hayo bila kuwabebesha wazazi gharama zinazowaumiza kiasi ambacho kinawafanya walalamike na kuona hakuna faida yoyote vijana wao kwenda JKT
2. Utofauti wa mahitaji ya vifaa katika kila kambi ubebwe na serikali maana ndio waliowaita maana wazazi wao ni walipa kodi kodi wazuri hivyo waangalia jinsi bora ya kuendesha mafunzo hayo pasipo kusababisha mfadhaiko wa kisaikolojia
Nimewasilisha maoni haya kama mdau wa JKT niliyewahi kutumikia kwa mjibu wa sheria mwaka mzima miaka ya 80s ambapo tuliyafaidi kwa kupata mafunzo yaliyo bora yaliyotuwezesha kuwa mabingwa wa 'justle' katika changam,oto yoyote inayojitokeza maishani bila kukata tamaa.
MAJUKUMU MEMA jeshi la kujenga taifa.