Joash Onyango Ajiunga na Kenya Police FC, Umri Wake Wazua Mjadala

Joash Onyango Ajiunga na Kenya Police FC, Umri Wake Wazua Mjadala

Beki mkongwe mwenye jina kubwa katika soka la Afrika Mashariki, Joash Onyango, amezua gumzo mara baada ya kujiunga rasmi na kikosi cha Kenya Police FC akitokea timu ya Dodoma Jiji ya Tanzania. Onyango, ambaye amewahi kung’ara na miamba wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC na Singida Black Stars, anatajwa kuwa na umri wa miaka 26, ingawa mitandaoni mashabiki wanazidi kufanya utani wakidai ana umri wake ni miaka 62.
View attachment 3459565
Onyango mwenye miaka 26 anasifika kwa kuwa mchezaji mwenye nguvu, uzoefu mkubwa wa kimataifa na nidhamu ya kipekee katika safu ya ulinzi. Katika misimu aliyocheza nchini Tanzania, alijijengea sifa ya kuwa beki asiyeogopa changamoto, akiwazuia washambuliaji hatari na mara nyingi akitoa uongozi ndani ya uwanja.
View attachment 3459566
Ujio wake ndani ya Kenya Police FC unatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya kikosi hicho kinachopania kupigania nafasi za juu katika Ligi Kuu ya Kenya. Mashabiki wengi wa Polisi wamesema hatua hii ni “saini ya kipekee” itakayoleta uthabiti na uzoefu kwa vijana waliopo.
Okwiii
 
huyu chammtotooooo

okwi.kaja ana 26

kavheza miaka kadhaa

kaenda nje ya nchi sio Kenya ana

26 chezea okwi wewekarudi kwao uganda ana 26

hata kuweka 26.5 tumsamehe hakuwa na huruma huyu mtu
 
huyu chammtotooooo

okwi.kaja ana 26

kavheza miaka kadhaa

kaenda nje ya nchi sio Kenya ana

26 chezea okwi wewekarudi kwao uganda ana 26

hata kuweka 26.5 tumsamehe hakuwa na huruma huyu mtu
Wanafanya ku-rewind na ku-pause miaka 😃
 
ni vile hazingatii skin care mkuu, halafu ule ukomavu ni wa ukoo
Hahahaaa 😆 😂 😆 😂
Umenikumbusha nilipoanza kazi nilikuwa na kademu kamoja nikakatajia na miaka yangu baada ya miaka 4 akanza kuliwa na boss wangu

Nkamvamia rafiki yakee baada ya mwaka akaniuliza na miaka mingapi nkamtajia 28 wooh una mwili ....

Asciende kumuliza recho hee 👌 hivi mpwa ana miaka.mingapi akamwambia nikiwa nae alikuwa na 28 demu Kuja akaniuliza tena nikamuliza unadate na miaka ama mm

Hakurudi tena

So.wakati mwingine ukweli huaribu bahati ya mtu
 
Wengi hamjaelewa,jamaa ana miaka 26 akiwa anacheza soka la ushindani. Kama alianza na miaka 18 ujumulishe 26 unapata 44. Hivyo umri sahihi wa onyango ni 44+
 
Bila kujali umri wake, wakati akiwa Simba jamaa huyu kwa kusaidiana na Ilonga walikuwa wanajua kuziba geti kweli kweli.
 
Kwa huu muonekane wake na hizo ndevu nyeupe hapana aisee yaani huyu akiwa kinda sana basi ni miaka 48.
Kwamba anataka kutufanya sisi wote macho yetu hayaoni vizuri
 
Back
Top Bottom