Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
mashuhuri wa nyimbo za Injili nchini, Joel Lwaga, amewatolea uvivu mashabiki na baadhi ya viongozi wa dini wanaomkosoa kwa kubadilisha mtindo wa muziki wake ikilinganishwa na alivyokuwa akiimba miaka ya nyuma.
Kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Joel Lwaga ameeleza kuwa dunia ya sasa inafuata "trend" na watu wanatafuta vitu vipya, hivyo asipobadilika na kwenda na wakati atajikuta akisahaulika kama ilivyotokea kwa waimbaji wengine wa zamani ambao watu walidai kuwapenda lakini kwa sasa hawawasikilizi wala kuwaalika.
Amewataka wakosoaji hao kuacha ubinafsi na kuacha kumlazimisha abaki na mtindo wa mwaka 2018 au 2019, akisisitiza kuwa hakuna mwanadamu aliyemtuma kufanya kazi hiyo bali aliitwa na Mungu kumtumikia.