John Heche amjibu Gerson Msigwa: Msemaji wa Serikali au Serikali inawezaje kuita watu Nguchiro

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Anaandika John Heche kwenye ukurasa wake wa X:

Kama kuna mtu alikua hajui kwanini serikali hii haiwajali Watanzania, Kama kuna mtu alikua hajui kwanini watu wanatekwa, wanauwawa, kama kuna mtu alikua hajui kwanini watu hawana maji, hawana barabara, hawana shule bora, kama kuna mtu alikua hajui kwanini kodi za umma zinaibiwa na watu wakisema hawasikilizwi..

Kama kuna mtu alikua hajui kwanini watu wanaweza kuuwawa kama kuku, watu wakadhulumiwa haki zao na bado watu walioko kwenye madaraka wasijali.

Soma pia: Msemaji Mkuu Wa Serikali Gerson Msigwa awaita walipa kodi 'Nguchiro'. Ni kiburi cha aina gani hiki?

Kama kuna mtu huyo ambae alikua hajui namna Serikali hii inavyowaona na Kuwafikiria Watanzania aje asome hii kauli ya msemaji wa serikali na kwa maana hiyo kauli ya serikali.

Tanzania ni Jamhuri, maana ya Jamhuri umma au Wananchi ndio wenye mamlaka, ndio wenye nguvu… ndio maana Katiba yetu ibara ya 8 inasema mamlaka yatatoka kwa wananchi no matter how wananchi wanaweza kumuudhi Kiongozi wa umma huwezi kuwaita “Nguchiro “ tumeona kwenye Nchi nyingi tu viongozi wanakosolewa tena hata vibaya, na sheria zipo kama kuna kosa kuna hatua za kuchukua…

Msemaji wa serikali au serikali inawezaje kuita watu Nguchiro!!!!

Kumbe ndio maana mnawadharau Watanzania, mnaiba kodi zao huku wao wakiteseka, mnaua na kuteka, mnauza rasilimali za Nchi .. kwasababu hamuoni utu wao mnaona Nguchiro, hamuoni thamani yao mnaona Nguchiro!!!

Nafikiri Hii ni statement ya serikali kupitia msemaji wake na katibu wa wizara..

Watanzania msikubali dharau hizi kwenu na watoto wenu, ndio maana wakitafuta kazi hawapati kwasababu hawa wanawaona nyie sio binadamu, kwamba wao ni binadamu kuliko nyie!!!

Hakuna kiwango cha hasira au matusi kinachoweza kujustify serikali kuita raia wake Nguchiro hata kama ni mmoja

heche.png
 
Huyu Msemaji kachemka kwa neno hilo.
Ukiwa Msemaji wa taasisi kubwa, lazima uwe na kifua, uwe fundi sana wa kutumia maneno yako kujihami. Kwa hali ilivyo sasa ya kisiasa huyu jamaa awe makini na kazi yake hiyo.
 
Asamehewe tu hajui asemalo na zaidi sana aombewe tu kwani kule kwao Mpitimbi Mfaranyaki na Magagula huitana majina ya ndege na wanyama.... Utasikia huyu ni Nyoni mara Mbega Mbawala n.k. 🤔
 
Heche sidhani kama hiyo nafasi inamtosha.

Sasa Msigwa ni kiongozi kweli?

Yule ni msemaji wa Serikali sio kiongozi.
 
Heche ni mpumbavu sana. Kuna sheria gani inaruhusu namba ya mtu kuwekwa hadharani kwa nia ovu ya kumtukana? Mkiambiwa mlikuwa nyuma ya machafuko ya October 29 mnakana.
 
Mbona amesema wazi kuwa wanaomtumia text za matusi ndiyo nguchiro? Mimi na wewe hatuwezi kuwa Nguchiro kwa sababu hatujamtumia hizo text "mentioning of one is the exclusion of others"
 
Anaandika John Heche kwenye ukurasa wake wa X:

Kama kuna mtu alikua hajui kwanini serikali hii haiwajali Watanzania, Kama kuna mtu alikua hajui kwanini watu wanatekwa, wanauwawa, kama kuna mtu alikua hajui kwanini watu hawana maji, hawana barabara, hawana shule bora, kama kuna mtu alikua hajui kwanini kodi za umma zinaibiwa na watu wakisema hawasikilizwi..

Kama kuna mtu alikua hajui kwanini watu wanaweza kuuwawa kama kuku, watu wakadhulumiwa haki zao na bado watu walioko kwenye madaraka wasijali.

Soma pia: Msemaji Mkuu Wa Serikali Gerson Msigwa awaita walipa kodi 'Nguchiro'. Ni kiburi cha aina gani hiki?

Kama kuna mtu huyo ambae alikua hajui namna Serikali hii inavyowaona na Kuwafikiria Watanzania aje asome hii kauli ya msemaji wa serikali na kwa maana hiyo kauli ya serikali.

Tanzania ni Jamhuri, maana ya Jamhuri umma au Wananchi ndio wenye mamlaka, ndio wenye nguvu… ndio maana Katiba yetu ibara ya 8 inasema mamlaka yatatoka kwa wananchi no matter how wananchi wanaweza kumuudhi Kiongozi wa umma huwezi kuwaita “Nguchiro “ tumeona kwenye Nchi nyingi tu viongozi wanakosolewa tena hata vibaya, na sheria zipo kama kuna kosa kuna hatua za kuchukua…

Msemaji wa serikali au serikali inawezaje kuita watu Nguchiro!!!!

Kumbe ndio maana mnawadharau Watanzania, mnaiba kodi zao huku wao wakiteseka, mnaua na kuteka, mnauza rasilimali za Nchi .. kwasababu hamuoni utu wao mnaona Nguchiro, hamuoni thamani yao mnaona Nguchiro!!!

Nafikiri Hii ni statement ya serikali kupitia msemaji wake na katibu wa wizara..

Watanzania msikubali dharau hizi kwenu na watoto wenu, ndio maana wakitafuta kazi hawapati kwasababu hawa wanawaona nyie sio binadamu, kwamba wao ni binadamu kuliko nyie!!!

Hakuna kiwango cha hasira au matusi kinachoweza kujustify serikali kuita raia wake Nguchiro hata kama ni mmoja

View attachment 3579557
Msigwa ni ku*ma.
 
Back
Top Bottom