Mponjoli
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 668
- 158
HISTORIA FUPI YA JOEL ARTHUR NANAUKA
Joel Arthur Nanauka ametangaza nia ya kuwania ubunge jimbo la Mtwara mjini kupitia CHADEMA. Tarehe 25 June 2015 alirejesha fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake (CHADEMA) kuwawakilisha wanaMtwara. Akiwa kama mtangaza nia ambaye anakubalika miongoni mwa wananchi, ni vyema jamii nzima ya watanzania ikamfahamu, Joel Nanauka ni nani hasa.
Alizaliwa tarehe 4 Julai 1983 mkoani Mtwara na kukulia mkoani humo mpaka alipomaliza elimu ya msingi. Joel Nanauka ni Mmakonde kwa kabila na wazazi wake wanaishi Mtwara. Mama yake mzazi ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Rahaleo iliyopo Mtwara Mjini.
ELIMU YAKE
Joel Arthur Nanauka amesoma shule ya msingi Shangani iliyopo Mtwara Mjini kuanzia mwaka 1992 mpaka mwaka 1998. Dalili njema ilianza kuonekana tangu alipokuwa shule ya msingi baada ya kushika nafasi ya tatu kimkoa katika mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Vipaji Maalumu ya Kibaha iliyopo mkoani Pwani.
Mwaka 2000 aliwashangaza wengi alipofanikiwa kuingia kumi bora ya mtihani wa kidato cha pili kwa kanda ya mashariki inayojumuisha pia Shule nyingine ya vipaji maalumu ya Mzumbe. Pia aliongoza masomo mawili kikanda ikiwemo hesabu.
Alipofika kidato cha nne mwaka 2002 alifanya maajabu yaliyoiletea Mtwara, Shule ya Sekondari Kibaha na Shirika la Elimu Kibaha sifa kubwa sana baada ya kupata alama A katika masomo tisa kati ya kumi aliyofanya katika mtihani wa taifa. Pia alikuwa mwanafunzi bora wa pili kitaifa.
Hii ilimfanya apewe tuzo mbalimbali. Aliingizwa katika kitabu cha mashujaa wa Shirika la Elimu Kibaha. Alitambuliwa rasmi na STANBIC BANK na kupewa tuzo na Wizara ya Elimu kwa udhamini wa kampuni ya COCA COLA. Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ilimtambua Joel Nanauka kwa mafanikio yake katika masomo ya sayansi na kumpa nafasi ya kuzungumza na wataalamu wa ngazi za juu katika mkutano wa kimataifa wa sayansi.
Joel Nanauka alipewa nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi, lakini alitoa msimamo wake kuwa anaamini katika kusoma hapa nchini kwa sababu wanafunzi wengi bora wakienda kusoma nje huwa hawarudi na hivyo taifa linapoteza watu wenye vipaji ambavyo vinaweza kulikwamua na changamoto zilizopo. Joel Nanauka anaamini kuna makusudi ya kipaji fulani kuzaliwa nchi husika.
Mwaka 2003 hadi 2005, Joel Nanauka alirudi tena Shule ya Vipaji Maalumu Kibaha kuendelea na elimu ya juu ya sekondari akichukua masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia. Alipomaliza mwaka 2005, alichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kitivo cha Biashara na Uongozi.
UONGOZI
Dalili njema ya uongozi kwa Joel Nanauka ilianza kuonekana tangu akiwa shule ya msingi Shangani iliyopo Mtwara Mjini. Joel Nanauka alichaguliwa kuwa mmoja wa viranja katika shule hiyo. Akiwa shule ya vipaji maalumu Kibaha, Joel alichaguliwa katika nafasi mbali mbali za uongozi kama uwakilishi wa darasa na kamati mbalimbali bila kujali umri wake mdogo wakati huo. Pia alijihusisha sana na siasa ndani ya CCM kama mwanachama hai akiwa Kibaha Sekondari.
Alipojiunga Chuo Kikuu Dar es Salaam akiwa mwaka wa kwanza tu, alichaguliwa na wanafunzi wenzake zaidi ya mia sita kuwa Mbunge wa kitivo cha Biashara na Uongozi akiwashinda wapinzani wake waliokuwa na umaarufu mkubwa kwa hoja nzito. Alikuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wanafunzi na kudai haki zao.
Joel Nanauka atakumbukwa kwa hoja zake nzito kwenye BUNGE la wanafunzi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lililosababisha Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wakati huo Mhe. Nimrod Mkono kufika Nkrumah Hall kuzungumza na wanafunzi wa Chuo na kuamuru wanafunzi wapatiwe mikopo yao mara moja.
