PreGE2025 Job Ndugai abadili msimamo, sasa autaka tena ubunge wa Kongwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa kwa zaidi ya miongo miwili, Job Ndugai, ameibua mjadala mpya katika siasa za jimbo hilo baada ya kutamka kuwa atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025—miezi kadhaa baada ya kutangaza kuwa hatagombei tena.

Mei 2022, Ndugai alisema hatogombea tena ubunge. Zaidi soma Job Ndugai: Sitagombea tena ubunge 2025!

Kauli hiyo imekuja kama mshangao kwa wengi, hasa baada ya kampeni za awali kufanywa na mke wake, ambaye alikuwa anatajwa kuwa ndiye anayetarajiwa kurithi kijiti hicho cha kisiasa kupitia baraka za mumewe.

Ndugai, ambaye ameiongoza Kongwa tangu mwaka 2000, amenukuliwa katika kikao cha ndani cha kimkakati akisema, "Wananchi wamenitaka, siwezi kuwakataa." Kauli hiyo imechukuliwa na baadhi ya wachambuzi kama ishara ya kuanza rasmi kurejea kwake kwenye ulingo wa kugombea, huku wengine wakiona ni mwitikio wa hali ya kisiasa ndani ya chama au maoni ya wapiga kura.

Mabadiliko haya ya msimamo yanaibua maswali mengi kuhusu hatma ya mipango ya awali ya kumpitisha mkewe kuwa mrithi wake kisiasa, pamoja na athari zake kwa wanachama wengine wa CCM waliokuwa wameanza kuonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo.

Endelea kufuatilia kwa undani, kwani kampeni za Kongwa 2025 zinaanza kuchukua sura mpya—na ya kusisimua zaidi.

Mzee wa kodi naendele kukupa code za watia nia wote na majimbo wanayotaka kugombea

Pia soma
- Tetesi: - Job Ndugai anajipanga kuliachia Jimbo la Kongwa kwa mkewe Bi. Fatma
Unadhani mtaani ni kuzuri Kukaa bila Kuitwa mheshimiwa 😁😁
 
May 22, Ndugai alitangaza msiamamo wa kutogombea ubunge kwa kuwa alijua atagombea urais. Lkn mama Abdul ameruka sarakasi na kujitangaza kuwa mgombea pekee.
 
Aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa kwa zaidi ya miongo miwili, Job Ndugai, ameibua mjadala mpya katika siasa za jimbo hilo baada ya kutamka kuwa atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025—miezi kadhaa baada ya kutangaza kuwa hatagombei tena.

Mei 2022, Ndugai alisema hatogombea tena ubunge. Zaidi soma Job Ndugai: Sitagombea tena ubunge 2025!

Kauli hiyo imekuja kama mshangao kwa wengi, hasa baada ya kampeni za awali kufanywa na mke wake, ambaye alikuwa anatajwa kuwa ndiye anayetarajiwa kurithi kijiti hicho cha kisiasa kupitia baraka za mumewe.

Ndugai, ambaye ameiongoza Kongwa tangu mwaka 2000, amenukuliwa katika kikao cha ndani cha kimkakati akisema, "Wananchi wamenitaka, siwezi kuwakataa." Kauli hiyo imechukuliwa na baadhi ya wachambuzi kama ishara ya kuanza rasmi kurejea kwake kwenye ulingo wa kugombea, huku wengine wakiona ni mwitikio wa hali ya kisiasa ndani ya chama au maoni ya wapiga kura.

Mabadiliko haya ya msimamo yanaibua maswali mengi kuhusu hatma ya mipango ya awali ya kumpitisha mkewe kuwa mrithi wake kisiasa, pamoja na athari zake kwa wanachama wengine wa CCM waliokuwa wameanza kuonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo.

Endelea kufuatilia kwa undani, kwani kampeni za Kongwa 2025 zinaanza kuchukua sura mpya—na ya kusisimua zaidi.

Mzee wa kodi naendele kukupa code za watia nia wote na majimbo wanayotaka kugombea

Pia soma
- Tetesi: - Job Ndugai anajipanga kuliachia Jimbo la Kongwa kwa mkewe Bi. Fatma
Nilipita Kongwa mwaka Jana niliumua Sana nikajiuliza jamaa ana jina kubwa lakini hakuna cha maana alichokifanya jimboni, nimepita baadhi ya wilaya za mkoa wa Dodoma kwa upande wangu Kongwa ni ya mwisho yupo yupo tu kajaza.miradi yake, poleni wana Kongwa mnaumizana wenyewe kwa wenyewe, maana waroho watampitisha tu.
 
Kauli hiyo imekuja kama mshangao kwa wengi, hasa baada ya kampeni za awali kufanywa na mke wake, ambaye alikuwa anatajwa kuwa ndiye anayetarajiwa kurithi kijiti hicho cha kisiasa kupitia baraka za mumewe.

Ndugai, ambaye ameiongoza Kongwa tangu mwaka 2000, amenukuliwa katika kikao cha ndani cha kimkakati akisema, "Wananchi wamenitaka, siwezi kuwakataa." Kauli hiyo imechukuliwa na baadhi ya wachambuzi kama ishara ya kuanza rasmi kurejea kwake kwenye ulingo wa kugombea, huku wengine wakiona ni mwitikio wa hali ya kisiasa ndani ya chama au maoni ya wapiga kura.
1744123028085.png
 
Maskini wakaguru na wagogo ndio wenye bahati mbaya ya kupata viongozi wasioweza kuwasaidia chochote!!na Kibajaji ni janga hilohilo
Hata Simbachawene ni janga tupu, ndiyo maana ni ngumu kukuta mfanyabishara tajiri mgogo Dodoma wala Tanzania
 
Wale watu sijui shida ni nini nikisema ni laana pengine nako pia naweza kuwa nakosea,wamechoka mno jamani.
Dodoma ni kwao lakini kukuta hata hardware ya mgogo ni ngumu sn, lakini wana mawaziri wanne, Yule bonge wa vijana sijui ana ajira, Simbachawene, Anthony Mavunde na Kijaju sijui wa Kondoa lakini kote ni masikini wa kutupwa
 
Back
Top Bottom