Mkuu,kutafutiwa kazi pia ni kazi.Kama unaona kwamba huwezi gharama za kutafutiwa kazi tafuta kazi za bure zipo nyingi sana.Utapeli na matapeli wapo tu ni we ujue jinsi ya kujihami.
JOB JUNCTION ni MATAPELI.
Mimi na jamaangu tuliona tangazo lao wanataka Supervisor ( jamaangu kasoma education Mimi nimesoma Engineering), ilibidi wote tutume bila kujali elimu zetu maana walitaka mtu mwenye degree au diploma (Bila kuspecify degree au diploma ya nn).
Ajabu wote tukatumiwa sms tuwapigie, tukapiga, wakasema kesho tupeleke cv ofisin kwao.
Tulipoenda tunakuta tupo zaid ya 50 tukaanza kuingia kwa magroup maana kaofisi ni jadogo ( nikagundua yeyote aliyeomba ile kazi aliitwa maana tulikutana watu tumesoma koz tofauti tofauti).
Wakasema kujaza fomu ni elf 50 kama skosei, ila ukishajaza ndo wataanza kusambaza cv yako kwenye kampun mbalimbali ili uitwe kwenye interview (ina naana ile post ya Supervisor ilikuwa chambo ili wapate watu.)
Basi kesho yake wote tukapigiwa simu kuwa tunequalify kwenda kujaza fomu, nikajiuliza inakuwaje Huyu kasoma education Mimi engineering alafu wote tuqualify kufanya Kaz moja, tukampigia jamaa mmoja tulikutana nae kule (yeye kasoma pharmacy), nae akasema kapigiwa akajaze fomu, tukaconclude hawa ni MATAPELI.
Kama ni kweli wanawatafutia watu ajira, kwanini wasisubiri nikishapata ndo wanikate asilimia kadhaa au hata mshahara mzima kucover cost zao?.
Kwann watake niwalipe kabla hawajafanya kazi?, KIJANA SHTUKA MATAPELI HAO, Usitoe pesa kabla hujapata kazi.
Sent from my Nokia C1 using
JamiiForums mobile app