Hilo la kunyimwa kukutana wala halina mjadala, na ushahidi upo. Nakumbuka zamani nikiwa mdogo nililelewa na mama wa kambo, mbali ya kunitesa sana, pia alikuwa na tabia ya kuninyima chakula. Sio kwamba alikuwa hanipi kabisa maana ningekufa, ila anaweza kunipa mara moja kwa siku, tena sio cha kushiba. Nikawa nashitaki kwa baba yangu hali hiyo. Akawa akimuona baba yangu akawa ananijazia chakula kisha anamwabia baba yangu, mtoto wako si huwa anakuambia simpi chakula, hicho hapo ni nini? Huyo John Heche kuwepo hapo kwenye mkutano, haimaanishi kuwa cdm hawakataliwi kufanya mikutano yao, tena kwa kakatazo haramu.