GE2025 John Heche ampinga Rais Samia. Adai hakuna uhuru wa kufanya Siasa

GE2025 John Heche ampinga Rais Samia. Adai hakuna uhuru wa kufanya Siasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara John Heche amedai kuwa kitendo cha chama hicho kuzuiliwa kufanya siasa ni njama inayotumiwa kukikandamiza chama hicho kikuu cha upinzani.

Heche ameyasema hayo Jumatatu Juni 30, 2025 wakati akitoa taarifa kwa umma kupitia mtandaoni akisisitiza kuwa kuzuiliwa kwa chama hicho na kesi ya Mwenyekiti wake taifa Tundu Lissu vinaashiria kutokuwepo kwa uhuru wa kisiasa nchini kinyume cha kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa hivi karibuni wakati akilihutubia Bunge.

 
Back
Top Bottom