Joe Biden: Kuna tishio la moja kwa moja la nyuklia kutoka Urusi

Hatuna cha kusaidia sisi.Hatua za mwanzo ni yeye Biden na wachokozi wenzake.
Mkuu Ami, nashindwa kabisa kusema Biden mchokozi kwa hili! Inabidi unipe shule hasa! Ukiwa mkorofi kwa lile sio lazima uwe na hili! Nimeona katika mada nyingine Marekani ndio kasababisha Hijab zitupwe Iran!
Anyway tukubalieni tunaangalia mambo kwa lensi tofauti sana! Natamani angalau kwa dakika moja nivae lensi yako !
 
Taarifa nazo huwa Ni ugonjwa punguzeni kuambukizana ikiwa hamna taarifa zenu binafsi
Mkuu Monroe, hatuna taarifa binafsi! Putin kaimbia dunia na wote tumesikia nini anataka kufanya! Na Mzee Biden kajibu, Tembo wapiganapo nyasi huumia, ndio hofu ya wengi!
 
Inabidi kila mmoja aanze kujinunulia jeneza mahali alipo; likiachiwa tu, kila mmoja aingie kwenye sanduku lake, hakuna atakayepona.
Boya ww, nyuklia ikifumuliwa sio Biden wala Putin atakaebaki ila wahuni tutaishi 😂
 
Mimi namwona ni mchokozi kwa ile ari yake ya kujitanua mpaka kwenye uwa wa nyumba ya jirani yako.Kwa lugha nyengine mtu anayetoka mbala akaja akashirikiana na jirani yako akunyang'anye nyumba yako.Na kwa nini huoni uchokozi wa Marekani anapohama kwake akaenda kuchonganisha ndugu wa korea na maeneo mengine duniani mpaka Somalia kafika.Anafuata nini kote huko kama si uchokozi.
 
Bomu limepigwa urusi mie sijapakana nao naathirika vipi?
Bomu la nyukia hapo juu limefafanuliwa hatari yake.Kama hujafahamu ni kuwa lina nguvu sana za kuharibu eneo kubwa kutoka kitovu la liliporipuliwa..Kila linapokuwa na uzito mkubwa na uharibifu unaongezeka. Madhara yake si kama haya mabomu ya kawaida,huwa yanaendelea vizazi na vizazi mbeleni kwa wale watakaobaki hai.Iwapo Ukraine inazalisha ngano nyingi.Basi muda huo hata wakitoa bure itakuwa hazifai kuliwa.
Naamini Putini yuko karibu kuiripua lakini lazima aangalie utabiri wa hali ya hewa ili siku akipiga mvuke usirudi ndani ya Urusi.Iwe ni siku upepo unaelekea Poland na mataifa mengine ya Ulaya.
 
Biden kashachafua chupi nyingi sana toka Putin azungumzie Nuke Biden kila mda mavi yanagonga kyupi yanarudi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu Ami hii nadhani itakuja kuwa ni mada nyingine, maana umeiingiza matukio mengi ya Kihistoria! Kwa mfano tu Korea, huwezi kuuzungumzia mgawanyo huo ukamwacha Soviet Union! Wengi hawana historia hiyo.
Nashindwa kuelewa mfano wako wa jirani kuja kukunyang'anya nyumba yako! Nani kati ya Urusi na Ukraine ananyang'anya cha mwenzie!
Kama nilivyosema hizo ni mada ndefu, sasa hivi tungoje tu kama watazamaji tuone huu mvutano utafika wapi! Sidhani by May Next year hii vita itakuwepo! Aisha Urusi atakuwa kaimeza Ukraine, au Ukraine itakuwa imeisimamisha himaya yake!

By winter Urusi hata Ukraine pia wanajua itakuwa ni game changer! Second World War winter ili play part kubwa mno wote wakiwa ni Soviet Union! Mimi na wewe tuvute subira tu.Vita ikiisha tutarudia mada za uchokozi wa Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…