Labda tunaweza kusema zipo sababu kuu mbili.
Mosi ,General Kiwelu alitoka kanda ya Kaskazini Mkoa wa Kilimanjaro.Ikumbukwe wakati wa utawala wa Mwl maafisa wa jeshi waliotokea Kanda ya Kaskazini waliondolewa jeshini kwa tuhuma za kutaka kupindua serekali.General Sarakikya Mirisho alikuwa Mkuu wa majeshi wakati huo alipelekwa Nigeria kama Balozi,Capt Mushi alipelekwa Arusha kama General Manager Fiberboard Arusha,Col Metili sikumbuki vizuri kama alikwenda Mkonge au KAMATA shirika la mabas ya taifa na wengine wengi waliondolewa jeshini.
Wakati wa vita ya Kagera (Uganda na Tanzania) General Kiwelu aliandaa mipango ya kivita kabla ya kurejeshwa makao makuu.Wakati wa kipindi chote cha maandalizi aligoma kumpatia taarifa Waziri Mkuu wakati huo Edward Moringe Sokeine lini majeshi yetu yangevuka mpaka kuelekea Uganda (Mto Kagera).Kwa mujibu wa nukuu yake mwenyewe Sokoine alishangaa na kuuliza hata mimi (Waziri Mkuu) nafichwa taarifa za kivita.Nadhani watawala waliofuta walitishwa na ujasiri wa General Kiwelu iwapo angepewa ukuu wa majeshi labda ingekuwa vigumu kumdhibiti/kumpeleka peleka.