Mzee wa Code
Member
- Sep 23, 2024
- 82
- 227
Ni wazuri wa kuhimiza vijana wajiajiri, lakini wao wenyewe hawana ujanja wa kujiajiri. Atakula nini akiacha siasa?NDUGAI ABADILI MSIMAMO: SASA AUTAKA TENA UBUNGE WA KONGWA
Kongwa, Dodoma
Aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa kwa zaidi ya miongo miwili, Job Ndugai, ameibua mjadala mpya katika siasa za jimbo hilo baada ya kutamka kuwa atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025—miezi kadhaa baada ya kutangaza kuwa hatagombei tena.
Kauli hiyo imekuja kama mshangao kwa wengi, hasa baada ya kampeni za awali kufanywa na mke wake, ambaye alikuwa anatajwa kuwa ndiye anayetarajiwa kurithi kijiti hicho cha kisiasa kupitia baraka za mumewe.
Ndugai, ambaye ameiongoza Kongwa tangu mwaka 2000, amenukuliwa katika kikao cha ndani cha kimkakati akisema, "Wananchi wamenitaka, siwezi kuwakataa." Kauli hiyo imechukuliwa na baadhi ya wachambuzi kama ishara ya kuanza rasmi kurejea kwake kwenye ulingo wa kugombea, huku wengine wakiona ni mwitikio wa hali ya kisiasa ndani ya chama au maoni ya wapiga kura.
Mabadiliko haya ya msimamo yanaibua maswali mengi kuhusu hatma ya mipango ya awali ya kumpitisha mkewe kuwa mrithi wake kisiasa, pamoja na athari zake kwa wanachama wengine wa CCM waliokuwa wameanza kuonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo.
Endelea kufuatilia kwa undani, kwani kampeni za Kongwa 2025 zinaanza kuchukua sura mpya—na ya kusisimua zaidi.
mzee wa kodi naendele kukupa code za watia nia wote na majimbo wanayotaka kugombea
je unadhani kuna umuhimu wa kuwa na sheria ya ukomo wa ubunge kama urais?Ni wazuri wa kuhimiza vijana wajiajiri, lakini wao wenyewe hawana ujanja wa kujiajiri. Atakula nini akiacha siasa?
Hii kama vile haijakaa sawa!Mbona kama ya kutunga!Aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa kwa zaidi ya miongo miwili, Job Ndugai, ameibua mjadala mpya katika siasa za jimbo hilo baada ya kutamka kuwa atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025—miezi kadhaa baada ya kutangaza kuwa hatagombei tena.
Mei 2022, Ndugai alisema hatogombea tena ubunge. Zaidi soma Job Ndugai: Sitagombea tena ubunge 2025!
Kauli hiyo imekuja kama mshangao kwa wengi, hasa baada ya kampeni za awali kufanywa na mke wake, ambaye alikuwa anatajwa kuwa ndiye anayetarajiwa kurithi kijiti hicho cha kisiasa kupitia baraka za mumewe.
Ndugai, ambaye ameiongoza Kongwa tangu mwaka 2000, amenukuliwa katika kikao cha ndani cha kimkakati akisema, "Wananchi wamenitaka, siwezi kuwakataa." Kauli hiyo imechukuliwa na baadhi ya wachambuzi kama ishara ya kuanza rasmi kurejea kwake kwenye ulingo wa kugombea, huku wengine wakiona ni mwitikio wa hali ya kisiasa ndani ya chama au maoni ya wapiga kura.
Mabadiliko haya ya msimamo yanaibua maswali mengi kuhusu hatma ya mipango ya awali ya kumpitisha mkewe kuwa mrithi wake kisiasa, pamoja na athari zake kwa wanachama wengine wa CCM waliokuwa wameanza kuonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo.
Endelea kufuatilia kwa undani, kwani kampeni za Kongwa 2025 zinaanza kuchukua sura mpya—na ya kusisimua zaidi.
Mzee wa kodi naendele kukupa code za watia nia wote na majimbo wanayotaka kugombea
Pia soma
- Tetesi: - Job Ndugai anajipanga kuliachia Jimbo la Kongwa kwa mkewe Bi. Fatma
Yaani kama anaua nyoka na huwa hachukuliwi hatua yoyote ya kisheria licha ya kutenda JINAI upenunihuyu anatembeaga na fimbo tena huwa anapiga za kichwa
Zile nyumba za tembe ndiyo kutukukaKazi zake ni zakutukuka, mitano tena
Ni mpuuzi sana! Alikuwa kibaraka wa jiwe!Aje tena atunge sheria za kuwawekia kinga wakuu wa mikoa.