Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Haya maneno kaongea yeye???
Sasa 2025 itaamua. Mkitoa waliopo sawa. Waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa endepo hiyo ndo namna ya kuendesha Nchi

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ndugai nae kichwa cha mgogo hakina akili, leo ndio anashtuka deni ni kubwa?
Kama anajua nchi yetu imelemewa na madeni, angekataa kabisa kabisa mradi hatari wa Bagamoyo, ambao kwa historia za nchi za kiafrika, huo mradi utakuwa ni deni na mzigo mkubwa sana kwetu.

Mradi wa Bagamoyo, ni karibu $ 10 bil, sawa na tshs 23 trillions ambazo wawekezaji watawekeza, of which hatujui hatma yake kwa nchi yetu, narudia, kwa historia za nchi zote za Afrika, miradi kama hii imegeuka kitanzi na kaburi zao.

Mh. Speaker angejua deni kubwa, mradi kama huo wa Bagamoyo angekaa mbali nao.
 
Wanakumbuka Shuka Kumekucha ,endeleeni kugonga meza tu huko mjengoni.
CCM ilishapoteza dira kitambo sana.
 
Spika wa Bunge ameonya kitendo cha serikali kuendelea kutegemea mikopo kutoka nje kuendesha nchi kitu ambacho kimefanya deni la taifa kuwa kubwa maradufu "Ipo siku hii nchi itapigwa mnada,kopeni tu".

View attachment 2060343
Nchi hii ina ela ila inaishia mifukoni mwa watu na matumizi yasiyo na tija na bado wanataka watutoze ili tuendelee kugharamia lifestyle lao.
Just imagine sasa mawaziri wako dar badala ya dodoma, hivyo wana makazi dar na dodoma gharama nyingine hiyo ya kuendesha magari na makazi yao.
Ela nyingi inaishia kwenye mifuko yao
 
Angefanya hata comparison kabla hajafanya conclusion hata na majirani wetu kenya.

Kenya deni la taifa na uwiano na GDP ni 67% na Tanzania ni 35%.

Hata mataifa makubwa yana madeni makubwa sana kama wafanyabishara wakubwa sana cha muhimu ni kuhakikisha kunakuwa na transparency na monitoring nzuri ya hiyo mikopo.
 
suluhisho ni lipi sasa kama yeye spika analalamika na yupo kwenye chombo kikubwa cha maamuzi bunge ambalo ni mhimili wa nchi ..bila shaka anajua wananchi wanaumia kiasi gani kwa makosa wanayo yafanya ifike mahala waangalie na wajue wananchi ndio wenye nchi sio watu wachache walioko kwenye power ata maamuzi wayapembue kikamilifu kwa mustakabali wa wananchi.
 
Hela ipo ila usimamizi sio mzuri! Tatizo linalotukwamisha ni usimamiz wa rasilimali zetu tumewapa madaraka watu wa hovyo!
 
Hakuna lolote, roho mbaya tu inawasumbua
Leo ndio mumeona deni kuwa kubwa?
Mama kaa chonjo watu wanajipanga ujueeee
 
Kati ya hizo pesa za mikopo tunamdai BILION 26 na ushee zilizotumika kumtibia maradhi yake India na kumfanya kuwa mgonjwa ghali zaidi duniani anayetarajiwa kuingia kwenye kitabu cha Guiness book of world records
Punguza kuwa Negative siku zote mkuu, wewe siku ukiigua ndugu na jamaa wakakuchangia ukapate matibabu wakikusema utajisikiaje.

Jaribu kutumia kichwa kufikiria sio kila kitu unaandika kwa kufikiria matako tu.
 
Ndungai Ndungai Ndungai, nimekuita mara ngapi? Umeamua sasa kutoka hadharani kumkabili Samia kuonyesha kuwa sasa Sukuma Gang mko tayari kwa mpambano? Shauri yenu
 
Aibu yake kageuka kuwa mpinzani ndani ya bunge lake mwenyewe.
Ndiyo wanavuna dhambi ya kuiba kura na kulifanya Bunge la kijani tupu lililosheheni vilaza kama kina Babu Tale na mazuzu wengine bila kuwasahau wale wahuni covid 19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…