Joh Makini, The Tanzania hip hop giant anayepita njia inayomfanya aonekane wa kawaida sana

Joh Makini, The Tanzania hip hop giant anayepita njia inayomfanya aonekane wa kawaida sana

ushauri wa maana sema mwamba analegeza sanaa saiv sio kama kipindi bum kubah
Miaka ya 2008 mpaka 2012 ukisikia jina JOH MAKINI unapata picha ya nguli wa Hip hop ambaye alipendwa na wagumu pamoja na mademu at the same time. Joh makini ni msanii wa hip hop ambaye ana vitu vifuatavyo;
Flow za aina nyingi halafu zinabamba
Ana sauti nzuri
Anaweza kurap ktk mdundo wowote
Ni mwandishi mzuri
Ana fanbase kubwa
Ana muonekano wa kisanii

Kila nikisikiliza Stimu zimelipiwa, Hao, Muda, Mfalme, kilimanjaro, brand(blue magic), popote, simwachii Mungu na nyingine kadhaa wa kadhaa naona huyu jamaa anajua sana na ana vitu vingi sana ila anafanya kosa moja

KOSA
Joh makini unapokaa kwenye kundi la weusi unamezwa. Anayenufaika na kundi la weusi ni Nikki wa pili ambaye hana mashabiki wake hvyo kundi linambeba na anatumia fursa vilivyo. Pia Gnako ananufaika na kundi kwa sababu huyu jamaa yeye aliumbwa na Mungu kwa ajili ya kolabo tu na akiimba mwenyewe ngoma zinabuma.

USHAURI
1.Baki katika kundi la weusi ila jikite kutoa ngoma zako mwenyewe na hizo za colabo ziwe chache sana.
2. Piga kotekote kama Fid Q anavyofanya siku hizi, yaani mashabiki zako wa zamani wape ngoma kama Stimu zimelipiwa na wa siku hizi wape nyimbo kama ‘mipaka’
3. Acha kujitenga sana na wasanii ambao sio weusi. Piga kolabo na akina kala jeremiah, mwana FA, Ali kiba, Jay moe, Lady Jay dee, n.k
4. Una package kama ya JAY Z ila ukimdate vanessa au mkatengeneza project na Vanessa mkawa kama mpo wote, mnatoa ngoma, shows na vitu vingine mtakuwa THE CATERS wa bongo.

Ni hayo tu MWAMBA WA KASKAZINI
 
Joh Makini alibadilika baada ya kutoa lile jisongi la HAO ile ilikua HiP Hop mpaka Rose Mhando alirudisha Tuzo ya Kilimanjaro, baadae kuanzia hio 2008 akaanza kuiga iga miziki ya kiulaya ulaya kuiga flow za Jay Z, ila katika ushauri mzuri ulioutoa ni ule wa kutoa ngoma kwa mashabiki wote wa Hip Hop na hawa wa kisasa ila mkuu umeua sana ulivyosema akimdate Vanessa Mdee hahaha hapo mkuu umetisha ila ni kweli watapendeza sana demu mfupi na jamaa mrefu inakuaga collabo nzuri sana...
 
Ume exaggerate uwezo wa huyu jamaaa.

Kuhusu Gnako umesem kweli, jamaa katik kolabo mtamu sana.

Sijawahi muelewaga Nikki wa pili. Anajikuta anajua sana bt actually kawaida kinoma, jina kubwa kuliko uwezo
 
Hana mke
Hana mtoto
Rapa inatakiwa ujishughulishe uache alama kama sio muziki basi familia..

John ni msanii mzuri sana alipotezwa kwenye game baada ya skendo ya ushoga
Hana mtoto una uhakika???? Wabongo bhana yaan wanataka uishi watakavyo
 
Hana mke
Hana mtoto
Rapa inatakiwa ujishughulishe uache alama kama sio muziki basi familia..

John ni msanii mzuri sana alipotezwa kwenye game baada ya skendo ya ushoga
Anae mtoto, ila hamweki katika media...
Fatilia vizuri mkuu, refer hata interview moja alifanya na Salama akajibu hilo swali
 
nina miaka sasa mitatu. sina nyimbo mpya hizi za joh makini. sizielewi kabisa.

nyimbo yake ya mwisho ninayo ikubali ni "najiona mimi"
 
Tatizo hip hop haiuzi

Wanaotamba saiz wabana pua na waimba singeli (dabliyusibi)
 
Siku zinavyozidi kwenda, naona Kama anazidi kupotea.
 
Back
Top Bottom