Anaandika John Heche kwenye ukurasa wake wa X:
Kama kuna mtu alikua hajui kwanini serikali hii haiwajali Watanzania, Kama kuna mtu alikua hajui kwanini watu wanatekwa, wanauwawa, kama kuna mtu alikua hajui kwanini watu hawana maji, hawana barabara, hawana shule bora, kama kuna mtu alikua hajui kwanini kodi za umma zinaibiwa na watu wakisema hawasikilizwi..
Kama kuna mtu alikua hajui kwanini watu wanaweza kuuwawa kama kuku, watu wakadhulumiwa haki zao na bado watu walioko kwenye madaraka wasijali.
Soma pia:
Msemaji Mkuu Wa Serikali Gerson Msigwa awaita walipa kodi 'Nguchiro'. Ni kiburi cha aina gani hiki?
Kama kuna mtu huyo ambae alikua hajui namna Serikali hii inavyowaona na Kuwafikiria Watanzania aje asome hii kauli ya msemaji wa serikali na kwa maana hiyo kauli ya serikali.
Tanzania ni Jamhuri, maana ya Jamhuri umma au Wananchi ndio wenye mamlaka, ndio wenye nguvu… ndio maana Katiba yetu ibara ya 8 inasema mamlaka yatatoka kwa wananchi no matter how wananchi wanaweza kumuudhi Kiongozi wa umma huwezi kuwaita “Nguchiro “ tumeona kwenye Nchi nyingi tu viongozi wanakosolewa tena hata vibaya, na sheria zipo kama kuna kosa kuna hatua za kuchukua…
Msemaji wa serikali au serikali inawezaje kuita watu Nguchiro!!!!
Kumbe ndio maana mnawadharau Watanzania, mnaiba kodi zao huku wao wakiteseka, mnaua na kuteka, mnauza rasilimali za Nchi .. kwasababu hamuoni utu wao mnaona Nguchiro, hamuoni thamani yao mnaona Nguchiro!!!
Nafikiri Hii ni statement ya serikali kupitia msemaji wake na katibu wa wizara..
Watanzania msikubali dharau hizi kwenu na watoto wenu, ndio maana wakitafuta kazi hawapati kwasababu hawa wanawaona nyie sio binadamu, kwamba wao ni binadamu kuliko nyie!!!
Hakuna kiwango cha hasira au matusi kinachoweza kujustify serikali kuita raia wake Nguchiro hata kama ni mmoja
View attachment 3579557