Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi hawakuridhia kama inavyosema na baadhi ya wanasiasa.

Kwa maneno hayo naona kuna mambo yanaendelea huko Lumumba yapo mambo hayajakaa sawa ukiona spika anaanza kulalamikalalamika! Alianza kuhusiana na serikali kuhamia Dodoma kuwa kwa sasa kazi zote za serikali na makongamano zimerudishwa Dar-es-Salaam.

Mheshimiwa Ndugai popote ulipo nakwambia hivi wewe na viongozi wako mnaifanyia nini hii nchi mbona mnakaa mnalalamika lalamika wakati chama ni cha kwenu na chama chenu ndicho kimeunda serikali.?

=====

UPDATES;

=====

=> Watu wengi wanatulaumu sana, ninyi ndio Wasomi. Hebu fikiria, Juzi mama kaenda kukopa 1.3 Trilioni deni.

=> Na tuna majengo hivi sasa ya Madarasa, ya Vituo vya afya, ambayo yanajengwa kwa tozo. Hivi ipi bora? Sisi Watanzania wa miaka 60 ya Uhuru tuendelee kukopa na Madeni au tubanane banane hapa tujenge wenyewe bila madeni Makubwa yasiyoeleweka? Ni lini tutajenga wenyewe?

=> Tutembeze bakuri ndo heshima? na tukishakopa tunapiga makofi! Sisi wa kukopa kila siku?

=> Tukasema pitisha Tozo, anayetaka asiyetaka, pitisha Tozo. Lazima tuanze kujenga wenyewe. Nani atatufanyia? Yupo wapi huyo Mjomba? Tukapitisha Tozo.

=> Sasa 2025 itaamua. Mkitoa waliopo sawa. Waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa endepo hiyo ndo namna ya kuendesha Nchi.

=> Hivi sasa deni letu ni 70 Trilioni. Hivi ninyi si Wasomi? Is that healthy? Kuna siku nyi itapigwa mnada hii. Madeni Madeni Madeni

=> Bajeti yetu Trilioni 30, Trilioni 10 kati ya hizo kwa Mwaka tunalipa Madeni.

=> Tumeenda Kukopa 1.3 Trilioni, Tunapiga Makofi. Tunawapa Wazungu Trilioni 10 Mariba Matupu. Wanatufanya Sisi Mazezeta. Hela yako Mwenyewe. Anachukua hela yako, halafu anakupa Kidogo Unashangilia.

=> Toza fanya hivi, tujitegemee, Tusimame wenyewe. Kuna ubaya gani? Hata msomi anatupinga.
View attachment 2060338

Nilishawai kusema mama simuelewi kabisa!! Na bado anaonekana ni mwenye kujikweza lazima atafakari kwann spika aseme ivyo!!!!! Ukishaona wanaongea hadi tunasikia huku nje ujue moshi umeshaonekana unapofuka..... mama akae vizuri na hawa Akina January na mwigulu watamponza
 
Labda ameona Bandari ya Bagamoyo imepotezewa wakati aliishakarimiwa kupitia Sino-Africa Blackmail, mimi nafikiri tupunguze matumizi ya Mhimili wa Bunge ili tulipie mikopo hiyo. Mbona Raila alimbana Kibaki hadi wabunge wakapunguziwa maslahi na serikali ikapumua.
Magufuli alipunguza hadi mshahara wake aki-reflect Nyerere Model. Tupunguze mishahara ya wabunge.
 
Basi tutumie mfuko wa jimbo kulipia deni la taifa. JMT ina majimbo ya uchaguzi 239 X 1,000,000,000/ @ = Tzs. 239,000,000,000/-

Mfuko wa jimbo wa Mbunge unaweza kulipa deni la taifa ili majimbo yabaki na bajeti kuu ya kawaida.
70 tr lakini bado miradi ya kimkakati inasuasua tu.
 
Ndugai anaanza unafki!??
Ndugai alitakiwa kusema hivi:

Kwa kuwa tozo za miamala na amana zililenga miradi ya shule, maji na afya na tayari Breton woods wametoa ela za Uviko kujengea miradi hiyo ya shule, maji na afya sasa basi tuambiwe tozo zinaenda wapi? Kwa sababu miradi mingine yote tayari ina fadhili za nje na bajeti za ndani. CAG atumulikie tozo zimehawilishwa kwenda wapi? Na je, uhawilishaji (reallocation) umefuata taratibu na sheria?

Isijekuwa tozo zimelenga kinyang'anyiro 2025.
 
IMG-20211228-WA0433.jpg
 
Ukweli mchungu anauzungumza bwana huyu ilaaaa, ninapata mashaka makubwa! Ni moja kati ya waliokuwa wanaupigia chapuo mradi wa Bandari ya Bagamoyo, alivyopelekwa India alitumia Billions of money kumtibia kende zake ila leo anaihurumia nchi kuelemewa na madeni.
 
Back
Top Bottom