Jogging pembeni ya barabara zinagharimu UHAI

Jogging pembeni ya barabara zinagharimu UHAI

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
Ndugu zangu wafanya mazoezi pembezoni mwa barabara. Chukueni tahadhari hususani wakati wa alfajiri na jioni/usiku.

Nimepoteza rafiki wawili (mmoja Dar mwingine Mtwara) kwa ajali wakiwa mazoezini. Wameacha familia changa mno.

Wakati mzuri wa kufanya mazoezi ya kukimbia huwa ni asubuhi au jioni, na mida hii mara nyingi kunakuwa na magari mengi sana barabarani, mfano, kuna magari unakuta ana taa moja tu, boda pia ni majanga mara nyingi katika kujihami na magari anakuja mpaka pembeni kabisa kwenye chaki,

Kuna magari yana overtake, hapa nadhani wanaokimbia watakuwa wananielewa nini huwa kinatokea, kuna boda nyingine hazina taa zenye mwanga wa kutosha, kuna wanaotembea na full light unaweza kumulikwa ukopoteza muelekeo,

Kuna boda boda zina beba mizigo mikubwa unaweza kuhisi yuko peke yake kumbe mzigo unatokeza pembeni, ni hatari sana kwakweli, kuweni makini.

Pia, Barabara nyingi sehemu za waenda kwa miguu ndio parking hizo hizo, boda boda humohumo

Vile vile Wakimbiaji wengi hawajali usalama wao barabarani wala kuchukua tahadhari. Unakuta mtu anakimbia akiwa amevaa headphones masikio yote mawili na sauti kaweka hadi mwisho, kiasi cha kushindwa kusikia honi za vyombo vya moto

Kama unaweza bora ukimbie kwenye uwanja maalumu kama wa mpira, ulio karibu na makazi yako kwa kuwa ukiachana na ajali
huo moshi unaovutwa na wanamazoezi huku wanapumulia mdomo ni janga lingine

Kama unalazimika kukimbia barabarani, Kimbia in opposite direction na uelekeo wa magari,,kaa upande wa magari yanayokuja mbele yako

NB: Lipia gym uwe salama
 

Attachments

  • images (33).jpeg
    images (33).jpeg
    17.4 KB · Views: 12
Kama unaweza bora ukimbie kwenye uwanja maalumu kama wa mpira, ulio karibu na makazi yako...ukiachana na ajali
huo moshi unaovutwa na wanamazoezi huku wanapumulia mdomo ni janga lingine
 
Umesema kweli kabisa. Dar maeneo mengi pembeni mwa barabara sio rafiki kwa jogging. Mimi muda wa jioni huwa nafanya mazoezi ya kutembea pembezoni mwa barabara na mara nyingi nimenusurika kugongwa. Barabara nyingi sehemu za waenda kwa miguu ndio packing hizo hizo, boda boda humohumo, hivyo kufanya jogging barabara za dar ni kuisogelea njia panda ya kuzimu
 
Wanao kimbia barabarani wanafanya Show-Off wanajifanya wazungu Earphones masikioni na mbwembwe nyingine nyingi tu... Unatoka nyumban unaacha jirani yako kuna uwanja wa mpira kwanin usifanyie mazoez hapo..? Ila unataka ukakimbie barabarani dakika 10 urudi home...
😎 ILA UKWELI NI KWAMBA UKIONA MWANAUME ANAKIMBIA KIMBIA JIONI UJUE NGUVU ZIMEPUNGUA ANAJIBUSTI NGUVU ZIRUDI😂
 
Back
Top Bottom