Mabeberu walitukopesha huku hela za ndani zilikuwepo ila tuliambiwa miradi inacheleweshwa na Visibility study.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mabeberu walitukopesha huku hela za ndani zilikuwepo ila tuliambiwa miradi inacheleweshwa na Visibility study.
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi hawakuridhia kama inavyosema na baadhi ya wanasiasa.
Kwa maneno hayo naona kuna mambo yanaendelea huko Lumumba yapo mambo hayajakaa sawa ukiona spika anaanza kulalamikalalamika! Alianza kuhusiana na serikali kuhamia Dodoma kuwa kwa sasa kazi zote za serikali na makongamano zimerudishwa Dar-es-Salaam.
Mheshimiwa Ndugai popote ulipo nakwambia hivi wewe na viongozi wako mnaifanyia nini hii nchi mbona mnakaa mnalalamika lalamika wakati chama ni cha kwenu na chama chenu ndicho kimeunda serikali.?
=====
UPDATES;
=====
=> Watu wengi wanatulaumu sana, ninyi ndio Wasomi. Hebu fikiria, Juzi mama kaenda kukopa 1.3 Trilioni deni.
=> Na tuna majengo hivi sasa ya Madarasa, ya Vituo vya afya, ambayo yanajengwa kwa tozo. Hivi ipi bora? Sisi Watanzania wa miaka 60 ya Uhuru tuendelee kukopa na Madeni au tubanane banane hapa tujenge wenyewe bila madeni Makubwa yasiyoeleweka? Ni lini tutajenga wenyewe?
=> Tutembeze bakuri ndo heshima? na tukishakopa tunapiga makofi! Sisi wa kukopa kila siku?
=> Tukasema pitisha Tozo, anayetaka asiyetaka, pitisha Tozo. Lazima tuanze kujenga wenyewe. Nani atatufanyia? Yupo wapi huyo Mjomba? Tukapitisha Tozo.
=> Sasa 2025 itaamua. Mkitoa waliopo sawa. Waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa endepo hiyo ndo namna ya kuendesha Nchi.
=> Hivi sasa deni letu ni 70 Trilioni. Hivi ninyi si Wasomi? Is that healthy? Kuna siku nyi itapigwa mnada hii. Madeni Madeni Madeni
=> Bajeti yetu Trilioni 30, Trilioni 10 kati ya hizo kwa Mwaka tunalipa Madeni.
=> Tumeenda Kukopa 1.3 Trilioni, Tunapiga Makofi. Tunawapa Wazungu Trilioni 10 Mariba Matupu. Wanatufanya Sisi Mazezeta. Hela yako Mwenyewe. Anachukua hela yako, halafu anakupa Kidogo Unashangilia.
=> Toza fanya hivi, tujitegemee, Tusimame wenyewe. Kuna ubaya gani? Hata msomi anatupinga.
View attachment 2060338
Magufuli alipunguza hadi mshahara wake aki-reflect Nyerere Model. Tupunguze mishahara ya wabunge.Labda ameona Bandari ya Bagamoyo imepotezewa wakati aliishakarimiwa kupitia Sino-Africa Blackmail, mimi nafikiri tupunguze matumizi ya Mhimili wa Bunge ili tulipie mikopo hiyo. Mbona Raila alimbana Kibaki hadi wabunge wakapunguziwa maslahi na serikali ikapumua.
Basi tutumie mfuko wa jimbo kulipia deni la taifa. JMT ina majimbo ya uchaguzi 239 X 1,000,000,000/ @ = Tzs. 239,000,000,000/-Ila usiguse mfuko wake.
70 tr lakini bado miradi ya kimkakati inasuasua tu.Basi tutumie mfuko wa jimbo kulipia deni la taifa. JMT ina majimbo ya uchaguzi 239 X 1,000,000,000/ @ = Tzs. 239,000,000,000/-
Mfuko wa jimbo wa Mbunge unaweza kulipa deni la taifa ili majimbo yabaki na bajeti kuu ya kawaida.
Labda mtamuongeza mitano huko kwenyu, huku hata madon wake wesha mchoka.
Ndugai alitakiwa kusema hivi:Ndugai anaanza unafki!??
Eti Nchi kupigwa mnada,bora wakianza kumpiga mnada yeye aliyeruhusu madeni yapite akiwa Spika.
Sasa Jenerali ulimwengu amemuelewa nini alichosema neno Zuzu
Eee Bwana eee... acha maneno hayo... tupe kidogo ya kumalizia siku. Mama amerush mno, kimya wakati fulani ni jibu. Kati ya Job na mama nani anaweza kumuondoa mwenzie?mama kamjibu vikali, ngoja tusubir Ndu atajibu nini
mda utaongea tusubiri ..Eee Bwana eee... acha maneno hayo... tupe kidogo ya kumalizia siku. Mama amerush mno, kimya wakati fulani ni jibu. Kati ya Job na mama nani anaweza kumuondoa mwenzie?
Katika mnada huo, Unguja na Pemba watahusika kuuzwa? Inawezekana maza akauza huko bara akijua huko kwake hapatauzwa.
Inawezekana wanatafsiri kukopa sana kama ni Economic Diplomacy ya Tz imepaa juu zaidi, kwamba kama haiko vizuri unaweza usipate mikopo hata misaada.Yaani bado 30 tr deni letu lifikie 1 quad (1 quadrillion) Baghosha!
SSH kwenye majibu yake anaweza kusema kama kukopa ni dhambi mbona zimekuja Bungeni kutumika kama sehemu ya bajeti yao na Job anaendelea kuzitumia pia?