Jogoo hasimami asubuhi

Muone tabibu kwa msaada Kabla mambo hayajawa sivyo ndivyo
 

Thumb up.....
 
iyo kitu huwaga inanitokea pia aisee coz nina mlundikano wa mawazo milioni na kipind cha nyuma nilikua mpiga puli
 
Umri na stress za maisha tu,kama ni kula kulala sawa
 
Unataka asimame asubuhi ili nini?kafanye kazi acha kuwaza mapenzi asubuhi yote hii
 
Unataka asimame asubuhi ili nini?kafanye kazi acha kuwaza mapenzi asubuhi yote hii
Kisayansi kusimama kwa uume wakati wa usiku hutokea bila kujijua "unconsciously" hii inaitwa nocturnal penile tumescence (NPT) na hutokea katika REM phase (Rapid eye movement) ya usingizi, kwa mwanaume wa kawaida asiye na matatizo inapaswa kutokea mara 3-5 kwa usiku mmoja, kama haitokei hivyo basi una matatizo flani either physical au psychological,

hii kitu ni muhimu kwa sababu tissue za uume zinahitaji oxygen na virutubisho ili ziweze kuwa na afya na kuufanya uume wako uwe na nguvu ,sasa uume unaposimama kwa kujaa damu wakati wa usiku unapokua umelala na hakuna usumbufu wowote tissue zinapata wakati mzuri wa kufyonza virutubisho kutoka kwenye damu na uume utakua na afya, kusipotokea hicho kitu tissue za uume wako hazitapata virutubisho vya kutosha hivyo kusababisha uume kusinyaa.

Kwa hiyo tukio hili ni muhimu tusilichukulie poa, kama hupigi puli basi punguza stress mambo yaende vizuri, au kachek magonjwa yanayopunguza mzunguko wa damu kama presha na kisukari, pia fanya mazoezi ya viungo kusaidia mzunguko wa damu.

CONCLUSION: Uume kusimama wakati wa usiku au asubuhi ni muhimu kwa afya ya uume wako.
 
Sasa asubuhi asubuhi hivi,unaleta jf,si ujifanyie utafiti wako kimya kimya
 
Sasa asubuhi asubuhi hivi,unaleta jf,si ujifanyie utafiti wako kimya kimya
Mimi sioni tatizo sababu kitu kiketokea asubuhi akaona aombe ushauri, hakuna muda maalum wa kupost vitu JF, ila kama inakukera pia unaweza kupita kimyakimya bila kuchangia , povu veepe jombaa
 
Kunywa maji mengi kabla ya kulala, yanaleta usumbufu wa kuamka kwenda msalani lakini yanasaidia body hydration. Mwili ukipungukiwa na maji hata BP inashuka. Kingine ni kujijengea utaratibu wa kufanya mazoezi.
Dr ntakutafuta
 
Mimi sioni tatizo sababu kitu kiketokea asubuhi akaona aombe ushauri, hakuna muda maalum wa kupost vitu JF, ila kama inakukera pia unaweza kupita kimyakimya bila kuchangia , povu veepe jombaa
Watu kama hao ni kuwapotezea tu mkuu lasivyo watakuumiza kichwa tu
 
Kama ukikutana na mwanamke, unamridhisha, achana na swala la jogoo asubuhi. watu typo tofauti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…