JKT Tanzania yatoa pole kufuatia Pacome Zouzoua kuvunjika mguu

JKT Tanzania yatoa pole kufuatia Pacome Zouzoua kuvunjika mguu

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Uongozi wa JKT Tanzania FC umetoa taarifa kwa umma ukieleza kusikitishwa na tukio la kuumia kwa kiungo wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, baada ya kugongana na mchezaji wa JKT Tanzania, Hassan Wahabi, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa Juni 30, 2025, katika Uwanja wa Major General Isamuhyo.

Katika taarifa hiyo, klabu hiyo imeeleza kuwa tukio hilo halikuwa la makusudi, huku ikibainisha kuwa Wahabi naye amesikitishwa na majeraha aliyoyapata Zouzoua kutokana na tukio hilo ambalo halikutarajiwa.

JKT Tanzania pia imetoa pole kwa Pacome Zouzoua na kumtakia apone haraka ili arejee uwanjani kuendelea kuonyesha kiwango chake.

Taarifa kwa umma

Klabu ya JKT Tanzania FC imetoa pole na kuomba radhi kwa mchezaji wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, kufuatia majeraha mabaya aliyopata katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara hapo jana June 30,2026 uwanja wa Jenerali Isamuhyo dhidi ya Yanga SC, mchezo uliomalizika kwa Yanga kushinda kwa magoli 3-0.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya JKT Tanzania FC, Uongozi wa klabu umesema umehuzunishwa na tukio la kuumia kwa Zouzoua yaliyosababibishwa na mchezaji wao Hassan Wahabi. Tukio hilo lilitokea wakati wachezaji hao wakiwania mpira katika mchezo wa JKT Tanzania FC dhidi ya Yanga SC uliochezwa Uwanja wa Major General Isamuhyo tarehe 30 Juni 2025.

Kwa niaba ya mchezaji Hassan Wahabi, uongozi umesema unaomba radhi kwa tukio hilo ambalo halikuwa la kimakusudi. JKT imesema kile kilichotokea kimsababishia maumivu makali Zouzoua na kummiza kifika mchezaji wao Wahabi, kwani Wahabi hakukusudia wala kutarajia kumjeruhi mwenzake.

Aidha, JKT Tanzania FC imetoa pole ya dhati kwa Zouzoua na kumtakia apone haraka. Klabu imesema inamuombea kwa Mwenyezi Mungu arejee katika hali yake ya kawaida na kuendelea kucheza mpira kwa kiwango na ubora wake wa siku zote.

photo_2026-07-01_10-41-41.jpg
 
Dah

Vijana sisi sote tunatafuta maisha acheni roho mbaya mtazani warundi

MUNGU akujalie uponyaji mpiganaji mwenzangu pacome kwa jina la YESU KRISTO
 
Baada ya kugongana??? Waligongana wale au alimfyeka?

Nchi hii kila kitu siasa tu nyoko kabisa.
 
Back
Top Bottom