John Boko asaini mikataba miwili kwa timu tofauti ni Simba SC na Polokwane FC

John Boko asaini mikataba miwili kwa timu tofauti ni Simba SC na Polokwane FC

Peramiho yetu

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2018
Posts
5,303
Reaction score
14,983
Habari wanajukwaa

Katika Hali ya kushangaza mchezaji mahiri wa Simba na timu yako Taifa Tanzania John Boko amesaini timu mbili tofauti , Polokwane FC ya Afrika Kusini na timu ya Simba ya Tanzania

Ikumbukwe mkataba wa Simba umeisha mwaka huu baada ya msimu wa ligi kuisha. Kwa mujibu wa msemaji wa Polokwane amesema mkataba wa Boko umeshapelekwa kwa mamlaka za soka Afrika Kusini PSL kuthibitisha kama mchezaji wao

Akiongea na msemaji huo wa Polokwane, mtangazaji wa E FM Sound Mkumba amethibitisha kuwa Boko ni mchezaji wa Polokwane kwa mkataba wa miaka 2

Hata hivyo pia kituo hicho kilimtafuta mwenyekiti wa Simba, Suedi Mkwabi kutoa mkanganyiko huo naye alisema anachojua Boko ni mchezaji wao halali.
 
Potelea mbali, hili lihuni lazima lifungiwe! Kwanza hata hiyo miaka 5 niliyopendekeza ni michache sana, tena sana!
Bocco ana uhuni gani?
Huyu ni moja ya wachezaji wastaarabu katika wachezaji wote Tanzania naweza kuthubutu kusema hivyo.

Fatilia mechi za Azam alipokuwako akiwa kama kiongozi uwanjani au za Simba anapokuwa anacheza kama timu inafanya mambo ya kijinga Bocco ni the best player mwenye nidhamu Bongo hana uhuni yule.
Wahuni ni kina Mkude hawa wako wengi wanakipiga sana uwanjani na uhuni ni nature yao
 
Bocco ana uhuni gani?
Huyu ni moja ya wachezaji wastaarabu katika wachezaji wote Tanzania naweza kuthubutu kusema hivyo.
Hata kusajiri timu mbili kwenye msimu mmoja nao ni uhuni sawa tu na ule wa akina Nyosso, tena heri ya ule wa akina Nyosso lakini huu wa akina Boko ni wizi!! Kwahiyo bado nasisitiza, huyu mhuni lazima afungiwe angalau misimu 5!!! Haya mambo tuliyazoea zamani, akina Idelfonce Amlima wanasajiri huku na huku, kote wanalamba mpunga, kisha wanaenda kujificha Msumbiji!!
 
Bocco kushoto akisaini Polokwane FC ya South Africa na mkataba ukionekana siku chache baadae picha ya kulia akisaini Simba mbele ya Mo dewji
Inst-image-20.jpeg
 
Hata kusajiri timu mbili kwenye msimu mmoja nao ni uhuni sawa tu na ule wa akina Nyosso, tena heri ya ule wa akina Nyosso lakini huu wa akina Boko ni wizi!! Kwahiyo bado nasisitiza, huyu mhuni lazima afungiwe angalau misimu 5!!! Haya mambo tuliyazoea zamani, akina Idelfonce Amlima wanasajiri huku na huku, kote wanalamba mpunga, kisha wanaenda kujificha Msumbiji!!
Una ushahidi kuwa kasaini katika timu zote mbili?
 
Bosi na CEO wa Simba Magoli anasema Ni kweli Bocco alisaini Polokwane city na wanajua walichofanya Ni kuongea na Polokwane city iwe Kama wanamnunua Bocco lakini Mazungumzo yamekuwa magumu hawajakubaliana lakini wanaamini litaisha
 
Back
Top Bottom