Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Sasa hivi dni linakimbilia tr 90
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi hawakuridhia kama inavyosema na baadhi ya wanasiasa.

Kwa maneno hayo naona kuna mambo yanaendelea huko Lumumba yapo mambo hayajakaa sawa ukiona spika anaanza kulalamikalalamika! Alianza kuhusiana na serikali kuhamia Dodoma kuwa kwa sasa kazi zote za serikali na makongamano zimerudishwa Dar-es-Salaam.

Mheshimiwa Ndugai popote ulipo nakwambia hivi wewe na viongozi wako mnaifanyia nini hii nchi mbona mnakaa mnalalamika lalamika wakati chama ni cha kwenu na chama chenu ndicho kimeunda serikali.?

=====

UPDATES;

=====

=> Watu wengi wanatulaumu sana, ninyi ndio Wasomi. Hebu fikiria, Juzi mama kaenda kukopa 1.3 Trilioni deni.

=> Na tuna majengo hivi sasa ya Madarasa, ya Vituo vya afya, ambayo yanajengwa kwa tozo. Hivi ipi bora? Sisi Watanzania wa miaka 60 ya Uhuru tuendelee kukopa na Madeni au tubanane banane hapa tujenge wenyewe bila madeni Makubwa yasiyoeleweka? Ni lini tutajenga wenyewe?

=> Tutembeze bakuri ndo heshima? na tukishakopa tunapiga makofi! Sisi wa kukopa kila siku?

=> Tukasema pitisha Tozo, anayetaka asiyetaka, pitisha Tozo. Lazima tuanze kujenga wenyewe. Nani atatufanyia? Yupo wapi huyo Mjomba? Tukapitisha Tozo.

=> Sasa 2025 itaamua. Mkitoa waliopo sawa. Waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa endepo hiyo ndo namna ya kuendesha Nchi.

=> Hivi sasa deni letu ni 70 Trilioni. Hivi ninyi si Wasomi? Is that healthy? Kuna siku nyi itapigwa mnada hii. Madeni Madeni Madeni

=> Bajeti yetu Trilioni 30, Trilioni 10 kati ya hizo kwa Mwaka tunalipa Madeni.

=> Tumeenda Kukopa 1.3 Trilioni, Tunapiga Makofi. Tunawapa Wazungu Trilioni 10 Mariba Matupu. Wanatufanya Sisi Mazezeta. Hela yako Mwenyewe. Anachukua hela yako, halafu anakupa Kidogo Unashangilia.

=> Toza fanya hivi, tujitegemee, Tusimame wenyewe. Kuna ubaya gani? Hata msomi anatupinga.
View attachment 2060338

Zaidi, soma: Thread 'Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏' News Alert: - Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏
Sasa hivi deni linachupa mwendo wa kupaa ndege
 
Mwendazake alikopa mara mbili ya jakaya,mama kakopa ukikusanya kuanzia nyerere,mwinyi,mkapa,Jk na JpM ndio mkopo jumla wa mama
Ok nimekuelewa sana
labda nikuulize rais akikopa hela zinakua zake? Halafu tunalipa sie au zinakuwa zetu wote halafu analipa yeye pekee?
Manake awamu tano za miaka hamsini zishindwe na mwaka mmoja?
Hii kali kuliko
 
Kwa King-Eleza
Akimbie Kushika Uraisi.

Tunahitaji wenye Kujali Uhuru wa Kweli.
 
“Kuna siku nchi itapigwa mnada hii” - Job Ndugai, 28/12/2021

Job Ndugai alisema mkopo wa fedha wa Sh1.3 trilioni kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ili kukabiliana na athari za kiuchumi za COVID-19 (ambazo walizipeleka kusikoonekana), malipo na riba ya mkopo huo ni Sh10 trilioni

Bila tashwishi na kupepesa macho, hii ni biashara kichaa.

Inapelekea mpaka Walimu wiliya ya Mvomero hawajalipwa Mishahara Yao.

Na tunakoelekea kuna siku kweli hii nchi itapigwa mnada, mikopo imekuwa mikopo. Madeni na Tanzania, Tanzania na madeni. MADENI WALIMU.