Pia wakati huo, BODI ya mikopo ilisikia kilio cha wanafunzi na kuamua kupandisha posho ya kujikimu (BOOM) kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vyote nchini.
Kutokana na nguvu yake kisiasa na uwezo wake wa kujenga hoja ndani ya siasa za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mara tu baada ya kumaliza elimu ya chuo alikuwa handpicked/alichukuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kupewa nafasi ya Ukatibu Msaidizi wa CCM wa wilaya ya Moshi Vijijini.
Kwa wakati huo alikuwa ndiye kiongozi mdogo kabisa kushika nafasi hiyo kulinganisha na wilaya zote Tanzania. Akiwa Moshi vijijini alileta mabadiliko makubwa baada ya kuhoji ufujaji mkubwa wa fedha za chama hasa ukizingatia alikuwa anashika pia nafasi ya Uhasibu wa Wilaya, akiitumia taaluma aliyosoma Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Baada ya takribani kukaa miezi 8 Moshi vijijini, Joel alitakiwa na chama kurudi Dar es Salaam mara moja ili kusimamia mradi maalumu wa ajira kwa vijana uliokuwa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni wakati huo, Bwana Jordan Rugimbana. Alihusika katika kuanzisha miradi mbalimbali na kushawishi wafadhili kuunga mkono miradi ya vijana wilaya ya Kinondoni. Alishawishi, kupitia Mkuu wa Wilaya, baraza la madiwani wilaya ya Kinondoni kupitisha miradi ya vijana na hadi wakati anaondoka alikuwa amefanikisha vijana zaidi ya elfu tatu (3,000) kupata ajira.
Mwaka 2010 aliingia katika kinyanganyiro cha kugombea UBUNGE jimbo la Mtwara Mjini akiwa ndiye mgombea mdogo kuliko wote. Uwezo wake wa kujenga hoja zenye mvuto na usemakweli wake ulimjengea umaarufu mkubwa na alijijengea ufuasi mkubwa miongoni mwa WanaMtwara.
Wakati kampeni zinaendelea ndani ya CCM, mizengwe ilianza, wagombea wenzake wakimchafua kuwa alikuwa pandikizi la CHADEMA kutokana na kufichua maovu ya watendaji wa serikali wakati wa kampeni. Mikakati ikapangwa kumuandikia taarifa mbaya ya wilaya na kumuibia kura jambo ambalo lilifanikiwa sana. Hata hivyo nguvu yake iliendelea kuwa kubwa miongoni mwa wananchi hata baada ya uchaguzi kuisha.
Joel Nanauka amewahi kuliwakilisha taifa katika kongamano la vijana wa dunia nchini Taiwan na alitajwa kuwa kiongozi bora kijana wa dunia katika kongamano hilo kutokana na mchango wake katika kuchambua changamoto zinazowakabili vijana na utatuzi wake. Pia amewahi kufanya kazi na Umoja wa Mataifa katika miradi ya elimu na demokrasia.
KUONGOZA KWA MFANO KUPITIA KUSAIDIA JAMII
Falsafa ya Joel Nanauka katika kusaidia jamii inajikita zaidi kwenye nia kuliko uwezo wa kifedha. Anaamini kuisaidia jamii si lazima uwe na kipato kikubwa bali uwe na nia na maono ya nini kinatakiwa kufanyika kwa wakati husika.
Joel Nanauka amelithibitisha hili kwani akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam kwa kutumia pesa yake ya kujikimu maarufu kama BOOM, alianzisha asasi ijulikanayo EDUCATION DEVELOPMENT AND POVERTY ALLEVIATION (EDPAE) iliyojishughulisha na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vya vijana na akina mama. Kupitia asasi hiyo aliunganisha vikundi vingi na mashirika na makampuni ya kuwapa misaada.
Pia akiwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kutumia pesa yake ya kujikimu maarufu kama BOOM, alianzisha taasisi nyingine inayoitwa NANAUKA EDUCATION DEVELOPMENT FUND (NEDF) ambayo aliitumia kusaidia kulipia ada wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu.
Wafaidika wa kwanza walikuwa wanafunzi wawili waliotoka shule ya sekondari Sabasaba iliyopo Mtwara Mjini. Katika hili alianzia na pesa yake ya kujikimu Chuo Kikuu (BOOM) kusaidia elimu. Hakuishia hapo, alianza kukusanya rasilimali fedha kutoka kwa marafiki mbalimbali hadi kufikia kuweza kulipia ada wanafunzi 100 kila mwaka. Wanafunzi hawa huchaguliwa kutoka familia zenye mazingira magumu.
