Joh Makini: Weusi tumeacha ushamba

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Rapa kutoka Weusi Kampuni, Joh Makini amefunguka kuwa kampuni yao kwa sasa haina ushamba tena kwenye muziki kwa kuamini kuwa video ndiyo inaweza kukuza muziki wao na kuwapeleka sehemu kubwa zaidi.

Akizungumza na eNewz Joh Makini, amesema kuwa anacho amini kwenye muziki ni ladha ya muziki mzuri 'audio' ndiyo inaweza kuuza muziki huo japokuwa ni vizuri muziki ukiwa na video.

“Mimi naamini kitu cha kwanza kwenye muziki ni audio, Ndiyo maana unaona watu zamani tulikuwa tunapiga audio strong na ilikuwa inauza..., Watanzania wameshaacha ushamba wa picha ndio maana hata ukitoa video kali kama audio sio nzuri ngoma inakufa” Amesema Joh Makini.

Katika hatua nyingine Joh Makini amefunguka kuhusu suala la mashabiki kutumiana nyimbo kupitia mitandao na kwamba watumie njia sahihi ili kusapoti kazi za wasanii wanaowakubali.

“Watu waache kutumiana audio kwenye Whats App au makundi halafu kwenye interview unakuta mtu anaulizwa album lini, kama umeshindwa kununua ngoma moja mtandaoni utawezaje kununua album?” Joh Makin alisema kwa mtindo wa kuhoji.

Chanzo: EATV
 
Track kuuza video inanafasi kubwa saana mazee. Wasipuuzie itawacost joo.
 
Wasanii wote Wa bongo mbona bado washamba na ndio maana maisha yao yanajulikana zaidi kuliko kazi zao.
 
Bujibuji kama watu wa Arusha ni washamba, wewe wa porini umelifanyia nini Taifa?
 
hata nyimbo mnazo imba siku hizi mkiwemo nyie weusi hazini vutii kuzinunua weusi nao wanaimba garbage,album ya fid q,christian belaa,ally kiba naweza kununua ni kati ya ubunifu unao ishi
 
Kutoa video kali ni ushamba? Sawa.
 
Nyie bado ni washamba huwezi ukataa ushamba kwa kujisema mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…