- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Madai
Kumekuwepo na kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni kikimuonesha Jonh Heche akifanyiwa mahojiano na Mwandishi wa Jambo TV ambapo anasikika akisema 'CCM ya Rais Samia ndiyo yenye unafuu zaidi'
Je, ni upi uhalisia wa kipande hicho?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search, utafutaji wa maneno muhimu (key words search) pamoja na marejeo ya video umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwa kukata na kuunganisha vipande vya video visivyohusiana na kutengeneza ujumbe usiokamilika hatimaye kupotosha uhalisia.
Ufuatiliaji umebaini kuwa kipande hicho kimekatwa kutoka kwenye mahojiano yaliyorushwa mbashara na Jambo TV kupitia mtandao wa YouTube ambapo Heche alikuwa akifanyiwa mahojiano Julai 31, 2025.
Heche aliulizwa tathmini yake ya uongozi wa utawala uliopita na utawala wa sasa unafuu ni upi kwao kama chama cha upinzani?
Akijibu swali hili alisema "CCM haijawahi kutupa unafuu, haitaki demokrasia, CCM ilileta demokrasia ya maigizo tangu mwaka 1992 tume ya kwanza kabisa iliyoundwa na Rais wakati wa vyama vingi, Tume ya jaji Nyalali na Kisanga ilipendekeza kubadilisha katiba sheria za nchi, sheria za uchaguzi ili CCM kisiwe chama dola, vyote viwe vyama vya siasa tushindane kwa haki, wamegoma kutoka mwaka 1992 mpaka leo"
View: https://www.youtube.com/live/IWpgJOtGPWQ?si=bB_lwa0u2VgJ0t_S&t=2109