Joe Biden aondoa vikwazo vya Viza ya bahati nasibu kwa Watanzania

Joe Biden aondoa vikwazo vya Viza ya bahati nasibu kwa Watanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Siku moja baada ya kuapishwa Joe Biden aondoa Visa Ban iliyowekwa kwa Tanzania.

1611321521392.png

1611322158374.png


====
Januari 30, 2020 serikali ya Donald Trump ilitangaza kuwawekea Watanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu hiyo pamoja na raia wa nchi nyingine kadhaa.

Kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi wa utawala uliopita wa Trump, nchi hizo ziliwekewa marufuku hiyo kwa kushindwa kufikia "kiwango stahiki cha ulinzi na kupashana taarifa".
2672892_1611322158374.jpg


"Nchi hizi, kwa sehemu kubwa, zinataka kutoa msaada lakini kwa sababu mbali mbali zimefeli kufikia viwango vya chini tulivyoviweka," aliyekuwa Naibu Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Chad Wolf aliwaambia wanahabari baada ya kutangazwa kwa vikwazo.

Hii leo, Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetangaza kuwa marufuku hiyo imefutwa rasmi na rais mpya wa nchi hiyo Joe Biden aliyeingia madarakani juzi Jumatano.

"Mojawapo kati ya hatua zake za mwanzo kabisa akiwa Rais, Rais Biden ameondoa kikwazo kilichowekwa kwa Watanzania kuomba Viza ya Bahati Nasibu (Diversity VISA - DV)," ubalozi huo umeandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Bahati nasibu hiyo ilipitishwa kisheria nchini Marekani mwaka 1990 na bahati nasibu ya kwanza ikafanyika mwaka 1995. Toka wakati huo, takribani watu 50,000 kila mwaka kutoka nchi mbalimbali duniani hushinda bahati nasibu hiyo na kupata viza ya kuingia Marekani na kufanya kazi kama wakazi wa kudumu.

Washindi wa viza hiyo pia huweza kuhamia nchini humo na wenza wao pamoja na watoto walio chini ya umri wa miaka 21.


Mujibu wa taarifa za Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, katika kipindi cha miaka 10 kutoka 2008 mpaka 2018, jumla ya Watanzania 643 walishinda bahati nasibu hiyo.

Katika kipindi hicho, mwaka ambao Watanzania walishinda wengi zaidi ilikuwa 2009 watu 137 na mwaka ambao walishinda wachache ilikuwa mwaka 2014 watu 28. Zaidi ya Watanzania 10,000 hutuma maombi ya kushiriki bahati nasibu hiyo.

Kwa mwaka 2017 pekee, Watanzania 13,733 walituma maombi, kati yao 6,919 waliingia kwenye kinyang'anyiro na mwishowe walioshinda bahati nasibu walikuwa 46.
 
Ilifahamika hivyo, Kwa kuwa sheria huanza kulindwa na mtunga sheria, sasa mtunga sheria anayepaswa azisimamie haziheshimu hizo Sheria, Iweje Kwa wengine ziwang'ate?

Kwa sasa, Kwa kuwa Marekani imeingiza Uongozi mpya, ni Sawa nchi zinazokiuka matakwa ya haki za binadamu kupigwa Pini

Ilikuwa ni Uonevu Kwa nchi zote zilizopigwa Pini na watu wake kutoingia Marekani, Kwa kuwa uvuniifu wa haki za binadamu ulifanywa pia na huyo mpiga Pini wa nchi za wengine

Hongera Rais Joe Biden Kwa kuliona hilo, tunaanza upyaaa!
 
Hii haihusiani na uchaguzi. Si dhidi ya viongozi, ilikuwa ni dhidi ya Watanzania kuomba green card kwa bahati nasibu.

Watanzania wataweza tena kuomba green card kwa lotto.
Yes, hiyo bahati nasibu ya Green Card iliwekwa Kwasababu ya hisia za ugaidi kutokana na watanzania wengi kujiunga kwenye vikundi vya kigaidi.

Haina mahusiano na uchaguzi wala wavunjaji wa haki za binadamu.
 
Siku moja baada ya kuapishwa Joe Biden aondoa Visa Ban iliyowekwa kwa Tanzania
View attachment 1683401
View attachment 1683412
Ni vema ukafafanua vizuri, maana usiwachanganye watu kuwa ile travel ban ya waliochafua uchaguzi mkuu imefutwa!
 
ni mwendo vice versa mpaka ule ukuta uliojengwa utabomolewa 🤣
 
Hii haihusiani na uchaguzi. Si dhidi ya viongozi, ilikuwa ni dhidi ya Watanzania kuomba green card kwa bahati nasibu.

Watanzania wataweza tena kuomba green card kwa lotto.
Ukimsoma kwa makini aliyeanzisha thread anareflect poor IQ za Watanzania waliowengi.

Imagine taarifa ya ubalozi wa Marekani wametowa taarifa hiyo kwa kiswahili na kingereza na bado jitu bogus hajui kilichoongelewa hapo ni kipi.

Makonda hatakiwi Marekani, na wote walioshiriki kuiba uchaguzi orodha yao ipo kamwe hawatakanyaga Marekani.

Serikali yoyote ya Marekani haicheki na waharibifu wa demokrasia Afrika.
 
Back
Top Bottom