Joe Nanauka alianzisha kampuni yake binafsi inayoitwa IQ MANAGEMENT SOLUTIONS ambayo hadi leo inatumika kutoa mafunzo bure kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu ili kuongeza ujuzi wao kupitia program inayoitwa YOUTH MENTORSHIP PROGRAME. Kupitia network yake ameweza kuleta wakufunzi/walimu kutoka ndani ya nchi na kutoka nje ya nchi kama vile Italy, France na Greece.
VUGUVUGU LA GESI MTWARA
Mtwara na Tanzania ilipitia wakati mgumu mwaka 2012 serikali ilipoamua kujenga mtambo wa kuchakata gesi Dar es Salaam kinyume na mpango uliokuwepo hapo awali wa kujenga Mtwara. Nia ya awali ilikuwa kusaidia kuinua uchumi wa eneo la kusini ambalo kiukweli liko nyuma sana.
Kutokana na ukweli kwamba kila kitu kizuri kinawekwa Dar es Salaam, mikoa mingi ambayo inatakiwa kusaidiwa kuinuka kiuchumi kama Kigoma, Lindi, Mtwara, Tabora, Rukwa na Katavi imeendelea kubaki nyuma huku Dar es Salaam ikigawiwa keki ya taifa kuliko uwezo wake wa kuitumia.
Joel Nanauka kwa kuamini kuwa mtambo ulistahili kujengwa Mtwara, kama wanavyoamini wanaMtwara na Watanzania wengi, aliandaa hotuba kuchambua suala zima la uwekezaji huo mkubwa. Hotuba hii ilifikia wakati ikawa ndiyo msimamo wa wanaMtwara.
Shura ya Maimamu na Baraza la Maaskofu walitumia sehemu kubwa hotuba hiyo kama tamko lao rasmi. Hotuba ilitolewa kopi na kugawiwa kwa watu Mtwara Mjini hadi kufikia Masasi na Newala. Hotuba ilikuwa inaombwa na wasikilizaji kwenye vituo vya redio kama wimbo. Kuna watu waliandaa CD za hotuba na kuziuza.
Hapo ndipo uhusiano wake na Chama Cha Mapinduzi uliingia doa na kudorora sana. Alianza kushutumiwa sana, kutishiwa maisha na hata wazazi wake wanaoishi Mtwara walitishiwa maisha. Kuna wakati aligundulika kuwa amepewa sumu, lakini aliwahi kupatiwa matibabu na haikumletea madhara makubwa kwenye ogani zake za ndani.
January 2014, aliamua kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuachana na CCM akiamini CCM haisimamii tena yale yote yaliyofanya kianzishwe mwaka 1977. Alijiunga na CHADEMA akiamini ni chama kinachompigania na kumtetea mnyonge wa Tanzania akiwemo mwananchi wa Mtwara.
KUGOMBEA UBUNGE MTWARA MJINI MWAKA 2015
Tarehe 25 June 2015, alirejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo la Mtwara kupitia CHADEMA. Nguvu yake iliendelea kuthibitika kwani umati mkubwa ulijitokeza kumlaki na kumsindikiza kurudisha fomu. Hivi sasa ni wazi mji mzima unazungumza jina lake.
Redio za Mtwara Mjini zimekuwa zikizungumza sana habari zake na wananchi wamekuwa wakiisii CHADEMA kutopoteza nafasi ya kufanya mabadiliko kupitia kijana huyu. Ukweli ni kwamba kuna wanachama wengi wa CCM waliokuwa wanamuunga mkono wameamua kujiunga na CHADEMA na habari zimeenea kuwa kama CHADEMA watapitisha jina lake, basi mgombea wa CUF atakuwa tayari kuachia ngazi ili kumuunga mkono. Hii ni kwa kutambua nguvu yake, uwezo wake na kukubalika kwake Mtwara Mjini.
Ingawa ndani ya CHADEMA kuna watia nia wane (4) ni wazi kuwa nguvu yake iko dhahiri na ilidhihirika hata jinsi alivyoshangiliwa siku ya mkutano wa hadhara wakati watia nia wote wa CHADEMA walipotambulishwa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Ndugu Salum Mwalimu.
Msemo maarufu kwa sasa Mtwara ni “Mtwara tuna jambo letu, Nanauka ni chaguo letu”, huyo ndiyo Joel Nanauka.