John Heche anastahili kuwa Mwenyekiti ajaye baada ya Kamanda Mbowe

John Heche anastahili kuwa Mwenyekiti ajaye baada ya Kamanda Mbowe

Tena hata sasa amechelewa. Yeye ndio alipaswa kuwa mwenyekiti hata sasa, ila Mbowe alilazimisha kuendelea kuwa mwenyekiti.
Heche alifaa sana kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA au Naibu Katibu Mkuu.

Toka wamewaweka Benson Kigaila na wenzake naona kama wamelala zaidi kuliko kawaida.
 
As if ulikuwa akilini mwangu.Naomba hata vikao vya mchujo aongoze yeye.Mbowe amevusha Chama kwenye uchaguzi wa ndani naamini ni wakati muafaka gia ibadilike tupate tone ya Kikurya kidogo.
Umeongea point mkuu
 
Anafaa lakini mimi naona kama ana jaziba hivi.
Sometimes Jazba ni muhimu sana,Mbowe busara nyingi nyingi sana ndio maana sometimes wale jamaa hua wanamzoea kidwanzi sana.
 
Tena hata sasa amechelewa. Yeye ndio alipaswa kuwa mwenyekiti hata sasa, ila Mbowe alilazimisha kuendelea kuwa mwenyekiti.
Huenda unachokisema kila uhalisia kabisa. Jamaa alipokuwa mwenyekiti BAVICHA taifa vijana CHADEMA waling'aa sana. Anastahili kuandaliwa kwa ajili ya jukumu hili zito mbele yake
 
.
Naunga mkono hoja kwa 100%.

Huyu mwamba alishawahi kumbana Magu kwny mkutano kule Tarime Magu akaishia tu kusema usinijibu hivyo, wewe ni sawa na Mwanangu,hahahah.
Bado hiyo nafasi anaweza kupewa hata wakati muhula wa Mh.Mbowe ukikamilika.Hajachelewa kupatiwa hiyo Kofia,hakuna adumuye hapa duniani.
Kiukweli CDM ni kiwanda cha viongozi mahiri,wasomi wenye upeo mpana kuhusu nchi yetu na wazalendo haswa.Mh.Heche ni miongoni mwa wengi wanaojengwa na Taasisi.
He deceive it,it's a matter of time&chance but right now wanakuwa Mbunge Tarime (V).
 
Heche ni bonge la jasiri,kukiwa na kina Heche kumi bungeni watu wangekaa kwa kujielewa.
Tuwapeleke Bungeni wagombe makini wa CDM/ACT wakaendeleleze kazi za ukombozi wa Tanzania yetu toka mikono ya mkoloni mweusi,tufanye reforms za kurejesha nchi kwenye misingi ya Haki,Uhuru ili tupate maendeleo shirikishi bila ubaguzi.Tuukatae Unyonge na Unyanyasaji wa aina yoyote.
Pia watenda Haki watatakiwa kuzingatia umuhimu wa maridhiano dhidi ya watawala waliovunja Katiba na Sheria zetu kwa wale watakaokuwa tayari kujirekebisha.Hili ni muhimu kwa sababu ndiyo hofu kuu inayowatesa CCM kiasi cha kutamani kutawala milele.
Mabadiliko hayaepukiki Sasa, tunatakiwa tuyalete kwa kutenda Haki tu.Tanzania ni yetu sote,hakuna mwenye hati miliki.
 
Huenda unachokisema kila uhalisia kabisa. Jamaa alipokuwa mwenyekiti BAVICHA taifa vijana CHADEMA waling'aa sana. Anastahili kuandaliwa kwa ajili ya jukumu hili zito mbele yake
Kitu hamtaki kuelewa nyakati za Heche siasa zilikuwa zinafanywa na vyama vyote sio kama sasa wanafanya cccm peke yao
 
Mbowe hastahili tena kubaki kwenye Kiti hata kama Chadema itashinda uchaguzi.
Itakua ni aibu kubwa kuwa na Chama Tawala kinachoongozwa na Mbowe.

Mbowe ana wivu sana.
Amekimbia Kampeni za Lisu baada ya kuona kuwa watu wote wanamkimbilia Lisu huku yeye akibaki kama Mjumbe na mshangiliaji tuu.
Media zote hazina habari na Mbowe.
Ameshindwa kujenga chama chake kwenye mkoa wake na Kanda nzima ya kaskazini Chadema imekufa kabisa tofauti na enzi za Ndesamburo.

Mbowe ni mbinafsi sana tofauti na Marehemu Ndesamburo ambaye alikua anatumia Alichonacho kujenga chama na kuhamasisha maendeleo kama kujenga mashule na kununua Computer kwenye mashule.

Nashauri tu baada ya uchaguzi huu Mbowe atimuliwe kwenye kiti Mara moja na ikiwezekana uchunguzi ufanyike ili kubaini wizi alioufanya kwenye michango na ruzuku na ujanja ujanja wote.
Mbowe kwa kweli ana hofu hata ukimtazama usoni.
 
Back
Top Bottom