Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Wakati naendelea kufuatilia marudio ya msiba wa Garder, namuona DJ JD akiwa katulia msibani. Mara kwa mara kamera zinamuonyesha akiwa katulia, na miwani yake myeusi juu ya paa la uso.
Ndipo ninapovuta kumbukumbu miaka ya 2005 kama sikosei, akiwa East Africa Radio. Kipindi chake cha usiku kilibamba sana. Kilikuwa na engagement ya kutosha. Alikuwa influential redioni. Kabla ya hapo nadhani alikuwa Radio One. Baada ya hapo sikumbuki sana ila mara nyingi nilimsikia kwenye udj, hasa wa zile nyimbo zetu pendwa za old school. Kitambo nikimsikia Las Vegas Casino ambapo baadae ikaitwa Isumba Lounge.
Kifupi huyu jamaa kwa kumtazama ni mbadala sahihi wa marehemu. Ni mtangazaji mahiri na mtulivu awapo kwenye mic. Ni mkongwe, jamii ya marehemu. Atafaa sana kuliongoza jahazi akisaidiwa na wabakiaji Mussa na George.