Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asaante kwa Uzi Juma1967 naomba kuchangia uzi kwa sababu mimi ni mdau mkubwa wa mazoezi hasa ya Jogging; Katika kufanya mazoezi hasa ya kufanya jogging ni vema sana kuchukua tahadhari kama ifuatavyo;Ndugu zangu wafanya mazoezi pembezoni mwa barabara. Chukueni tahadhari hususani wakati wa alfajiri na jioni/usiku.
Nimepoteza rafiki wawili (mmoja Dar mwingine Mtwara) kwa ajali wakiwa mazoezini. Wameacha familia changa mno.
RIP
NB: Lipia gym uwe salama
Leo wakati natoka kwenye kibarua changu asubuhi nikiwa na rafiki yangu kituo cha vetenary nyuma kulikuwa na kundi la wanajeshi wamevaa nguo za kimichezo truck suit wakikimbia jogging nais ni wa jkt mgulani walitoka upande wa Tazara wakielekea sokota mim na mwenzangu tukavuka upande kutoka kulia kuelekea kushoto yaani kituoni kabisa na kusimama yule mwanajeshi kijana alikuwa kashika bendera nyekundu akiongoza kile kikundi alisimama ghafla na kutuambia rudi mara moja upande tuliotoka akituonesha kwa bendera "rudi haraka kabla sijakasirika atukubisha tukatoka upande wa kituoni na kurudi upande mwingine maana pembeni nliona kulikuwa na madimbwi ya maji lile kundi likapita baadae nikamuhuliza yule jamaa nliyekuwa nae kosa letu nin akasema akuna kosa uo ni ubabe wa kijeshi na tungebisha wangetutia aibu mbele ya abilia waliokuwa wamekaa kituoniNdugu zangu wafanya mazoezi pembezoni mwa barabara. Chukueni tahadhari hususani wakati wa alfajiri na jioni/usiku.
Nimepoteza rafiki wawili (mmoja Dar mwingine Mtwara) kwa ajali wakiwa mazoezini. Wameacha familia changa mno.
RIP
NB: Lipia gym uwe salama
napigaga hiyo route Alhamis nikitokea Job maeneo ya Sokoine Drive, katika route ambazo ni nzuri kukimbia hiyo ya Toure ni moja wapo! anyway mjuba uje basi Jerusalem Children's marathon Kigamboni 23/07 baada ya hapo tukutane NBC tarehe 31/07 pale Dom.Binafsi huwa nakimbia Toure drive,Tanzanite bridge,Obama drive na mitaa ya ndani ndani Oysterbay na Masaki.
ni wazo zuri sana lakini kwa wakimbiaji ambao wamefanya mazoezi kama sehemu yao ya maisha ni ngumu kidogo maana, kuzunguka uwanja ukamilishe 10Kms aisee sio jambo dogo na ina bore sana imagine kila siku ufanye hivyo hadi ukamilishe target ya 200Km ya mwezi!!Kama unaweza bora ukimbie kwenye uwanja maalumu kama wa mpira, ulio karibu na makazi yako...ukiachana na ajali
huo moshi unaovutwa na wanamazoezi huku wanapumulia mdomo ni janga lingine
Ndani ya mwezi mmoja nimesikia matukio mawili moja limepelekea kupoteza maisha Kigamboni. Mmoja bodaboda imebeba geti ikamzoa, mwingine juzi nimesikia kagongwa na gari Ungindoni sijui anaendeleaje.napigaga hiyo route Alhamis nikitokea Job maeneo ya Sokoine Drive, katika route ambazo ni nzuri kukimbia hiyo ya Toure ni moja wapo! anyway mjuba uje basi Jerusalem Children's marathon Kigamboni 23/07 baada ya hapo tukutane NBC tarehe 31/07 pale Dom.
