Pre GE2025 John Heche kumuunga mkono Lissu asema Lissu ni mkweli, muwazi na muadilifu sana

Pre GE2025 John Heche kumuunga mkono Lissu asema Lissu ni mkweli, muwazi na muadilifu sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Rula ya Mafisadi

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2024
Posts
404
Reaction score
852
==
Mhe John Heche anasema yeye waziwazi anamuunga mkono Mhe Tundu Lissu kwa sababu ni mtu mkweli sana ni muadilifu sana na anachukia rushwa kwa moyo na nguvu zake zote.

Mhe John Heche ilitarajiwa na wengi kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa lakini baada ya Mhe Tundu Lissu kuamua kugombea yeye ameamua kumpisha Tundu Lissu kwani anaamini nafasi hiyo ya Uenyekiti anaiweza zaidi na ndio sababu ya kumuunga mkono.

Mpaka sasa haijafahamika kama John Heche atagombea nafasi yoyote ndani ya chama au atabaki pembeni kumuunga mkono Tundu Lissu,

Tusubiri tuone mpaka hiyo tarehe 05.01.2025 ambae ndio mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu Kwa mujibu wa kalenda ya Uchaguzi ya chama.

IMG-20241231-WA0092.jpg


==
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (@ChademaTz), @HecheJohn, ameonesha dhamira yake ya kuendelea kupigania mustakabali wa chama hicho na Taifa kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) leo Jumanne Desemba 31, 2024,
Heche ameandika ujumbe mzito akisisitiza umuhimu wa CHADEMA kama taasisi muhimu kwa maslahi ya taifa na wananchi wa Tanzania.

"Tuna taasisi ya kuilinda, tuna nchi ya kutetea, tuna Watanzania wa kupigania. CHADEMA ikifa madhara yake ni makubwa mno kwa nchi yetu," aliandika Heche.

Katika ujumbe huo, Heche amemuelezea mwanasiasa mashuhuri na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara @TunduALissu, kama kiongozi mwadilifu, mkweli, na mwenye uwazi wa hali ya juu.

"Lissu sio muongo ni mkweli, muadilifu na muwazi," aliandika, akionesha imani yake kubwa kwa Lissu.

Lissu, ambaye kwa sasa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ameendelea kuungwa mkono na viongozi na wafuasi wa chama hicho.

Uchaguzi wa nafasi hiyo unatarajiwa kufanyika tarehe 21.02.2025.
 
John Heche asema atamuunga mkono Tundu Lissu kwa sababu ni mkweli sana ni muadilifu sana na anachukia rushwa sana
View attachment 3189380
AMESHAJICHIMBIA KABURI KWA MTU AMBAYE HATASHINDA UENYEKITI SIJUI WATAKIMBILIA WAPI MBOWE HANA CHA KUPOTEZA AKISHINDA HATA CHAMA KIKIFA HANA SHIDA ATAKUWA AMEWANYOOSHA HAO WANAOMKATAA SASAHIVI
 
Mbowe alitamani sana kuachia uenyekiti wa Chama kwa heshima na aendelee kuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati nyeti. Ila sasa, machawa ambao hawawezi kusurvive bila yeye na baadhi ya watu ndani ya mfumo either wamemconvince aendelee kubaki au wamemtisha kwamba maslahi yake yatakuwa shakani kama ataachia kiti

Hata kama Mbowe atashinda kiti, heshima yake kwa jamii na imani ya wananchi wapenda mabadiliko wasio na kadi za chama chochote cha siasa (ambao ni wengi sana) itapotea kwa Chadema na CCM haitohitaji kuiba kura nyingi hapo October 2025
 
Mbowe alitamani sana kuachia uenyekiti wa Chama kwa heshima na aendelee kuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati nyeti. Ila sasa, machawa ambao hawawezi kusurvive bila yeye na baadhi ay watu ndani ya mfumo either wamemconvince aendelee kubaki au wamemtisha kwamba maslahi yake yatakuwa shakani kama ataachia kiti

Hata kama Mbowe atashinda kiti, heshima yake kwa jamii na imani ya wananchi wapenda mabadiliko wasio na kadi za chama chochote cha siasa (ambao ni wengi sana) itapotea kwa Chadema na CCM haitohitaji kuiba kura nyingi hapo October 2025
Aisee itawagharimu sana
 
AMESHAJICHIMBIA KABURI KWA MTU AMBAYE HATASHINDA UENYEKITI SIJUI WATAKIMBILIA WAPI MBOWE HANA CHA KUPOTEZA AKISHINDA HATA CHAMA KIKIFA HANA SHIDA ATAKUWA AMEWANYOOSHA HAO WANAOMKATAA SASAHIVI
Nakuomba Erythrocyte usije kutumbukia shimoni kama Heche. Sisi na Mbowe hadi kieleweke ili ajira yako uilinde
 
Back
Top Bottom