Tozo zinazidi kuongezwa kila kukicha haijulikani zinatumika wapi na kukopa wanazidi kukopa kazi ipo.

Mr mkiki.
View attachment 2493902
 
Sasa watu kuchelewa kulipwa mishahara na mikopo kuna uhusiano gani?

At least ingekuwa kipindi cha mkapa wangecheleweshewa mishahara ni sawa kwasababu yeye alikuwa anafanya kila namna ya kurudisha deni
 
Sasa watu kuchelewa kulipwa mishahara na mikopo kuna uhusiano gani?

At least ingekuwa kipindi cha mkapa wangecheleweshewa mishahara ni sawa kwasababu yeye alikuwa anafanya kila namna ya kurudisha deni
CCM imechoka!! Nchemba hajui lolote.
 
“Kuna siku nchi itapigwa mnada hii” - Job Ndugai, 28/12/2021

Job Ndugai alisema mkopo wa fedha wa Sh1.3 trilioni kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ili kukabiliana na athari za kiuchumi za COVID-19 (ambazo walizipeleka kusikoonekana), malipo na riba ya mkopo huo ni Sh10 trilioni

Bila tashwishi na kupepesa macho, hii ni biashara kichaa.

Inapelekea mpaka Walimu wiliya ya Mvomero hawajalipwa Mishahara Yao.

Na tunakoelekea kuna siku kweli hii nchi itapigwa mnada, mikopo imekuwa mikopo. Madeni na Tanzania, Tanzania na madeni. MADENI WALIMU.

Tozo zinazidi kuongezwa kila kukicha haijulikani zinatumika wapi na kukopa wanazidi kukopa kazi ipo.

Mr mkiki.
View attachment 2493902

Wakipiga mnada waturuhusu wananchi tutoke nje ya nchi
Nichi isijepigwa mnada na watu wake [emoji1781]
 
Labda hyo inaweza kuwa ni point
Ndio unataka kusema unajua Leo. Yani CCM wanasema wanaendeleza Nchi kwa Tozo na buku za Umeme kila mwezi.

Wakati Rasilimali za nchi zipo kibao.

Walimu hawapati hela tena mwezi huu.
 
“Kuna siku nchi itapigwa mnada hii” - Job Ndugai, 28/12/2021

Job Ndugai alisema mkopo wa fedha wa Sh1.3 trilioni kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ili kukabiliana na athari za kiuchumi za COVID-19 (ambazo walizipeleka kusikoonekana), malipo na riba ya mkopo huo ni Sh10 trilioni

Bila tashwishi na kupepesa macho, hii ni biashara kichaa.

Inapelekea mpaka Walimu wiliya ya Mvomero hawajalipwa Mishahara Yao.

Na tunakoelekea kuna siku kweli hii nchi itapigwa mnada, mikopo imekuwa mikopo. Madeni na Tanzania, Tanzania na madeni. MADENI WALIMU.

Tozo zinazidi kuongezwa kila kukicha haijulikani zinatumika wapi na kukopa wanazidi kukopa kazi ipo.

Mr mkiki.
View attachment 2493902
Mkuu nenda Taratibu kwa post za aina hii unafanya JF Iwe kama kijiwe cha Kahawa. Serikali inalipa Mishahara kwa watumishi wake wote kwa wakati mmoja kupitia BOT kwa mifumo ya kielektroniki, kwa kifupi haaachwi mtu yaani is just Click mshiko unakufikia muda huo huo. aidha akaunti ya Benki ikiwa imekosewa ama mwajiri kamuondoa mtumishi kwenye mfumo kwa sababu zake yeye hapo atakosa. Na mshahara wanalipa from 21 -23 ya kila mwezi.
Ni ngumu sana uskie Kakonko wamelipwa na Mvomero bado hapo ikitokea tatizo litakuwa sio la Wizara/Serikali kuu bali tatizo litakuwa la mwajiri yaaani DED husika atakuwa kafanya uzembe na mara nyingi wanapewa onyo au adhabu zinginezo.
 
Back
Top Bottom