#RUNFORbetterHEALTH #runyourpace
Yeah Tarehe 6/7 tulimpoteza mwenzetu mmoja hata hivyo yeye hakugongwa akiwa barabarani alikuwa amepakiwa kwenye Boda ambayo iligongwa na Mlevi mmoja akitoka misele yake town (Rest easy Dastan)Ndani ya mwezi mmoja nimesikia matukio mawili moja limepelekea kupoteza maisha Kigamboni. Mmoja bodaboda imebeba geti ikamzoa, mwingine juzi nimesikia kagongwa na gari Ungindoni sijui anaendeleaje.
yeah Kibada, case hizi zipo sana last 2 years tulimpoteza runner mwingine Tabata aligongwa na Gari akadumbukia kwa mtaro na kupoteza maisha (Rest in peace Yahaya Kipande)Hii ilikua kigamboni eeh?
Mazoezi ni afya mkuu. Si unaona mzee Mwinyi alivyofiti.Wanao kimbia barabarani wanafanya Show-Off wanajifanya wazungu Earphones masikioni na mbwembwe nyingine nyingi tu... Unatoka nyumban unaacha jirani yako kuna uwanja wa mpira kwanin usifanyie mazoez hapo..? Ila unataka ukakimbie barabarani dakika 10 urudi home...
😎 ILA UKWELI NI KWAMBA UKIONA MWANAUME ANAKIMBIA KIMBIA JIONI UJUE NGUVU ZIMEPUNGUA ANAJIBUSTI NGUVU ZIRUDI😂
unaongelea ile ya kigamboni jamaa kaacha mke hata hawajazaa ndoa ya mwaka mmoja. mimi mwenyewe mtu wa jogging ila nako kaa hakuna migari mingi so mara nyingi nafanyia mazoezi uwanjani na mara chache sana barabara ya vumbi isiyokuwa na gari.Huwajui bodaboda wewe. Kuna mmoja alipakia Geti kuzidi boda. Akamzoa mfanya mazoezi akamtupa mferejini
Umehamia lini Oysterbay wakati tulikuwa tunaishi wote Buza.Mimi ni mkimbiaji sana sana jioni nashauri haya
1. Kimbia barabara zenye sehemu maalum ya watembea kwa miguu
2.Kimbia upande wa kulia wa barabara
3.Usikimbie wakati wa giza
4.Ukivaa headphone weka sauti ambayo ukiongea na mtu mnasikilizana au unasikia magari,honi etc
5.Ukiweza, epuka main roads, kimbia kwenye mitaa isiokuwa na magari mengi.
Binafsi huwa nakimbia Toure drive,Tanzanite bridge,Obama drive na mitaa ya ndani ndani Oysterbay na Masaki.
Mimi mlinzi huku nikitoka lindoni ndio naanza mchakamchaka hadi Buza.Umehamia lini Oysterbay wakati tulikuwa tunaishi wote Buza.
Jambo hili kiusalama ni muhimu sana lakini wengi hawalijui. Wakimbiaji na watembea kwa miguu wanapaswa kuwa upande wa kulia wa barabara, ili wayaone magari yaliyo karibu nao. Kutembea au kukimbia ukiwa kushoto ni hatari sana, kwani magari yatokayo nyuma yako mko nayo pamoja upende huo.Kimbia in opposite direction na uelekeo wa magari,,kaa upande wa magari yanayokuja mbele yako
du hivi kutembea nako ni mazoezi,mimi huwa natoka kkoo mpaka gmboto kwa mguu,kukiwa na foleni kubwa ya daladala.Umesema kweli kabisa. Dar maeneo mengi pembeni mwa barabara sio rafiki kwa jogging. Mimi muda wa jioni huwa nafanya mazoezi ya kutembea pembezoni mwa barabara na mara nyingi nimenusurika kugongwa. Barabara nyingi sehemu za waenda kwa miguu ndio packing hizo hizo, boda boda humohumo, hivyo kufanya jogging barabara za dar ni kuisogelea njia panda ya kuzimu