Job Ndugai: Wabunge watarajiwa wapimwe afya ya akili

Job Ndugai: Wabunge watarajiwa wapimwe afya ya akili

"Ndugai: Kuna wanaotoa maoni wabunge wapimwe afya ya akili

Spika wa zamani wa Bunge, Job Ndugai amesema kumekuwa na maoni wabunge wapimwe afya ya akili kabla ya kwenda kuomba ridhaa ya kuwawakilisha wananchi bungeni akieleza kuwa jambo hilo ni la kuwaachia wananchi ili kuona kama lina umuhimu ama la.
Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu Oktoba 10, 2022 katika hospitali ya Mirembe aliposhiriki maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani.

“Hata kule bungeni wakati fulani panatolewa wito kwamba wabunge wapimwe akili, waende Mirembe kwanza kabla ya kupata Clearence, tunapojaza fomu zile za kuomba ubunge tujaze fomu kisha tuje Mirembe tupimwe na katikati ya muhula tuje tena tupimwe, hili ni pamoja na madiwani na viongozi wengine wakuchaguliwa, sijui kama jambo hilo ni muhimu ama si muhimu lakini kuna wengine wanasisitizaga sana jambo hilo, lakini hilo ni la wananchi tuwaachie wananchi."

“Ni kuonyesha tu kwamba kama mtu ana tatizo aweze kupata tiba, nia sio kumbagua mtu, nia ni kuona kama tatizo lipo ili mtu aweze kupata huduma inayostahili kwasababu madhara ya afya ya akilli ni makubwa sana,” amesema Ndugai.

Ndugai ameeleza dawa za kulevya zimesababisha wagonjwa wengi wa afya ya akili wanaosababisha maovu mbalimbali kwenye jamii, pamoja na wanafunzi kuwa watoro shuleni huku akitoa wito kwa wanafunzi kujiepusha na matumizi ya dawa hizo.

View attachment 2382971
Spika wa zamani wa Bunge, Job Ndugai"

----
Job Ndugai kaamka toka usingizi wa kisiasa.

Akiwa mgeni rasmi sherehe za afya ya akili kitaifa huko Mirembe, ametoa maoni kuwa wabunge wanaowawakilisha wananchi wapimwe afya ya akili.

Katika hili mimi Jidduzz namuunga mkono kabisa.

Awamu ya Tano CCM ilituletea kiongozi mwenye kuhisiwa kuwa na matatizo ya schizophrenia, aina ya ugonjwa wa akili.
Tuliyopitia wote tunayajua.
Hivi ndungai ameshapona kichaa chake alichokuwa anatibiwa mirembe?
 
Mh. Ndugai sio afya ya akili tu bali kuongeza vigezo vya kuwa Mbunge. Tusitumie vigezo wa wakati wa uhuru alivyotumia baba wa Taifa. Tunge waengua wote wanaonunulika kirahisi kwa ajili ya udhaifu wao wa kielimu mfano Kibajaji anawezaje kuusoma na kuuelewa mkataba uliopo Bungeni sasa hivi wa kutaifisha bandari zote za nchi hii?? Kwa kiwango cha Dunia ilipofikia na kwa kiwango cha Elimu cha nchi yetu hakuna kijiji TZ ambacho kitakosa watu wenye Degree moja kwa nini degree isiwe kigezo cha ubunge??
 
Lakini pia wote wale ambao wamekuwa wakiumbuliwa na CAG miaka nenda rudi ni wale wenye madigirii kibao !! Mark my words !
 
Lakini pia wote wale ambao wamekuwa wakiumbuliwa na CAG miaka nenda rudi ni wale wenye madigirii kibao !! Mark my words !
Nakubaliana nawewe ndio maana nimesema utadhani wabunge na viongozi wengine sio wazawa wa nchi hii. Ila kisomo nacho ni tatizo pia kuna vitu vya kawaida kabisa huatarajii mwanafunzi wa darasa la saba aelewe kiufasaha na kuweza kulilinda Taifa lake hapo ndipo nilipo sisitiza tuangalie upya through katiba mpya qualifications za member of parliament. Isiwe tu kusoma na kuandika hii sio sawa. Kwa kipindi kile tunapata uhuru ilikuwa sawa kwani kulikuwa hakuna watu wakutosha wailiosoma nchini
 
Hivi mwanasheria wa serikali kwa sasa ni nani na yeye anaseja kuhusu mkataba huu?? ni ngumu kuelewa.
 
Nakubaliana nawewe ndio maana nimesema utadhani wabunge na viongozi wengine sio wazawa wa nchi hii. Ila kisomo nacho ni tatizo pia kuna vitu vya kawaida kabisa huatarajii mwanafunzi wa darasa la saba aelewe kiufasaha na kuweza kulilinda Taifa lake hapo ndipo nilipo sisitiza tuangalie upya through katiba mpya qualifications za member of parliament. Isiwe tu kusoma na kuandika hii sio sawa. Kwa kipindi kile tunapata uhuru ilikuwa sawa kwani kulikuwa hakuna watu wakutosha wailiosoma nchini
Sahihi kabisa. !!
 
Back
Top Bottom