John Bocco aandaliwe kama golikipa wa akiba

Hoja mzuri ila umemvunjia heshima Bocco
 
Ungesema tu kuna haja ya Simba ya kuwa na golikipa ingetosha sana na ningekuelewa/ tungekuelewa ila kumhusisha Bocco hapo umemvunjia heshima.. Maneno haya yangeandikwa na Utopolo ningeelewa ila wewe mshabiki/mpenzi/ mwanachama kindakindaki hapa Jf na hata huko mtaani...Nimeshangaa..labda Bocco mtani wako.
Kwa nini unadhani hivyo?
 
Dah sikuwa na nia hiyo kabisa. Ni nia njema kabisa. Mbona nafasi ya golikipa ni nafasi muhimu sana katika timu, inakuwaje inakuwa dharau? Ngoja nikuulize, kuna mpango gani wa kuwakuza kina Salim na Ferooz kama replacement ya baadae ya Manula au wataendelea kuwa makipa wa akiba maisha yao yote?

Kwa mtazamo wangu unapokuwa mchezaji unayeheshimika katika timu, utafanya kila uwezalo ili kuhakikisha timu inabaki imara. Ndiyo maana nikatoa mfano mimi nilipokuwa nacheza, nilikuwa naangalia sehemu gani katika timu ina mapungufu siku hiyo naenda kuicheza ile nafasi na naicover vizuri tu. Bocco siku hizi akiingizwa anaonekana kupambana sana kwa ajili ya timu ingawa mwili ndiyo hivyo unakataa, ndiyo maana nikatoa ushauri huo ajifue na afuliwe ili likitokea la kutokea, tusijikute Salim kama option pekee tuliyonayo. Kuna kitu kinaniambia ukiacha labda mwili wake kuwa umechoka, Bocco anaweza kuicover hiyo nafasi kuliko wengi tunavyodhani.

Vilevile kule mbele kumejaa, yaani miamba yote ile ituangishe?
 
Bado muda upo kwa wazo langu kufikiriwa. Mambo mengine yanahitaji tu kujiamini baasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…