View attachment 3122169
Mwenyekiti wa wakati wote na wakudumu wa Chama kikuu Cha Upinzani nchini Tanzania Chama Cha Demokrasia & Maendeleo CHADEMA Mhe Freeman Aikael Mbowe huenda akung'atuka kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Taifa aliyoihudumu kwa zaidi ya miongo Mitatu mapema mwezi ujao.
Habari za chini chini toka CHADEMA zinasema huenda Mhe Freeman Aikael Mbowe akawa na imani zaidi endapo tu atakiacha chama hicho chini ya Mkurya huyo jasiri wa muda mrefu mwenye misimamo thabiti isiyoyumba wala kutetereka au kutetereshwa hasa katika kusimamia haki za Watanzania.
Duru za siasa nchini Tanzania zinasema Mhe John Heche ambae pia ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Uchaguzi la Tarime Vijijini ndio kijana pekee kati ya Vijana wote walio rithishwa nafasi ya uenyekiti wa BAVICHA( wing ya vijana) na Mhe Freema Mbowe aliyeweza kuiongoza taasisi hiyo kwa Mafanikio zaidi na kuifanya BAVICHA| CHADEMA kupata imani kubwa toka kwa makundi na watu mbalimbali hasa ya Vijana waishio nje na ndani ya Tanzania.
Taarifa zinaonesha Mhe John Heche ndio mwanasiasa pekee wa Upinzani aliyeahidiwa mambo mengi zaidi na mazuri ikiwemo nafasi ya Uwaziri na aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt John John Joseph Magufuli huku taarifa zikidokeza kuwa alikataa kata ofa zote hizo zilizoelekezwa kwake ili kuihama CHADEMA.
Mwanasiasa John Heche anatazamwa na WanaChadema walio wengi nchini Tanzania kama mtu pekee anayeweza kuhamasisha kundi kubwa la watu hasa vijana wasio na Ajira na Mafukara kujiunga na Chama hicho na hatimaye 2025 CHADEMA iweze kushinda na kuongoza Serikali | Dola 2025-2030 kupitia Uchaguzi huru na haki utakaofanyika nchini Tanzania baadae mwakani huku Upinzani mkali ukitarajiwa kati ya Tundu AM Lissu wa CHADEMA na Rais wa Sasa wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan wa CCM.
Soma Pia: Ni kweli Mbowe hawataki Lissu, Heche, Lema, Msigwa na Wenje ndani ya CHADEMA?
Mhe John Heche anayetajwa kuwa swaiba mkubwa wa Mhe Tundu AM Lissu na mwanasiasa asiye na chembe ya woga wa ama kufa ama kuishi duniani anaonekana kuwa mwiba mchungu kwa Upande wa Chama Cha Mapinduzi CCM kiasi Cha CCM kumtamani Mhe Freeman Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho kwa muhula mwingine wa miaka mitano ( 2024-2029 ) huku Lissu akisalia kuwa Makamu wake na Mgombea wa Urais 2025 kama alivyokwisha kutangaza nia yake hiyo.
Hata hivyo vijana wanaotaka mabadiliko ndani ya CHADEMA hasa wasomi wameendelea kumsihi Mhe Freeman Mbowe akae pembeni ili kupisha damu changa na zaidi sana kuionesha demokrasia wanayoihubiri nje na ndani ya Chama hicho kwa Vitendo.
Pamoja na hayo vijana wanufaika wa Bwana Freeman Mbowe kama ilivyokuwa kwa vijana wa Hayati Mwl Julius Nyerere walivyomgomea Mwl Nyerere kung'atuka madarakani kwa kisingizio kuwa Nchi ni changa ndivyo hivyo ilivyo kwa vijana wa Mhe Freeman Mbowe leo wanamwambia kuwa asithubutu kuachia Chama kwa sasa kwani chama bado ni kichanga sana huku baadhi yao wakiwatazama wao na familia zao kuwa ndio wachanga ila si CHADEMA huku chama hicho kikiendelea kuzorota siku baada ya siku kiasi Cha wanachama kugoma hata kuandamana jambao ambalo halijawahi kushuhudiwa tangu kuasisiwa kwa Chama hicho nchini Tanzania chini ya mamlaka hizo hizo za Serikali ya Tanzania.
Mhe John Heche anatajwa kama kijana mwenye mvuto zaidi ndani na nje ya CHADEMA kwa Sasa na huenda ndio mtu pekee atakayeweza kumwangusha Mhe Freeman Mbowe kwenye sanduku la kura mapema mwezi ujao endapo tu Mhe Freeman Mbowe atasalia kuwa king'ang'anizi wa kiti hicho kwa miaka mingine mitano ili kutimiza mihula sita inayofanya jumla ya miaka 30 Uongozini akivunja rekodi ya Hayati Augustino Mrema aliyefia madarakani.
[CHADEMA tunawatakia kila lenye heri kuelekea uchaguzi wenu huu Mkuu wa Chama na Serikali sisi tusio na chama tunahitaji kuona Upinzani imara ili kujenga Serikali madhubuti ya Tanzania]
View attachment 3121911
Mhe John Heche Mwenyekiti Mtarajiwa wa CHADEMA 2024-2029