Tetesi: John Heche adaiwa kukiuka kanuni za uchaguzi CHADEMA, hatarini kuenguliwa

Niliona hilo kosa, lakini naomba asamehewe, Japo kama akishinda yeye na labda akashinda mgombea mwingine na si Lissu anatakiwa kujiuzulu siku hiyo hiyo, maana alishatangaza kutoshirikiana na yeyote mwingine
Nilijua na wewe angalau zimo kidogo kumbe na wewe ndio walewale wakina Yericko na Ntobi.
 
Asamehewe na nani? Kwa kosa gani
Unaifahamu katiba ya Chadema? Hivi vyama siyo vijiwe vinazo taratibu zake, tunataka kila anayetaka agombee, lakini kwa kufuata katiba ya Chama.

Sina ugomvi wowote na Heche, hata yeye anajua lakini hakuna mgombea mwenza kwenye uongozi wa Chadema
 
Nilijua na wewe angalau zimo kidogo kumbe na wewe ndio walewale wakina Yericko na Ntobi.
Mkuu hao wote unaowasema wanavunja katiba ya Chadema, ni wapi umeona mimi nimevunja?

Kuna maisha baada ya Uchaguzi
 
Ndio kusema hatuoni wenje akimuunga mkono sultan, anamtukana lisu, anamdhihaki na anaonesha kabisa upande wake.

Tulieni dawa iingie safari hii mbowe hachomoki
 
Naona somo la engua engua mlilofundishwa na sponsor wenu CCM limekolea sasa mnataka kulifanyia kazi kwa vitendo.
 
Unahangaiaka sana ila Lissu atashinda
 
Tunahitaji Mabadiliko kwa kweli!
 
Yeyote anayepambana kupingana na mpango wa Mungu , anayajua madhara yake ? Anajua Mungu anaweza kumfanya nini mtu anayepingana na mpango wa Mungu?
 
Mkifanya hilo kosa la kumkata ndio mtaharibu kila kitu bora muibe kura kuliko kumkata. Tunarudia makosa yale yale ya CCM alafu tukifanyiwa sisi tulalamike
 
Mnatapatapa, jambo la muhimu Mbowe kachokwa na kila mwanachadema mwenye akili isipokuwa wachumia tumbo na machawa kama wewe tu
Naona mmeamua kuja na zile ID zenu zote,

Ama kweli mabavicha safari hii mmnalo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…